Danny Lyanga ni Samatta Mpya Msimbazi

Danny Lyanga ni Samatta Mpya Msimbazi

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
Kama kuna watu wazuri wa kumbukumbu wautunze uzi huu akilini mwao lakini amini usiamni straika ambaye hatajwi sana Danny Lyanga ndiye tishio zaidi kwenye safu mpya ya ushambulizi katika usajili wa msimu huu

nimemuangalia kwa makini anahitaji vitu vichache sana kuweza kucheza kwa kiwango cha juu na kuwika hatimaye kuwa tegemeo si tu kwa simba bali hata timu ya Taifa.

My best wishes goes with him!
5.jpg

Danny%2BLyanga1.jpg

ndo namsikia toka kwako, katokea timu gani na ana umri gani?
 
wewe utakua si mtu wa mpira

Ni mtu wa mpira sana, ni kwamba toka VPL imeisha sijafuatilia usajili hapa bongo unaendaje!
Okei, nimeiona picha yake, anaonekana ni dogo na kwa Simba, yuko timu sahihi kabisa, maana Simba ndo timu pekee inayotengeneza na kukuza vipaji vya yosso ikifuatiwa kwa mbali na Azam.
 
Amna mchezaj umo kk m nmemuona dhidi ya villa

Huwezi muona mchezaji ktk mechi moja ukafikia tamati kuwa hajui,ndio maana mtoa mada anasema kama anapewa muda na ushirikiano ni bonge la hadhina pale msimbazi,umemuona the next match kama una jicho la tatu ktk ushambuliaji alitakiwa kuwa the man of the match
 
Danny Lyanga ni nani?

1. Kazaliwa 28/07/1991 (miaka 24) jijini Arusha

2. Baada ya kucheza soka kwa kiwango cha juu kabisa mitaani, msimu wa 2010/2011 akiwa na miaka 19 tu, alitua timu ya Arusha FC na kuingia moja kwa moja 1st eleven, ambapo rekodi yake ya kutupia magoli ni ile ile kama ya Mavugo.. Mechi moja, Goli moja au zaidi.

3. Kutokana na kuonesha kiwango bora msimu uliofuata alitua Coastal Union, ambapo alicheza misimu miwili. Msimu wake wa mwisho alitupia goli 7, na goli la mwisho kufunga lilikua katika uwanja wa Mkwakwani dhidi ya timu yako (Azam FC) na gemu iliisha 1-1.. Na siku hiyo Yanga wakatangaza ubingwa wakiwa na mechi mbili mkononi.

4. Msimu uliofuata, alijiunga DC Motema Pembe.. na hii ni baada ya kuzipiga chini Simba, Ndala na Azam.

5. Msimu uliopita, mkataba wake umeisha.. Hivyo anatua Simba SC akiwa huru.

KARIBU SANA SIMBA SC.. Danny Lyanga.

Waione Amavubi barafuyamoto na Masuke
 
Last edited by a moderator:
ndo namsikia toka kwako, katokea timu gani na ana umri gani?

Mkuu, Danny alitoka Machava United ya Moshi akaenda Coastal Union msimu wa 2012/2013 kama sikosei. Ni mmoja wa wachezaji wazuri wataratibu na wasio na makeke mengi uwanjani... Nimemuona kwa kuwa alikuwa timu niliyokuwa naifanyia kazi.

Msimu wa huo alifunga goli moja sumu dhidi ya Mtibwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, goli ambalo Shaffih Dauda alilitaja kuwa goli bora la wiki: Shaffih Dauda in Sports.: BAO LA WIKI VPL: DAN LYANGA vs MTIBWA SUGAR.

aione: sembo
 
Last edited by a moderator:
Jamaa anajitahidi mtulivu yuko makini makosa yake ni machache sana yanarekebishika!anamiliki mpira vizuri na kushirikiana na wenzie vizuri nilimtazama mechi na ura ila aongeze kasi kidogo .
 
Mkuu, Danny alitoka Machava United ya Moshi akaenda Coastal Union msimu wa 2012/2013 kama sikosei. Ni mmoja wa wachezaji wazuri wataratibu na wasio na makeke mengi uwanjani... Nimemuona kwa kuwa alikuwa timu niliyokuwa naifanyia kazi.

Msimu wa huo alifunga goli moja sumu dhidi ya Mtibwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, goli ambalo Shaffih Dauda alilitaja kuwa goli bora la wiki: Shaffih Dauda in Sports.: BAO LA WIKI VPL: DAN LYANGA vs MTIBWA SUGAR.

aione: sembo

Haha.. Sawa Mkuu Mphamvu nimeiona.
 
Last edited by a moderator:
Danny Lyanga ni nani?

1. Kazaliwa 28/07/1991 (miaka 24) jijini Arusha

2. Baada ya kucheza soka kwa kiwango cha juu kabisa mitaani, msimu wa 2010/2011 akiwa na miaka 19 tu, alitua timu ya Arusha FC na kuingia moja kwa moja 1st eleven, ambapo rekodi yake ya kutupia magoli ni ile ile kama ya Mavugo.. Mechi moja, Goli moja au zaidi.

3. Kutokana na kuonesha kiwango bora msimu uliofuata alitua Coastal Union, ambapo alicheza misimu miwili. Msimu wake wa mwisho alitupia goli 7, na goli la mwisho kufunga lilikua katika uwanja wa Mkwakwani dhidi ya timu yako (Azam FC) na gemu iliisha 1-1.. Na siku hiyo Yanga wakatangaza ubingwa wakiwa na mechi mbili mkononi.

4. Msimu uliofuata, alijiunga DC Motema Pembe.. na hii ni baada ya kuzipiga chini Simba, Ndala na Azam.

5. Msimu uliopita, mkataba wake umeisha.. Hivyo anatua Simba SC akiwa huru.

KARIBU SANA SIMBA SC.. Danny Lyanga.

Waione Amavubi barafuyamoto na Masuke

Uwe consistent: unapotaja Simba au Azam ni sharti utaje Yanga pia. Endapo utaamua kutumia nick names mfano ndala (Yanga) basi utumie 'mikia' kwa Simba na 'lambalamba' kwa Azam.

Sasa kama aliipiga chini mikia na sasa karudi, huoni kwamba kalamba matapishi yake mwenyewe?
 
Haya majina mengine hatari sana

Huku kitaa chetu, Lyanga ni kupiga kavu
 
5. Msimu uliopita, mkataba wake umeisha.. Hivyo anatua Simba SC akiwa huru.
Kama alikuwa in mzuri kiasi cha inavyosimuliwa, kwa nini Motema Pembe wasimwongezee mkataba? Alikataa ili awe huru kujiunga na timu za Ulaya zitapomuhitaji? Kuja Simba ambayo haichezi michuano yoyote ya kimataifa kunaendana na dhana hi you? Akili za kuambiwa ongeza na zako.
 
Back
Top Bottom