Msimamo wa ligi kuu bara Msimu uliopita ulikua hivi;
View attachment 278434
Nichoking'amua hapo juu ni kua;
1. Pamoja na Ndala kuwa na mabeki + makipa bora kabisa nchini ambao ni tegemeo pia timu za Taifa, waliruhusu kufungwa goli 18, sisi tuliokua na beki ambayo haijazoea ligi, vijana, tuliruhusu goli 19.
Msimu huu Mtalamu Kerr katujengea Great Wall Of China.. Sidhani kama kuna beki atakua na udhibiti wa kupita.. Atakaye jaribu asije sema hatukumuonya.
2. Safu ya ushambuliaji ya Ndala ilikua moto msimu uliopita, na hii ni baada ya sisi kuwauzia bunduki yetu.. Safu yao ilifunga goli 58, ukitoa magoli ya bunduki tuliyowapatia.. Sidhani hata kama wangetuzidi kwa wingi wa Magoli.
Msimu huu tumejifunza kitu, ili kuongeza idadi ya magoli ya kufunga tumewaleta Kiiza, Mgosi, Mwalyanzi na yule mshambiliaji kiboko ya mabeki visiki Emily Ndayisenga.
"When you talk about this new striking force, you means dozen of goals in a single match" - sembo