Teko Modise
JF-Expert Member
- May 20, 2017
- 2,331
- 7,733
Hii imetokea mtaa wa Lumumba, haifahamiki kulikuwa na nini?
Jamaa walikuwa wamekunjana kama ugomvi katikati ya kundi la watu.
Hamadiii, difenda ya polisi yawasili na askari kuanza kupiga risasi hewani.
Jamaa mmoja (mwanaume wa dar ) anakamatwa na kuanza kula makofi kisha anapakiwa kwenye gari la polisi.
Basi akaruka upande wa pili na kuanza kukimbia, kutokana na maaskari kushika bunduki wakashindwa kumkimbiza.
Basi akatokea askari mmoja nyuma kabisa tena akiww amevaa uniform (kachomekea) akamkimbiza jamaa na kumdaka kirahisi.
Najua huko alipo huyo jamaa kwasasa atataja mpaka jina la utotoni la mzee mpili.🤣🤣.
My take:
Wanaume wa Dar, fanyeni mazoezi acheni kufakamia chips.