DAR: Akram Aziz akamatwa, afikishwa Mahakama ya Kisutu. Ana makosa 75!

DAR: Akram Aziz akamatwa, afikishwa Mahakama ya Kisutu. Ana makosa 75!

Watanzania tuamke!!! Mazingira haya yametengenezwa tu, kama taarifa ya mwanzo ilivyosema kua "askari wamemkamata akiwa na vibali sahihi, ila wakaamua kuondoka navyo vibali vyote original na kukataa kuacha copy ofisini kwake". Hapa kama kawaida, serekali inatuhamisha toka maswala fulani kutupeleka kwengine. Tumeshafanywa kama watoto wa chekechea sasa!!!

Watanzania lini tutapata akili jamani ya kuchanganua mambo na ukweli????? Tulishuhudia YUSUF MANJI alikamatwa na akafikishwa mahakamani kwa kukutwa na NYARA ZA SEREKALI, MIHURI YA JESHI, VITAMBAA VYA SARE ZA JESHI. Case iliishia wapi?????? Nani anaehoji mpaka sasa kuhusu hio tuhuma zake au case alizoshitakiwa nazo?????? Kama kweli angeachiwa huru????

Inasikitisha sana kuona mtu akitetea uonevu unaofanywa na askari kwa raia, na uongo tunaopewa raia na serekali yetu, kama huu na iliopita.

Na inasikitisha zaidi kuona wafanya biashara wakubwa wakionewa mpaka kufikia hatua wanafunga biashara zao na watanzania wenzetu kibao wanakosa ajira.

Kwahio unamtetea mtuhumiwa wa ujangili?

Si uachie mahakama iamue kama ni jangili au sio jangili?

Mtu ana makosa 75 wamtetea kweli, unayafahamu hayo makosa?
 
Umeandika mavi kabisa,kwahiyo mtu aliyefanikiwa hata akifanya makosa asiadhibiwe.
sijasema asiadhibiwe, nimesema hivi "HUWEZI FANIKIWA KWA KUMCHUKIA YULE AMBAYE AMEKWISHA FANIKIWA" hii ni baada ya kuona uvccm wengi mmekuwa mkishangilia pale mnaposikia mtu fulani mwenye pesa anatuhuma. hata mahakama haijamtia mtu hatian nyie mnapiiga vigelegele
 
ni kwa sababu wana fikra kondefu. jinsi wanavyoshabikia chama au vyama wanajua watanzania wote ni mandondocha ya kichama. wanasahau kuna wachache bado wana akili timamu ambazo hazijawa corrupt na vyama. kuna watu tunaangalia maslahi ya tanzania na si vyama.
 
inawezekana hata huelewei mlipa kodi ni nani.. maana hili swali lako linaonesha utakuwa darasa la saba au umemaliza kidato cha nne. mtu msomi mwelewa hawezi uliza swali kama hili. unamuuliza mtu analipa kodi tsh ngap? we hata unafahamu kodi ni nini kweli?
 
Safi sana. Wanyama wetu wapone sasa. Nauliza hiviii Nyarandu atapona kweli kwenye hii muvi? Nasubiri.
 
Safi sana JPM. Majizi yote mpaka yale ya EPA, ESCROW etc bado tunasubiri zamu yao ifike. Usibague
 
Hakuna mharifu mjinga ambaye anaweza kaa na ushahidi kwake
 
Kwahio unamtetea mtuhumiwa wa ujangili?

Si uachie mahakama iamue kama ni jangili au sio jangili?

Mtu ana makossa 75 wamtetea kweli, unayafahamu hayo makosa?
Mbona mlivomweka ndani Yusuf Manji mlisema amekamatwa na Mihuri ya Jeshi, Sare za jeshi na vitambaa vya sare za jeshi??? Yalikua mashtaka ya kweli haya??? Na kama ya kweli yameishia wapi mbona hajafungwa???? Au ulikua uonevu???
 
Mbona mlivomweka ndani Yusuf Manji mlisema amekamatwa na Mihuri ya Jeshi, Sare za jeshi na vitambaa vya sare za jeshi??? Yalikua mashtaka ya kweli haya??? Na kama ya kweli yameishia wapi mbona hajafungwa???? Au ulikua uonevu???

Mimi na wewe hatufahamu hayo.

Huenda ameonyesha stakabadhi ya hivyo vifaa kwamba amenunua nje ya nchi na havikupatikana hapahapa Tanzania, na kisha wakamwachia.

Ndo maana hakufikishwa mahakamani na kumalizana na jeshi na polisi, who knows?

Yaani kwa kifupi sisi raia hatufahamu chochote ila hatuwezi kulaumu polisi kwa kila kitu kwa vile tu imejengwa picha mbaya juu yao.
 
Dq1nItwWkAEFMqT.jpg

Mfanyabiashara Akram Azizi Abdul Rasool ambae ni mdogo wa Rostam Aziz amefikishwa Mahakamani Kisutu akikabiliwa na makosa 75 ikiwemo kukutwa na Nyara za Serikali na utakatishaji fedha U.S.D 9018, upelelezi haujakamilika hivyo amerudishwa rumande, kesi imeahirishwa hadi Nov 12.
 
Duh, maskini kazi yetu kushangilia kila tajiri anaponyanyaswa, lakini hamkumbuki maisha yetu yameshikwa na huyo tajiri. Tunashangilia ujinga, uonevu na kila aina ya dhulma inayofanyika kwa matajiri. Iko siku nyuma huu mchezo siri iliyojificha itafunuliwa!!
 
Mimi na wewe hatuwezi mjuwa aliyefanikiwa, ni kujidanganya tu machoni na moyoni
Kweli akili zako ndogo, eti mimi na wewe hatuwezi kujua aliefanikiwa? Kweli unafikilia kutumia nini? Hauwezi kupata chakula, kwa kumchukia aliekula!!
 
Nadhani ni katika harakati zinazoendelea nchini dhidi ya nyie mliofanikiwa kimaisha kwamba ni wakati wenu sasa muishi kama mashetani!
So kweli kabisa. Wengi wanaotaka tuamini wamefanikiwa hawasemi wametumia njia gani kupata hayo mafanikio.
Kufanikiwa kwa sababu ya kuwa jangili sio mafanikio....kuiba hela za wananchi kwa rushwa na ufisadi sio mafanikio.
Leo hii wengi waliotumia nafasi zao kwa dhuluma wanaona sifa tuwanyenyekee kama role model wa mafanikio.
Naamini katika haki. Kila mtu avune anachopanda. Ukweli peke yake ndio utatuweka huru
 
Duh, maskini kazi yetu kushangilia kila tajiri anaponyanyaswa, lakini hamkumbuki maisha yetu yameshikwa na huyo tajiri. Tumashangilia ujinga, uonevu na kila aina ya dhulma inayofanyika kwa matajiri. Iko siku nyuma huu mchezo siri iliyojificha itafunuliwa!!
Dhulma gani amefanyiwa huyo tajiri?
 
Back
Top Bottom