Watanzania tuamke!!! Mazingira haya yametengenezwa tu, kama taarifa ya mwanzo ilivyosema kua "askari wamemkamata akiwa na vibali sahihi, ila wakaamua kuondoka navyo vibali vyote original na kukataa kuacha copy ofisini kwake". Hapa kama kawaida, serekali inatuhamisha toka maswala fulani kutupeleka kwengine. Tumeshafanywa kama watoto wa chekechea sasa!!!
Watanzania lini tutapata akili jamani ya kuchanganua mambo na ukweli????? Tulishuhudia YUSUF MANJI alikamatwa na akafikishwa mahakamani kwa kukutwa na NYARA ZA SEREKALI, MIHURI YA JESHI, VITAMBAA VYA SARE ZA JESHI. Case iliishia wapi?????? Nani anaehoji mpaka sasa kuhusu hio tuhuma zake au case alizoshitakiwa nazo?????? Kama kweli angeachiwa huru????
Inasikitisha sana kuona mtu akitetea uonevu unaofanywa na askari kwa raia, na uongo tunaopewa raia na serekali yetu, kama huu na iliopita.
Na inasikitisha zaidi kuona wafanya biashara wakubwa wakionewa mpaka kufikia hatua wanafunga biashara zao na watanzania wenzetu kibao wanakosa ajira.