Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tuacheni kutetea maovu , mtu anakamtwa na meno ya Tembo tena vizibiti vipo tunasema ameonewa eti kwa kuwa ni tajiri au kwa kuwa anapingana na serikali iliyopo madarkani, watanzania mbona tuko down sana kiasi hiki? kweli mtu kakamatwa na uwindaji haramu tuna sema serikali inanyanyasa matajiri? wangapi wamekamatwa Tanzania hii kwa uwindaji haramu na wako huko wanasubiri kesi zao? kama ameonewa mahakama ipo itatoa hukumu, lakini sio tuache kuchukua hatua pindi watu wanapokuwa na hatia, tunataka kujenga taifa la ajabu sana kisa eti tunataka huyo tajiri aliyekamatwa tumtetete hapa tumchonganishe na serikali ili akitoka basi aungane nasi katika vyama vyetu kisa tupate misaada ya ufadhili, siasa ni mbaya sana tukiicha iwe katika akiri zetu muda wote maana kila kitakachokuwa kinatokea hapa nchini baada ya kujadili in a facts way tunalichukulia ni suala lakutafutia wafuasi, lets the government do the work, kuna mahakama zitaamua, ndio maana mimi nasem serikali iliyopo itakuwa ngumu sana kuyatoa, maana yanazidi kupata uungwaji mkubwa wa watu na kujiweka katika mazingira mazuri kwa kipindi kijacho,wanacheza na agenda zao vizuri, rushwa, ujangili,madawa ya kulevya na kadhalika, sisi tunadharau lakini wenzetu ndo wanakimbia hivyo.
Hii siyo stori ya Musiba kweli hii?Habari Mpasuko: Mtandao Ndugu wa Rostam, Zitto Wanaswa
Kuna habari huenda ikaripuka wakati wowote ya kukamatwa ndugu wa Rostam aitwae Ikram kwa kuhusika na ujangiri.
Huyu jamaa amekuwa akimiliki silaha na kuendeleza ujangiri nchini kwa manufaa ya wakubwa wengine walioko nyuma yake wa wenye maslahi flani.
Tetesi zinasema Mbunge Zitto Kabwe naye huenda yumo katika mtandao wa kunufaika na nyara hizo.
Taarifa kamili itawajia punde. Chini ni baadhi ya silaha na nyara hizo haramu.
Nani amekataa kuwa srikali ndo inatoa je una uhakika serikali imempa kibali Cha kuwinda utitiri wa hao wanyama hapo.Swali lako ni zuri, ni serikali yenyewe ndio inatowa vibali vya uwindaji wa wanyama, Simba, tembo, chui, nyati na wanyama wengine.
Dhulma tu,nawajua hawa jamaa kitambo sana ,wameua tembo ile mbaya pori la mpembambazi,simba ,chui,
Kungekuwa na jangili ambaye ni upinzani longtime angeshadakwa. Na wenyewe si wanatambuwa hilo?Ndiyo maana hata siku moja siwezi kukubali kuwa sapota wa ccm, kwasababu hawana nia njema na hii nchi. NEVER EVER!Huyu bwana Akram ni kada na mdogo wake aliyekuwa mbunge kipenzi wa CCM, kwa taarifa yenu CCM ndio ujangili wenyewe na ujangili ni CCM.
Kama kuna mtu ana uwezo wa kusimama kututajia majangili wawili 2 wakubwa ambao sio CCM asimame ahesabiwe.
Kuna mbunge wa Mbalali na familia yake wanatuhumiwa kwa ujangali na anaweza kukamatwa tu siku atakapo acha kuunga mkono.
HUWEZI FANIKIWA KWA KUMCHUKIA ALIYEKWISHA KUFANIKIWA
+1Mpaka sasa tunakamata waliopenya na kwenda kuiba lakini tunawaacha walioruhusu nakuachia njia watu waende wakaibe, halafu unasema unapambana na Ufisadi wakati hao watu bado wana kadi za chama na wako uraiani.
Anawanyoosha au kaomba hela ametolewa nje ? Na kumteka kama Mo anaona ata aibika ? Hivi mahakama ya mafisadi ina nini ?Hapa ndipo huwa nakuwa upande wa JPM wa kuwanyoosha mafisadi
Hata kuandika siku hizi huwezi unavizia kuingia JfNi ndugu was Rostam..I believe
Huyu naye mshamba sana, hakusoma alama za nyakati kama kaka yake.
Kale kausemi wataishi kama masheteni Rostam alikakimbia alijua watapata tabu sanaaa wacha tumnase kwa mlango WA nyuma maana serikali ina mkono mrefu ukikosa kukuteka unakutaja Muuza Unga ukikimbia list ya Unga unahujumu uchumi mradi lazima tugawane gawio lako au maduhuli yetu tuchukue wenyewe.new movie has been started.Kwa wana JF,
Natambua kuwa kuna threads 2 humu; ila taarifa ni kuwa Akram Aziz ambaye ni mdogo wa Mbunge wa zamani wa Igunga, Ndg. Rostam Aziz, ni kweli alikamatwa na Vyombo vya Dola na mchana huu amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu.
View attachment 917003
Kwa kuanzia, ana makosa takribani 75 ambayo anahusishwa nayo. Kuna utakatishaji fedha/uhujumu uchumi na kukutwa na nyara za serikali pia katika makosa hayo.
View attachment 917001
View attachment 917002
Kwa Taarifa za awali, Soma => Akram Aziz adaiwa kukamatwa na nyara za Serikali... - JamiiForums
Hata kuandika siku hizi huwezi unavizia kuingia Jf
umeona mkuu?Kawa kiumbe wa hovyo sana! You don't need a brain once a ccm member. Huo ni ukweli. Siku hizi hata hana hoja ya kuandika, hakuna thread anaanzisha ya maana. Sasa sijui alikuwa na yeye ni mtu wa kupinga tuu?Hata kuandika siku hizi huwezi unavizia kuingia Jf
Lakini ndio UFISADI (kleptocracy) wenyewe huo. Sisi hoja yetu ni kwamba kama kweli Mhe JPM anapigana vita dhidi ya ufisadi kwa dhati (na sio kwa chati) na kufukua makaburi ya ufisdai, basi na hilo kaburi asiliache kando bila kujali ni nani na nani walishiriki (awe Nkapa, Sumaye, na kiranja aliyepewa kazi ya kusimamia utekelezaji). Vinginevyo tutaendelea kuona futuyis at work!!Alijibu Sumaye, Yale yalikuwa maamuzi ya baraza la mawaziri wakiongozwa na Mzee Nkapa
Mfanyabiashara mkubwa wa Utalii na uwindaji Akram Azizi ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Kilombero North Safaris jana mchana alivamiwa na askari wakiwa na maofisa wananyamapori, akituhumiwa kuwa kontena lililosheheni nyara za taifa kinyume cha sheria zikiwamo pembe za ndovu, ngozi za chui na simba.
Baada ya upekuzi huo ulioanzia ofisini kwake na kisha kuhamia nyumbani kwake Masaki, askari hao hawakukuta kontena hilo wala ngozi za simba na chui kama walivyodai kutonywa.
Saa 20 baada ya kufanyika kwa kazi hiyo ambayo iliendeshwa huku watu wakizuiwa kuingia au kutoka katika maeneo hayo mawili, kumeanza kusambazwa picha mitandaoni zikiambatana na maelezo ya kumhusisha Mfanyabishara huyo wa Utalii wa Uwindaji (Akram Azizi) na tuhuma za ujangili zinaonekana kulenga kutia doa kazi halali na ya kisheria anayofanya, sambamba na kuilenga familia yake na watu wengine wenye undungu naye.
Picha hizo zimepigwa nje ya ofisi yake inayoitwa Kilombero Hunting Safaris na si nyumbani kwa Akram kama inavyoelezwa katika taarifa zinazosambazwa.
Bunduki zinazoonekana kupangwa katika picha hizo, zote ni za kampuni hiyo ya uwindani na utalii ambayo yeye Akram mkurugenzi wake na si za mtu binafsi na zote zimekutwa zikiwa na vibali vyote halali.
Katika upekuzi huo zimekutwa pembe sita za ndovu ambazo zina mihuli na vibali vyote vya serikali na pembe zote zina ‘serial numbers’ zikionyesha zilipatikana mwaka 2014. Hii ni kwa mujibu wa sheria.
Kisheria watu au makampuni yanayotaka kununua pembe za ndovu wanatakiwa kupata vibali serikalini na kwenda kununua ktk kampuni halali na zenye usajili kama hiyo ya Akram.
Upekuzi uliofanyika nyumbani kwake haujakuta kitu chochote tofauti kabisa na inavyotaka kuonekana katika taarifa za awali mitandaoni.
Hakuna anayepinga au kuhoji mamlaka halali za serikali kuhoji mtu kisheria, kinacholeta shida ni hatua ya watu wasiojulikana kusambaza kwa makusudi picha ambazo zinaambatanishwa na taarifa potofu ambazo kwa hakika malengo yake hadi sasa hayajawa bayana.
Wanasheria wa Akram wanashtushwa na bado wanaendelea kufuatilia ili kujua maana hasa ya hatua ya askari waliofanya ukaguzi huo kuondoka na hati zote halisi ‘originals’ na vibali vya umiliki wa silaha na hizo pembe za ndovu.
Askari hao ambao wanatokea Idara ya Maliasili na Polisi walipofika ofisini kwa Akram jana walidai kwamba, taarifa walizoambiwa ni kuwa kuna ngozi za simba, chui na nyara nyingine za serikali vitu ambavyo baada ya upekuzi mkali wa kushtukiza hawakuvikuta.
Kitendo cha kuondoka na vibali halali vyote na kuvizuia na kukataa kuacha nakala za nyaraka hizo na kitendo cha kuanza kusambaza taarifa mitandaoni kwa taswira ya upotoshaji kumetafsiriwa na wanasheria wa Akram na wa kampuni ya Kilombero North Safaris kuwa yenye nia ya kuandaa mazingira ya kutenda dhuluma.
Ahsante
Kilombero North Safaris
Dar es Salaam
31st October 2018
Hahahaa!! Hivi thamani ya Vodacom Tanzania kwa sasa ni shilingi bilioni mia ngapi?! The question is: Mmiliki wa takribani 26% ya hayo mabilioni atakuwa tayari kumuona kaka yake anaozea jela kwa kesi ay tumilioni kadhaa?! Kaka ambae kwa namna moja au nyingine huwa anamtumia kwenye biashara zake kama ile ya kummilikisha tone la kampuni inayomiliki 26% ya Vocadom Tanzania!
Btw, yupo ndani au yupo nje kwa dhamana? Manake kwa hizo tuhuma anatakiwa kuwa ndani kwa sababu, mathalni kesi ya uhujumu uchumi nadhani haina dhamana!!!