Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Duuuuu!!
Usishangae..
Hawa ndo wahujumu uchumi wakubwa ambao wana say kwenye serikali yoyote ile.
Pengine hata serikali ya upinzani ingeingia madarakan raisi wake angeitwa na kuambiwa atulize mpira.i
Hao ndo humfadhili na humuita raisi aingiae madarakani,wakamkalisha chini na kumwambia atulize mpira awaache wao waendelee na shughuli zao.
Raisi JPM amekataa jambo hilo (na amelisema mara nyingi) na wakaanza kufanya vurugu za chinichini huku wakilalama bishara zao zinayumba.
Hawa ndo miaka ya nyuma walikuwa askari wakitumwa kuwakamata wanawekwa kati na kukabidhiwa bahasha ndefu za khaki, kisha wanatuliza mpira.
Hawa ndo walikuwa wakiikwepa sheria ya uhujumu uchumi na kuonekana haipo kiasi cha watu wengi kusahau sheria ipo na kwamba ipo "live" na yafanya kazi.
Yasadikiwa kuwa hawa hutumia vibaya vibali vyao vya uwindaji kwa kuua tembo wadogo na wanyama wadodgowadogo badala ya kutafuta aina za wanyama wakubwa ambao wanaruhusiwa kwenye vibali vyao.
Je wafahamu athari za kuua Wanyama wadogowadogo kwenye mbuga zetu na mapori?
Msiwatete majangalili maana hata William mwanamfalme wa Uingereza, alipokuja Tanzania mapema mwezi huu aliulizia jitihada za serikali zimefikia wapi za kudhibiti ujangaili nchini.
Hivyo tuiamini serikali, tuiache ifanye kazi zake kuwashughulikia majangili na wahujumu uchumi kwa umakini bila kutetereka na mwisho tutachambua mchele ni upi na pumba ni zipi.