DAR: Akram Aziz akamatwa, afikishwa Mahakama ya Kisutu. Ana makosa 75!

DAR: Akram Aziz akamatwa, afikishwa Mahakama ya Kisutu. Ana makosa 75!

Me kitu ambacho huwa nashindwa kuelewa ni pale tu tunapojuzwa alfa lkn omega hatuambiwi kuwa imeaMriwa vp
 
Mkuu na maovu yanayofanyika kwenye box la kura ili ccm ishinde tutakuona ukikemea pia?

Kaka Tindo , maovu ni maovu tu tusisite kukemea ili tuwe na taifa la wawajibikaji, sichukii mtu wala chama Fulani ,lakini tafiti ndani na nje ya nchi zote zinaonyesha kuwa rushwa ni chanzo kinacho angamiza mataifa mengi ya Africa,rasilimali zilizopo Africa zinatumika isivyo halali ,kama mtu amepatikana anaweza jaribu kuzuia hili hata kwa asilimia chache bila kujali itikadi zetu kwa nini nisiinge mkono,mimi sikubaliani na ovu lolote bila kujali limefanywa na nani au na chama kipi, hivyo serikali ifanye kazi yake na kama mtu anaona hajatendewa kuna upande mwingine wa kutafuta haki.
 
Tulianza na Mohammed Enterprises, sasa Rostam Aziz. Sijui baadae nani. Ila sijui kama akina Kazibure watakuwemo kwani hawa ni wazalendo halisi huwa wanachota vijisenti tu alafu na ubunge juu na uenyekiti mjengoni.
 
Shida hapa sio kufanikiwa! Shaka inakuja paleee..... umefanikiwafanikiwaje!!.
Nadhani ni katika harakati zinazoendelea nchini dhidi ya nyie mliofanikiwa kimaisha kwamba ni wakati wenu sasa muishi kama mashetani!
 
Huyu ndie yule wa madawa ya kulevya yaliyokamatwa kabuku. kesi yake iliisha kwa 'mishemishe' awamu ya 4! pambaf! misi kuba hii!
 
Ni Tanzania pekee ambapo Mtu baada ya Kuikosoa Serikali anaaonekana anayo hatia, Sioni ajabu ata MAKONDA siku atakapoanza kumkosoa Baba yake atapelekwa kisutu na kupewa kesi ya vyeti Fake..
Nchi hii hakuna wakosoaji,kuna wazodoaji tu,mkosoaji huwa na mpango mbadala,hawa wanaomba mchana kutwa serikali ishindwe ni wakosoaji hao?
 
Kwa wana JF,

Natambua kuwa kuna threads 2 humu; ila taarifa ni kuwa Akram Aziz ambaye ni mdogo wa Mbunge wa zamani wa Igunga, Ndg. Rostam Aziz, ni kweli alikamatwa na Vyombo vya Dola na mchana huu amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu.

View attachment 917003

Kwa kuanzia, ana makosa takribani 75 ambayo anahusishwa nayo. Kuna utakatishaji fedha/uhujumu uchumi na kukutwa na nyara za serikali pia katika makosa hayo.

View attachment 917001
View attachment 917002

Kwa Taarifa za awali, Soma => Akram Aziz adaiwa kukamatwa na nyara za Serikali... - JamiiForums

===========
Mfanyabiashara Akram Azizi amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 75 ya uhujumu uchumi, ikiwamo kukutwa na nyara za Serikali, silaha, risasi na utakatishaji wa fedha Dola za Marekani 9,018.

Mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka 70 ya kukutwa na silaha, mawili ya kukutwa na risasi, mawili ya kukutwa na nyaraka na moja la utakatishaji wa fedha.

Mshtakiwa huyo amesomewa mashtaka hayo na mawakili wa Serikali wakuu, Paul Kadushi na Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa huyo hakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama hiyo ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.

Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria shtaka la utakatishaji fedha halina dhamana. Mshtakiwa ameenda rumande katika gereza la Segerea.

Upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 12, 2018.
These guys can never been clean,sijui tatizo ni nini.Dini au kabila?Mimi simuamini ponjoro yeyote.
 
Back
Top Bottom