TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Anaandika Boniyai kutoka Account yake ya X

1000061123.jpg

1000061125.jpg

======

20240908_102548.jpg

Ali Mohamed Kibao Ameuawa

Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu umekutwa hospitali ya Mkoa wa Kinondoni,Mwananyamala katika chumba cha kuhifadhia maiti mwili wake ukiwa UMEHARIBIWA VIBAYA SANA.

Mwili wa ALI MOHAMED KIBAO ulikutwa umetupwa jana alfajiri maeneo ya UNUNIO (jirani na viwanja vya NSSF) ukiwa na majereha makubwa sehemu za usoni kiasi ndugu zake walipata tabu kuutambua kirahisi.

ALI MOHAMED KIBAO alikamatwa na watu wanao dhaniwa kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi eneo la TEGETA, mbele ya Jengo la KIBO COMPLEX baada ya gari mbili za Jeshi za Polisi za Landcruiser hardtop nyeupe kuzuia (block) basi la TASHIRIF lenye namba T 343 EES alilokuwa amepanda ALI MOHAMED KIBAO kutoka Dar es saalam kuelekea nyumbani kwao Mkoani Tanga.

Kwa bahati nzuri wakati wote wa tukio likitendeka ndani ya gari palikuwa na askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani (Traffic) ambaye alikuwa kiti cha mbele kama abiria na alishuhudia tukio lote, anatambulika kama MACHIWA anayepatikana kwa namba 0652484802.

Namba ya simu aliyokuwa anatumia ALI MOHAMEDKIBAO ni +255 624 724 247 mpaka wakati anatekwa na kwenda kuuwawa,pia ndiyo namba ambayo mara kadhaa waliomteka walikuwa wakimpigia kuhakiki kama ni yeye.

Kwa mujibu wa wenyeji wa UNUNIO ambao ni walima mchicha, wanasema Jana asubuhi walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi baada ya Kuona mwili wa Mtu mzima, mweupe mwenye asili ya Kiarabu ambaye baadae Jana jioni ndugu waliutambua kuwa ni mwili ALI MOHAMED KIBAO ukiwa na majeraha.

Kabla ya umauti wake ALI MOHAMED KIBAO aliwahi kuwa afisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akastaafu na kujiunga na CCM,baadae akachaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Tanga wakati wa Rais Kikwete,na baadae alijiunga CHADEMA.

Baada ya mauaji haya ya Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA na Msaidizi wa Katibu Mkuu kuwawa idadi ya Viongozi wa CHADEMA wakiotekwa inaongezeka
1. Dioniz Kipanya 2. Kombo Bwana Twaha 3. Godwin Mlay 4. Deusdedith Soka 5. Frank Mbise.
Boniface Jacob
Ex-Mayor
0712 239 595


Soma Pia:
 
Yule waziri, wizara imemshinda.
Samia anayafurahia haya mambo.
Naanza kuona bora utekaji wa kipindi cha magufuli. Nilijua mwiulu mchemba ndio wazuri mbovu wa mambo ya mdani kuliko wote waliopita kumbe nilikuwa najidanganya.
 
Hili sio Jambo zuri
Wale mnaowaua Watanzania na wanadamu wenzenu kwasababu zozote zile HAKIKA Mungu hatawaacha salama.
HAKIKA Mungu yuko pahala ambako bunduki yako kiburi na kiu yako ya damu za Watu haitafua dafu..Hii nchi ni yetu wote haya mambo ya kuwauwa watanzania wenzetu YAMETOSHAA haya mambo HAPANAAAA..
.
 
Kama MTU anatekwa Katikati ya mji, kitovu cha Nchi! Anauwawa na mwili wake unatupwa Jirani tu hapa, je tuko salama kama Nchi?? Who's next? Tunajuaje usalama WA VIONGOZI wetu kama upo? Ununio na magogoni sio mbali, ununio kuna VIONGOZI wakubwa Sana wanaishi huko, je usalama wao ukoje?? Haya wacha tuone who's next....
 
Yule waziri wizara imemshinda.
Samia anayafurahia haya mambo.
Naanza kuona bora utekaji wa kipindi cha magufuli. Nilijua mwiulu mchemba ndio wazuri mbovu wa mambo ya mdani kuliko wote waliopita kumbe nilikuwa najidanganya.SAMIA ANAHUSIKA NA HUU UTEKAJI
Mzee baba usisena eti bora utekaji wa kipind cha magufuli tunatakiwa tuukemee kwa nguvu hii hali yakijinga sana siku akitekwa mtt wa waziri ndo tutakaa sawa ngoja twende tusije kua km colombia magenge ya walanguzi wa dawa za kulevya yanawinda familia za viongozi for revenge ni hali mbya sana twende tu.Tanzania ilifika hatua kiongozi akifa watu wanafurahia kabisa tujiulize kwann tumefika yote kwa sababu watawala wakiwa na wadhifa wanajisahau wanaon wengine takataka hawafai kuishi
 
Mzee baba usisena eti bora utekaji wa kipind cha magufuli tunatakiwa tuukemee kwa nguvu hii hali yakijinga sana siku akitekwa mtt wa waziri ndo tutakaa sawa ngoja twende tusije kua km colombia magenge yanalonda familia za kiongozi nni hali mbya sana twende tu.
Hapana.magufuli ana afadhali.
Idadi ya utekaji ya kipindi cha samia ni KUBWA SANAkuliko kipindi cha magufuli. Huu ukweli tuuseme na tuukubali.wewe hauoni?
 
Back
Top Bottom