TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Hapana.magufuli ana afadhali.
Idadi ya utekaji ya kipindi cha samia ni KUBWA SANAkuliko kipindi cha magufuli. Huu ukweli tuuseme na tuukubali.wewe hauoni?
Tatizo sio JPM na wala sio Samia. Tatizo ni mfumo, haya yote yalitokea na yanaendelea kutokea kwa sababu ya mifumo chini ya serikali ya chama cha kijani na wapo kimya. Inasikitisha sana sijui kama taifa tunaelekea wapi kama serikali inashindwa kuhakikisha raia wake wanakuwa salama.
 
Anaandika Boniyai kutoka Account yake ya X

ALI MOHAMED KIBAO AMEUWAWA..!

Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu umekutwa hospitali ya Mkoa wa Kinondoni,Mwananyamala katika chumba cha kuhifadhia maiti mwili wake ukiwa UMEHARIBIWA VIBAYA SANA.

Mwili wa ALI MOHAMED KIBAO ulikutwa umetupwa jana alfajiri maeneo ya UNUNIO (jirani na viwanja vya NSSF) ukiwa na majereha makubwa sehemu za usoni kiasi ndugu zake walipata tabu kuutambua kirahisi.

ALI MOHAMED KIBAO alikamatwa na watu wanao dhaniwa kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi eneo la TEGETA, mbele ya Jengo la KIBO COMPLEX baada ya gari mbili za Jeshi za Polisi za Landcruiser hardtop nyeupe kuzuia (block) basi la TASHIRIF lenye namba T 343 EES alilokuwa amepanda ALI MOHAMED KIBAO kutoka Dar es saalam kuelekea nyumbani kwao Mkoani Tanga.

Kwa bahati nzuri wakati wote wa tukio likitendeka ndani ya gari palikuwa na askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani (Traffic) ambaye alikuwa kiti cha mbele kama abiria na alishuhudia tukio lote ,anatambulika kama MACHIWA anayepatikana kwa namba 0652484802.

Namba ya simu aliyokuwa anatumia ALI MOHAMEDKIBAO ni +255 624 724 247 mpaka wakati anatekwa na kwenda kuuwawa,pia ndiyo namba ambayo mara kadhaa waliomteka walikuwa wakimpigia kuhakiki kama ni yeye.

Kwa mujibu wa wenyeji wa UNUNIO ambao ni walima mchicha,wanasema Jana asubuhi walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi baada ya Kuona mwili wa Mtu mzima,mweupe mwenye asili ya Kiarabu ambaye baadae Jana jioni ndugu waliutambua kuwa ni mwili ALI MOHAMED KIBAO ukiwa na majeraha.

Kabla ya umauti wake ALI MOHAMED KIBAO aliwahi kuwa afisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akastaafu na kujiunga na CCM,baadae akachaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Tanga wakati wa Rais Kikwete,na baadae alijiunga CHADEMA.

Baada ya mauaji haya ya Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA na Msaidizi wa Katibu Mkuu kuwawa idadi ya Viongozi wa CHADEMA wakiotekwa inaongezeka
1.Dioniz Kipanya 2.Kombo Bwana Twaha 3.Godwin Mlay 4.Deusdedith Soka 5.Frank Mbise.

Boniface Jacob
Ex-Mayor
0712 239 595

View: https://x.com/ExMayorUbungo/status/1832674223258476755?t=aXBxUnhaC6U0JYRnw4SXKg&s=19

Aiseeeeeèe
Napitatu niko kwenye maombj ya....
 
Magufuli alisha ustikia huu mchezo.

Kuna kijana CDM Mbeya uchaguzi uliopita walimteka hivi hivi na kumpotezea maisha yake.

Ikabidi Magufuli akaombe msamaha kwa ile familia na kuwapa pole (Lakini hela) aifidii maisha ya mtu.

Chadema na genge lenu la wahusika huko serikalini acheni huu ushenzi. Ushindi aupatikani kwa njia hizi za udhalimu.

R.I..P
 
Yule waziri wizara imemshinda.
Samia anayafurahia haya mambo.
Naanza kuona bora utekaji wa kipindi cha magufuli. Nilijua mwiulu mchemba ndio wazuri mbovu wa mambo ya mdani kuliko wote waliopita kumbe nilikuwa najidanganya.SAMIA ANAHUSIKA NA HUU UTEKAJI

Kwa kweli hii Serikali ya sasa ni aheri hata ya wakatiwa Magufuli. Japo kulikuwa na utekaji na mauaji ya wanasiasa, lakini hayakufikia kiwango hiki. Shetani ameweka makao ya kudumu kwente Serikali ya awamu hii. Kusipofanyika kitu, hawa watu wataendelea kuua Watanzania kama vile wanavyouawa kuku.

Mungu wa mbinguni tunaomba atusaidie, uovu huu ambao haya mashetani yanatenda dhidi ya wanadamu wengine, ukawarudie na wao mara 2 zaidi.
 
Tatizo sio JPM na wala sio Samia. Tatizo ni mfumo, haya yote yalitokea na yanaendelea kutokea kwa sababu ya mifumo chini ya serikali ya chama cha kijani na wapo kimya. Inasikitisha sana sijui kama taifa tunaelekea wapi kama serikali inashindwa kuhakikisha raia wake wanakuwa salama.
Nakubaliana na wewe
 
Kwa kweli hii Serikali ya sasa ni aheri hata ya wakatiwa Magufuli. Japo kulikuwa na utekaji na mauaji ya wanasiasa, lakini hayakufikia kiwango hiki. Shetani ameweka makao ya kudumu kwente Serikali ya awamu hii. Kusipofanyika kitu, hawa watu wataendelea kuua Watanzania kama vile wanavyouawa kuku.

Mungu wa mbinguni tunaomba atusaidie, uovu huu ambao haya mashetani yanatenda dhidi ya wanadamu wengine, ukawarudie na wao mara 2 zaidi.
Hii serikali ni dhalimu kupita kiasi
 
Back
Top Bottom