TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Hapana. Hapana. Hapana.

Hii itakuwa ni kuitesa familia ya marehemu.

Cha kufanya, ni chadema nao waanze kuwateka watoto, wake, na viongozi wa ccm.
Unataka CDM kuwa branded kuwa chama cha kigaidi? Tutumie akili kidogo.
 
Hivi,alipo Gen Mabeyo,yeye hajilaumu kweli? Alitendea haki katiba,lakini hakufanya maamzi sahihi.
 
Unajua hakuna kitu kama haki ambacho Mungu alimuumbia mwanadamu kifo,na kila mtu atakufa,hata ungekuwa na madaraka na nguvu vipi utakufa,hata ukiniuwa mimi na wewe kesho utakufa
 
Watu wanauliwa kama wanyama
Yaani ina maana kuna kikosi maalum kina baraka zote za wao kuua

Ova
 
Mambo ya kwenye mapori hayo according to DC aliyetumbuliwa baada ya kutoa nje shuka chakavu na chafu la baba mwenye nyumba ambaye kila siku hujinadi huko nje kwamba yeye ni msafi sana
 
Usalama wa Watanzania uko wapi , Ee Mwenyezi Mungu tunaomba haya mambo yaishe. Inasikitisha sana watu wanapotezwa kimahisara tu
 
Watanzania this is a wake up call.
Tuamke. Tumezidi kua makondoo.
Your browser is not able to display this video.
 
Baada ya Kuutambua kwa sasa wanasubiri uchunguzi wa Madaktari.

View attachment 3090144
Kwa mkuu wa nchi hii bado kwake ni DRAMA.
Mambo ya aibu sana kwenye hii nchi.
Una toaje roho ya mwanadamu kama kuku? Bora hata kuku una shahadia kabla ya kumtoa roho. Sisi Wakristo kwenye amri za Mungu tuna ambiwa USIUE!!! Hao wanao ua wana pata wapi mamlaka? Na ni kwanini ni hizi awamu mbili za mwisho? Who is behind this scene??? Watanzania tuse sasa YATOSHA!!!
 
Aliacha kazi JWTZ akaenda ccm, akaja kuhamia CHADEMA..

Mapinduzi?
Mwenyewe najiuliza, kwamba huyo mzee alikuwa na uwezo wa kuorganize mapinduzi?

Au ukishakuwa JWTZ huruhusiwi kuwa upinzani itabidi uuawe?

Au alikuwa anajua siri gani ama alikuwa na nini cha mno hadi kuamua kumnyamazisha?
 
Kulaumu basi la Tashriff ni kujaribu kuukimbia mzizi wa fitina tu (trying to project the problem).

Kizimkazi ndiyo shida hapa.
 
Chadema punguzeni kuandikaaaaa tu na kulaani. Maamuzi magumu yana nafasi kubwa. Mlizuiwa mlikamatwa mkadhihakiwa mkawekwa rumande mkasafirishwa kas kus mashariki na magharibi mpo kimya, vijana wenu wamekamatwa hamjui walipo mpo kutwa kuandika warudisheni,

wafia vyama mnakwama mno. Punguzeni kusifu na kuabudu kama chawa wa jirani.

Watesi wametambua uoga wenu ndio maana haya yanaendelea. Mtaitisha press conference tena then what?
 
Magufuli ndio muasisi wa huu uchafu
Roho yangu inanituma vinginevyo:

Haya mambo yalikuwa ya kawaida sana kule Zanzibar. Yalikuwa yanafanywa na wale waliokuwa wakijiita mazombi.

Je, haiwezekani, huu ushetani tumeurithi toka Zanzibar? Mshauri namba 1 wa Rais wa JMT ni Makamu wa Rais wa JMT. Je, haiwezekani huyu mshauri wake namba 1 ambaye alikuwa anatoka Zanzibar kulikokuwa kumejaa siasa za namna hii, kuwa ndiye aliyemshauri JPM? Haiwezekani ikawa ndiyo sababu ya matukio haya kuongezeka maradufu, maana sasa madaraka yameshikwa na aliyekuwa mshauri kwenye siasa za kiharamia za mazombi, ambaye ana uzoefu wa ushetani huu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…