Na hapa ndio tulipopotoka kama Taifa na nasikitika hata wananchi tushaingia kwenye huu Upuuzi..., Hakuna vijana wa CHADEMA kuna vijana wa Tanzania na Watanzania..., tutakapoendelea kujigawa kwa mafungu sisi wa huku chini tutaendelea kutumika kama madaraja kwenye Siasa....
Jambo kama hili likemewe sababu sio la kibinadamu no matter aliyeshikwa ni mwanasiasa au teja...., Ama sivyo hizi Divide and Rule zitaendelea kuwanufaisha wachache no matter Chama gani kitakuwa kimeshika Hatamu,... Kwahio yoyote anayefanyiwa ndivyo sivyo kila mtu akemee kwa nguvu zote na wakati wote....