TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Utatuomba kura tena 😳
 

Attachments

  • 5815043-accbb0cbe8f7594024e835ceb053134c.png
    20.3 KB · Views: 2
Kaka hapa wakutuokoa tu ni Mungu, Mungu mwenyewe mpaka atake yeye mwenyewe, amekuwa mgumu sana wa kuchukua maamuzi, ni kama Shetani anataka kumzidi nguvu...sio kwamba nakufuru lakini najaribu kuwaza.
Watu wanatekwa wanapotea, hawajulikani walipo na tuna waziri wa mambo ya ndani ya nchi na Jeshi lake ambalo ndio limelalamikiwa muda wote. Yupo tu na hajigusi na mamlaka yake ya uteuzi haimgusi, kwamba anafanya kazi nzuri? Hii ni aibu.

Hivi hawa ndio watu wanaotupigia kelele na ving'ora huko barabarani tuwapishe wakimbie? Huwa wanakimbilia wapi?
 
Daah hatari sana aisee watu wanakufa harafu wahusika wakuu wapo kimya na wanaendelea na mambo yao kama kawaida hii mbaya sana aisee harafu ukiuliza kitu wanachouana ni cha kijinga kabisa mambo ya Siasa tu..
Nimeumia sana huyu Mzee wa daslm mstaarabu kufa kwa namna ile wakati mtu mwenyewe alikua mstaarabu sana..
 
Unafikiri hajui watu zaidi ya 100 wametekwa. Unafikiri hajui kinachoendelea? Kuna briefing kila siku kuhusu hali ya usalama wa nchi. Huwa mnamfanya kama mtoto, anajua kila kitu. Anaidhinisha.
Tunamtaka achukuw hatua sio suala la kujua
 
Huyu mama atakua na tatizo kubwa sana. Sio bure
 
Huyo unayemtaka achukue hatua ndio aliyepitisha sheria mpya ya usalama wa taifa. Lengo la sheria ile, haya ndio matokeo yaliyokuwa yanatarajiwa.
 
Huyo unayemtaka achukue hatua ndio aliyepitisha sheria mpya ya usalama wa taifa. Lengo la sheria ile, haya ndio matokeo yaliyokuwa yanatarajiwa.
CCM itamuzaje kwa wananchi yule bibi 2025?
 
Dah inasikitisha sana. Nadhani huu si wakati wa kufanya vitendo vya kuwafanya wapiga kura waogope, kwani uwazi na maendeleo ya science na technolojia, inapelekea kila kitu kuwa wazi. Haifahamiki nani yupo nyuma ya huu muendelezo ila ni ukweli usiopingika ushiriki wa makundi shindani ndani ya mfumo wetu wa utawala yanafahamu kabisa kinachoendelea. Tuchukue tahadhari!
 
Uchunguzi wa kina unahitajika,sitaki kuamini kuwa Polisi wamekuwa wapuuzi kiasi cha kujionyesha mbele za raia kuwa wao ndio wavunja sheria...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…