milele amina
JF-Expert Member
- Aug 16, 2024
- 6,045
- 8,080
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kaka hapa wakutuokoa tu ni Mungu, Mungu mwenyewe mpaka atake yeye mwenyewe, amekuwa mgumu sana wa kuchukua maamuzi, ni kama Shetani anataka kumzidi nguvu...sio kwamba nakufuru lakini najaribu kuwaza.
Huu ni muendelezo tu ila yeye ndio muasisi wa huu uhuni...na Wala uwezi kumvua Samia na huu uhuni unyama unaoendeleaR.I.P JPM ulikua unasingiziwa sana. Ona sasa watu wanaendelea kuokotwa wameuwawa ila wala Rais hatajwi kwenye h
Tunamtaka achukuw hatua sio suala la kujuaUnafikiri hajui watu zaidi ya 100 wametekwa. Unafikiri hajui kinachoendelea? Kuna briefing kila siku kuhusu hali ya usalama wa nchi. Huwa mnamfanya kama mtoto, anajua kila kitu. Anaidhinisha.
View attachment 3090383View attachment 3090383View attachment 3090383View attachment 3090383View attachment 3090383View attachment 3090383View attachment 3090383View attachment 3090383View attachment 3090383View attachment 3090383View attachment 3090383View attachment 3090383View attachment 3090383View attachment 3090383View attachment 3090383View attachment 3090383View attachment 3090383View attachment 3090383View attachment 3090383View attachment 3090383
Huyu mama atakua na tatizo kubwa sana. Sio bureChukua hatua Rais wangu.
Pengine umesahau , wacha nikukumbushe wewe ndie Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote nchini.
Na pengine umesahau wacha nikukumbushe wewe ndie Mwenyekit wa Baraza la mawazir nchini.
Chukua hatua Rais wangu.
Labda umesahau, wacha nikukumbushe wewe ndie uliyemteua Hamadi Masauni kuwa waziri wa Mambo ya ndani.
Naendelea kukumbumbusha Kwa nia njema Rais wangu, wewe ndie uliyemteua Cammililius Wambura kuwa inspeta jenerali wa polisi nchini.
Na kubwa kuliko yote nakukumbusha kuwa yanayotokea nchini yapo kinyume na sheria za duniani Hadi za dini yako.
Chukua hatua Tafadhar.
Inawezekana mwanae ndio anaengineer haya mambo ndio maana huyu mama yupo kimya ila yana mwishoTunamtaka achukuw hatua sio suala la kujua
Yuko hapo kwa maelekezo ya watu wengine.Huyu mama atakua na tatizo kubwa sana. Sio bure
Huyo unayemtaka achukue hatua ndio aliyepitisha sheria mpya ya usalama wa taifa. Lengo la sheria ile, haya ndio matokeo yaliyokuwa yanatarajiwa.Chukua hatua Rais wangu.
Pengine umesahau , wacha nikukumbushe wewe ndie Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote nchini.
Na pengine umesahau wacha nikukumbushe wewe ndie Mwenyekit wa Baraza la mawazir nchini.
Chukua hatua Rais wangu.
Labda umesahau, wacha nikukumbushe wewe ndie uliyemteua Hamadi Masauni kuwa waziri wa Mambo ya ndani.
Naendelea kukumbumbusha Kwa nia njema Rais wangu, wewe ndie uliyemteua Cammililius Wambura kuwa inspeta jenerali wa polisi nchini.
Na kubwa kuliko yote nakukumbusha kuwa yanayotokea nchini yapo kinyume na sheria za duniani Hadi za dini yako.
Chukua hatua Tafadhar.
CCM itamuzaje kwa wananchi yule bibi 2025?Huyo unayemtaka achukue hatua ndio aliyepitisha sheria mpya ya usalama wa taifa. Lengo la sheria ile, haya ndio matokeo yaliyokuwa yanatarajiwa.
Akifufuka bibi anahama nchi.Labda Magufuli kafufuka
UKISHALEWA MADARAKA MUNGU HUWEZI KUMKUMBUKA HATA KAMA ULIKUWA UNASALI KIASI GANI. TATIZO AFRIKA MTU AKIWA KIONGOZI ANAJIONA KAMA YEYE NDIO MUNGUEhee.kule kule kwa jana.
Samia sijui kama ana swali sala 5.hana hofu ya mungu. Nchi ishamshinda
Dah inasikitisha sana. Nadhani huu si wakati wa kufanya vitendo vya kuwafanya wapiga kura waogope, kwani uwazi na maendeleo ya science na technolojia, inapelekea kila kitu kuwa wazi. Haifahamiki nani yupo nyuma ya huu muendelezo ila ni ukweli usiopingika ushiriki wa makundi shindani ndani ya mfumo wetu wa utawala yanafahamu kabisa kinachoendelea. Tuchukue tahadhari!Anaandika Boniyai kutoka Account yake ya X
View attachment 3090046
View attachment 3090047
======
Ali Mohamed Kibao Ameuawa
Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu umekutwa hospitali ya Mkoa wa Kinondoni,Mwananyamala katika chumba cha kuhifadhia maiti mwili wake ukiwa UMEHARIBIWA VIBAYA SANA.
Mwili wa ALI MOHAMED KIBAO ulikutwa umetupwa jana alfajiri maeneo ya UNUNIO (jirani na viwanja vya NSSF) ukiwa na majereha makubwa sehemu za usoni kiasi ndugu zake walipata tabu kuutambua kirahisi.
ALI MOHAMED KIBAO alikamatwa na watu wanao dhaniwa kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi eneo la TEGETA, mbele ya Jengo la KIBO COMPLEX baada ya gari mbili za Jeshi za Polisi za Landcruiser hardtop nyeupe kuzuia (block) basi la TASHIRIF lenye namba T 343 EES alilokuwa amepanda ALI MOHAMED KIBAO kutoka Dar es saalam kuelekea nyumbani kwao Mkoani Tanga.
Kwa bahati nzuri wakati wote wa tukio likitendeka ndani ya gari palikuwa na askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani (Traffic) ambaye alikuwa kiti cha mbele kama abiria na alishuhudia tukio lote, anatambulika kama MACHIWA anayepatikana kwa namba 0652484802.
Namba ya simu aliyokuwa anatumia ALI MOHAMEDKIBAO ni +255 624 724 247 mpaka wakati anatekwa na kwenda kuuwawa,pia ndiyo namba ambayo mara kadhaa waliomteka walikuwa wakimpigia kuhakiki kama ni yeye.
Kwa mujibu wa wenyeji wa UNUNIO ambao ni walima mchicha, wanasema Jana asubuhi walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi baada ya Kuona mwili wa Mtu mzima, mweupe mwenye asili ya Kiarabu ambaye baadae Jana jioni ndugu waliutambua kuwa ni mwili ALI MOHAMED KIBAO ukiwa na majeraha.
Kabla ya umauti wake ALI MOHAMED KIBAO aliwahi kuwa afisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akastaafu na kujiunga na CCM,baadae akachaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Tanga wakati wa Rais Kikwete,na baadae alijiunga CHADEMA.
Baada ya mauaji haya ya Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA na Msaidizi wa Katibu Mkuu kuwawa idadi ya Viongozi wa CHADEMA wakiotekwa inaongezeka
1. Dioniz Kipanya 2. Kombo Bwana Twaha 3. Godwin Mlay 4. Deusdedith Soka 5. Frank Mbise.
Soma Pia:
Boniface Jacob
- CHADEMA: Mzee Ally Kibao ametekwa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama akiwa kwenye basi. Usalama wa Taifa waeleze alipo
- Polisi: Tunachunguza kubaini chanzo na watu waliohusika kumchukua Ally Kibao
Ex-Mayor
0712 239 595