Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
- Thread starter
-
- #721
Huyu dogooo siku zake tunamusabiaaa....cheo dhamanaHuyu hapa View attachment 3090481
Hawa watu no wajinga sana.Huyu dogooo siku zake tunamusabiaaa....cheo dhamana
Mimi binafsi sikuwahi kumsikia Marehemu katika kauli za kisiasa na nikiri nilikuwa simjui lakini nimeguswa sana na kifo chake jinsi alivyouawa kinyama na kwa mateso makubwa bila kosa ,lolote. .Anaandika Boniyai kutoka Account yake ya X
View attachment 3090046
View attachment 3090047
======
Ali Mohamed Kibao Ameuawa
Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu umekutwa hospitali ya Mkoa wa Kinondoni,Mwananyamala katika chumba cha kuhifadhia maiti mwili wake ukiwa UMEHARIBIWA VIBAYA SANA.
Mwili wa ALI MOHAMED KIBAO ulikutwa umetupwa jana alfajiri maeneo ya UNUNIO (jirani na viwanja vya NSSF) ukiwa na majereha makubwa sehemu za usoni kiasi ndugu zake walipata tabu kuutambua kirahisi.
ALI MOHAMED KIBAO alikamatwa na watu wanao dhaniwa kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi eneo la TEGETA, mbele ya Jengo la KIBO COMPLEX baada ya gari mbili za Jeshi za Polisi za Landcruiser hardtop nyeupe kuzuia (block) basi la TASHIRIF lenye namba T 343 EES alilokuwa amepanda ALI MOHAMED KIBAO kutoka Dar es saalam kuelekea nyumbani kwao Mkoani Tanga.
Kwa bahati nzuri wakati wote wa tukio likitendeka ndani ya gari palikuwa na askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani (Traffic) ambaye alikuwa kiti cha mbele kama abiria na alishuhudia tukio lote, anatambulika kama MACHIWA anayepatikana kwa namba 0652484802.
Namba ya simu aliyokuwa anatumia ALI MOHAMEDKIBAO ni +255 624 724 247 mpaka wakati anatekwa na kwenda kuuwawa,pia ndiyo namba ambayo mara kadhaa waliomteka walikuwa wakimpigia kuhakiki kama ni yeye.
Kwa mujibu wa wenyeji wa UNUNIO ambao ni walima mchicha, wanasema Jana asubuhi walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi baada ya Kuona mwili wa Mtu mzima, mweupe mwenye asili ya Kiarabu ambaye baadae Jana jioni ndugu waliutambua kuwa ni mwili ALI MOHAMED KIBAO ukiwa na majeraha.
Kabla ya umauti wake ALI MOHAMED KIBAO aliwahi kuwa afisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akastaafu na kujiunga na CCM,baadae akachaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Tanga wakati wa Rais Kikwete,na baadae alijiunga CHADEMA.
Baada ya mauaji haya ya Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA na Msaidizi wa Katibu Mkuu kuwawa idadi ya Viongozi wa CHADEMA wakiotekwa inaongezeka
1. Dioniz Kipanya 2. Kombo Bwana Twaha 3. Godwin Mlay 4. Deusdedith Soka 5. Frank Mbise.
Soma Pia:
Boniface Jacob
- CHADEMA: Mzee Ally Kibao ametekwa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama akiwa kwenye basi. Usalama wa Taifa waeleze alipo
- Polisi: Tunachunguza kubaini chanzo na watu waliohusika kumchukua Ally Kibao
Ex-Mayor
0712 239 595
Kuna magari yanabadilishwa namba kama nguo za ndani3. Genge hili la ugaidi linaloendesha shughuli zake mchana kweupe, kila linapomlenga mtu fulani na likimfikia hujitambulisha kuwa ni "police" wakitumia magari ya kifahari sana na wakati mwingine ya Jeshi polisi kwa sura na usajili wa namba zao. Swali muhimu ni hili, kwamba, inakuwaje genge hili la kihalifu linalojitambulisha kama "police" pale linapotenda uhalifu wake mchana kweupe na nyie polisi halisi hamfanyi kuchukua hatua zozote kuwatia mikononi mwenu wauaji hawa...?
Dunia iko kiganjani huhitaji kuzunguka dunia , the world 🌎 is on your finger tipsJukumu la usalama wetu ni la kwetu wenyewe, kama yupo wa kukusaidia inabidi akukute upo kwenye mapambano.
Pamoja na ukweli kwamba Watanzania tu waoga sana dhidi ya Serikali ambayo haioni shida kuuondoa uhai wa mwanadamu, bado ni muhimu kuitaarifu Dunia kwa kina juu ya uharamia unaofanywa na dola dhidi ya Raia wake. Tafuteni wasaa wa kufikisha taarifa hizi, tena kwa vielelezo, kwenye mabunge yote ya kidemokrasia Dunia, mkianzia na lile Bunge la Ulaya. Hata ile kujua tu kuwa, huku Tanzania kuna uharamia unafanywa dhidi ya wakosoaji wote wa Serikali, vyombo vyake na CCM, inatosha, ili hata kama itatokea siku moja,Watanzania watasimama kutetea uhai wao dhidi ya watawala, Dunia ijue kuwa ni mapambano kutetea haki ya kuishi ambayo kwa sasa, nchini Tanzania, haiheshimiwi. Kwa sasa vyombo vya dola vinajiamlia nani aishi na nani asiishi; nani akishauawa maiti yake ionekane, na nani isionekane milele.
Wakati yakifanyika haya, wana wa Mungu, tuzidi kumwomba Mungu, tukiunganisha na jitihada nyingine. Mungu wetu ni mwaminifu, hujibu kwa wakati na kwa namna iliyo sahihi.
Hatari mnoKwa hiyo waliopotea wote na kuuawa ni mashushushu wa zamani? Lame explanations hizi.
Hata hili litapita kama mengine sisi tugoje yetu tu. Huu ndiyo mfumo tulio amua twende naa kwa sasa, tutauzoea tu, mbona nchi za wenzetu hivi vitu ni kawaida tu. Wewe ukiamka salama mshukuru Mungu nenda kazini kama utabahatika kurudi salama nyumbani shukuru Mungu. Mfa maji haishi kutapa tapaRaia Samia hajatoa kauli thabiti dhidi ya kundi hili la kigaidi linaloendelea kufanya uhalifu wa kuteka na kuua raia wasio na hatua....
Aidha polisi wameendelea kutoa kauli tata, zilizobeba mizaha, kutojali na zinazoonesha "zero responsibility" kwa Jeshi la Police kinyume kabisa na wajibu wao wa kisheria na kikatiba.......
Kwa niaba ya raia wenzangu, naomba serikali kwa ujumla (Rais Samia Suluhu Hassan) na specific Jeshi la police wajibu maswali haya muhimu ya wananchi:
1. Kazi na jukumu la msingi la Jeshi la Police ni kulinda Usalama wa raia na Mali zao. Kazi yenu polisi pia hutekekezwa kutumia intellejensia ya kunusa uhalifu, kisha kuchunguza, kudhibiti na kukamata wahalifu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Kama hizi ndizo kazi zenu, ni kwanini mauaji haya yanaendelea na ninyi mkiwa mpo kimya tu....?
2. Circumstantial evidence inaonesha wazi kuwa polisi kwa upande wa pili ni nyie mnahusika. Mmeunda genge la utekaji na uuaji wa kuteka na kutesa watu mnaoambiwa na viongozi wenu muwaue. Haina shaka kuwa mnafadhiliwa na wanasiasa vigogo ndani ya CCM na serikalini lengo likiwa ni kulinda madaraka na influence yao ya kisiasa. Polisi mmezikana tuhuma hizi. Mmesema hamhusiki. Kama ndiyo hivi, ni nani wanahusika....?
3. Genge hili la ugaidi linaloendesha shughuli zake mchana kweupe, kila linapomlenga mtu fulani na likimfikia hujitambulisha kuwa ni "police" wakitumia magari ya kifahari sana na wakati mwingine ya Jeshi polisi kwa sura na usajili wa namba zao. Swali muhimu ni hili, kwamba, inakuwaje genge hili la kihalifu linalojitambulisha kama "police" pale linapotenda uhalifu wake mchana kweupe na nyie polisi halisi hamfanyi kuchukua hatua zozote kuwatia mikononi mwenu wauaji hawa...?
4. Serikali (Rais Samia Suluhu Hassan), TANPOL na Waziri wa mapolisi ndugu Masauni, Je mmeshindwa kulinda uhai wa raia? Mnafanya nini kwenye ofisi zetu za umma kama genge hili la ugaidi limewashinda nguvu kiasi cha kujiona lenyewe ndiyo serikali? Kwanini mnadhani mnastahili kuaminika ktk mazingira haya?
##Rais Samia Suluhu Hassan toka mafichoni, acha kuwa chura kiziwi wa Kizimkazi waambie raia kuwa wewe na serikali yako mmeshashindwa kazi, mmeshindwa kutumia vyombo vya ulinzi kutulinda uhai wa watu ili kila mtu achukue hatua binafsi za kujilinda muone kama tutashindwa....!!