Raia Samia hajatoa kauli thabiti dhidi ya kundi hili la kigaidi linaloendelea kufanya uhalifu wa kuteka na kuua raia wasio na hatua....
Aidha polisi wameendelea kutoa kauli tata, zilizobeba mizaha, kutojali na zinazoonesha "zero responsibility" kwa Jeshi la Police kinyume kabisa na wajibu wao wa kisheria na kikatiba.......
Kwa niaba ya raia wenzangu, naomba serikali kwa ujumla (Rais Samia Suluhu Hassan) na specific Jeshi la police wajibu maswali haya muhimu ya wananchi:
1. Kazi na jukumu la msingi la Jeshi la Police ni kulinda Usalama wa raia na Mali zao. Kazi yenu polisi pia hutekekezwa kutumia intellejensia ya kunusa uhalifu, kisha kuchunguza, kudhibiti na kukamata wahalifu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Kama hizi ndizo kazi zenu, ni kwanini mauaji haya yanaendelea na ninyi mkiwa mpo kimya tu....?
2. Circumstantial evidence inaonesha wazi kuwa polisi kwa upande wa pili ni nyie mnahusika. Mmeunda genge la utekaji na uuaji wa kuteka na kutesa watu mnaoambiwa na viongozi wenu muwaue. Haina shaka kuwa mnafadhiliwa na wanasiasa vigogo ndani ya CCM na serikalini lengo likiwa ni kulinda madaraka na influence yao ya kisiasa. Polisi mmezikana tuhuma hizi. Mmesema hamhusiki. Kama ndiyo hivi, ni nani wanahusika....?
3. Genge hili la ugaidi linaloendesha shughuli zake mchana kweupe, kila linapomlenga mtu fulani na likimfikia hujitambulisha kuwa ni "police" wakitumia magari ya kifahari sana na wakati mwingine ya Jeshi polisi kwa sura na usajili wa namba zao. Swali muhimu ni hili, kwamba, inakuwaje genge hili la kihalifu linalojitambulisha kama "police" pale linapotenda uhalifu wake mchana kweupe na nyie polisi halisi hamfanyi kuchukua hatua zozote kuwatia mikononi mwenu wauaji hawa...?
4. Serikali (Rais Samia Suluhu Hassan), TANPOL na Waziri wa mapolisi ndugu Masauni, Je mmeshindwa kulinda uhai wa raia? Mnafanya nini kwenye ofisi zetu za umma kama genge hili la ugaidi limewashinda nguvu kiasi cha kujiona lenyewe ndiyo serikali? Kwanini mnadhani mnastahili kuaminika ktk mazingira haya?
##Rais Samia Suluhu Hassan toka mafichoni, acha kuwa chura kiziwi wa Kizimkazi waambie raia kuwa wewe na serikali yako mmeshashindwa kazi, mmeshindwa kutumia vyombo vya ulinzi kutulinda uhai wa watu ili kila mtu achukue hatua binafsi za kujilinda muone kama tutashindwa....!!