TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Huwa bado nawaza sana balozi Simoni Sirro enzi akiwa IGP aliwahi kusema kuwa Polisi wana ushahidi kamili kuhusu mashitaka dhidi ya Freeman Mbowe katika kesi yake ya 'ugaidi' iliyokuwa inahusisha pia utekaji na mipango ya mauaji kwa viongozi mbalimbali wa kisiasa na tuliona kina Kingai wakienfa mahakamani kutoa matokeo ya upelelezi wao, ambapo mahakama ilimkuta Mbowe na wenzake wana kesi ya kujibu; mara ghafla bin vuu tukaona DPP amesita kuendelea na kesi, Mbowe akatoka jela yeye na washtakiwa wenzake, siku hiyo hiyo akaenda Ikulu kuonana na Samia, mara ghafla tukaambiwa maridhiano, Kisha IGP Sirro anatolewa U-IGP na kuteuliwa kuwa balozi Zimbabwe;....
 
Hamkani si shwari tena.
Na kama moto huu ukiwaka......hakuna mwenye uwezo wa kuuzima......LENGO LITATIMIA central corridor Atlantic to Indian Ocean via tz and drc
 
Mh Rais Samia Suluhu Hassan tafadhali shutuka kuna watu wanakuharibia Uongozi wako kiaina. Hawa watekaji si polisi rasmi ni kikundi fulani kinachodanganya raia wawaamini kumbe ni maharamia.
 
Kesi Ile ilikuwa ya kimkakati. Lengo kuu likiwa kumpaisha Bi Kizimkazi!
 
Huu ndio wasiwasi wangu kama serikali inahusika basi inapanda mbegu ambayo ita back fire rai yangu wajisafishe.
Kwa hatua waliyofikia hakuna namna watajisafisha! Washakula nyama na damu za watu... Hawawezi kukoma!
 
Au ndio utekelezaji wa ile kauli ya "Hakuna uhuru usio na mipaka"?? 😳 πŸ€”
Au "Polisi, tukuwapoteza msiwatafute?"😳😳😳
 
Mbowe na genge lake walimsema sana Dkt Magufuli ndiye anaagiza waty wafe, walifanya sherehe hahaha, ngoja sasa ngoma inogile. Dkt Magufuli alikuwa mkarimu sana
 
Sio jambo jipya watu kufanya mauji huko mitaani tunapoishi kama Kuna watu wapo tayari kukuua sababu yakunyang'anya simu tu sasa mtu kama huyu ukimpa posho nzuri na maisha yakufurahia hapa duniani kuua itakuwa ni jambo dogo

Kama mnavyosikia habari za watu kupotea ni wengi sana lakini zinazolipotiwa ni zile tu za watu wenye nyazifa fulani kwenye tukio

Maono yangu nazani Kuna uwezekano mkubwa kwenye hii plan hawa wazee wa tinted nyeusi hawakujua wanayekuja kumkamata mpaka wamekuja kudedisha walijua ni raia wa kawaida lakini ndio hivyo mtu wa watu alikuwa mtu wa dini wamejikuta wanajichanganya maiti huwa zinatupwa polni Leo hii tumeiona ununio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…