TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Anaandika Boniyai kutoka Account yake ya X
View attachment 3090046
View attachment 3090047

======


Ali Mohamed Kibao Ameuawa

Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu umekutwa hospitali ya Mkoa wa Kinondoni,Mwananyamala katika chumba cha kuhifadhia maiti mwili wake ukiwa UMEHARIBIWA VIBAYA SANA.

Mwili wa ALI MOHAMED KIBAO ulikutwa umetupwa jana alfajiri maeneo ya UNUNIO (jirani na viwanja vya NSSF) ukiwa na majereha makubwa sehemu za usoni kiasi ndugu zake walipata tabu kuutambua kirahisi.

ALI MOHAMED KIBAO alikamatwa na watu wanao dhaniwa kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi eneo la TEGETA, mbele ya Jengo la KIBO COMPLEX baada ya gari mbili za Jeshi za Polisi za Landcruiser hardtop nyeupe kuzuia (block) basi la TASHIRIF lenye namba T 343 EES alilokuwa amepanda ALI MOHAMED KIBAO kutoka Dar es saalam kuelekea nyumbani kwao Mkoani Tanga.

Kwa bahati nzuri wakati wote wa tukio likitendeka ndani ya gari palikuwa na askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani (Traffic) ambaye alikuwa kiti cha mbele kama abiria na alishuhudia tukio lote, anatambulika kama MACHIWA anayepatikana kwa namba 0652484802.

Namba ya simu aliyokuwa anatumia ALI MOHAMEDKIBAO ni +255 624 724 247 mpaka wakati anatekwa na kwenda kuuwawa,pia ndiyo namba ambayo mara kadhaa waliomteka walikuwa wakimpigia kuhakiki kama ni yeye.

Kwa mujibu wa wenyeji wa UNUNIO ambao ni walima mchicha, wanasema Jana asubuhi walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi baada ya Kuona mwili wa Mtu mzima, mweupe mwenye asili ya Kiarabu ambaye baadae Jana jioni ndugu waliutambua kuwa ni mwili ALI MOHAMED KIBAO ukiwa na majeraha.

Kabla ya umauti wake ALI MOHAMED KIBAO aliwahi kuwa afisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akastaafu na kujiunga na CCM,baadae akachaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Tanga wakati wa Rais Kikwete,na baadae alijiunga CHADEMA.

Baada ya mauaji haya ya Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA na Msaidizi wa Katibu Mkuu kuwawa idadi ya Viongozi wa CHADEMA wakiotekwa inaongezeka
1. Dioniz Kipanya 2. Kombo Bwana Twaha 3. Godwin Mlay 4. Deusdedith Soka 5. Frank Mbise.

Boniface Jacob
Ex-Mayor
0712 239 595
PoliCCM wanatumia nguvu nyingi ssna kuwaua raia wasiokuwa na hatia. Wakiua watu wakaisha wataongoza wanyamapori.
 
Makao makuu ya Jeshi la polisi yapo Tanganyika, waziri WA mambo ya ndani ni mzanzibar. Anaishi na kuzaliwa unguja.
Tunalindwa na nani sisi raia na Mali zetu?
Yule Waziri aliitws kwenye interview na media flani hapa akaulizwa kuhusu watu kutekwa na kupotea.
Kikubwa alichosema hakuna hayo matukio watu wanazua taharuki kwa kuwa Mama anauburuza mwingi.
Mawaziri wa namna hii hata huyo Mama kuendelea kua nao haimsaidii
 
Yule waziri ,wizara imemshinda.
Samia anayafurahia haya mambo.
Naanza kuona bora utekaji wa kipindi cha magufuli. Nilijua mwiulu mchemba ndio wazuri mbovu wa mambo ya mdani kuliko wote waliopita kumbe nilikuwa najidanganya.
Kwa hio Masauni ajiuzulu au mpaka achomolewe kinguvu?
 
Yule Waziri aliitws kwenye interview na media flani hapa akaulizwa kuhusu watu kutekwa na kupotea.
Kikubwa alichosema hakuna hayo matukio watu wanazua taharuki kwa kuwa Mama anauburuza mwingi.
Mawaziri wa namna hii hata huyo Mama kuendelea kua nao haimsaidii
Watanganyika Kuna mahali upstairs hatuko sawa, watu 60 million tunalindwa na 1.5 million?
 
Yule Waziri aliitws kwenye interview na media flani hapa akaulizwa kuhusu watu kutekwa na kupotea.
Kikubwa alichosema hakuna hayo matukio watu wanazua taharuki kwa kuwa Mama anauburuza mwingi.
Mawaziri wa namna hii hata huyo Mama kuendelea kua nao haimsaidii
Masauni ajiuzulu au achomolewe kinguvu?
 
Acheni kuchezea maisha ya watu

Mnatengeneza mazingira ya wazi kabisa

Kwenda kupoteza maisha ya watu

CCM na serikali Ina sababu gani ya kumteka mtu ambae hata jamii haimjui.

Kila ukiambiwa Samia CDM sio watu wazuri uelewi somo.

Inasikitisha sana huu uhuni wa CDM ifike hatua serikali iache kumchekeq muuaji Mbowe na genge lake
Mtu ametekwa na Polisi, tena ndani ya basi, watu ikiwemo CDM wamepiga kelele kuhusu kutekwa kwa mtu huyo na kutaka Polisi waseme yupo wapi lakini Polisi wakawa kimya, leo anapatikana chumba cha maiti halafu wewe unakuja kuilaumu CDM? Hivi unajisikiliza na kujielewa kweli?
 
Inasikitisha, kama Mungu yupo, kuwa CCM ni tiketi ya moja kwa moja kwenda motoni, hawa watu hawana utu wanachowaza ni dola tu, na hiyo dola sio kwa maslahi ya nchi bali kwa maslahi yao binafsi na ufisadi, Mungu amlaze mahali pema, na hayo ndio matunda ya kizazi walichokilea
 
Back
Top Bottom