TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Hata kama ni CHADEMA, Serikali na Taasisi husika inabidi zichukue hatua na kukomesha huu upuuzi na upumbavu..., mmoja wetu akifa (mwananchi / nguvu kazi) lazima vyombo husika vifuatilie na kuwahoji watuhumiwa no matter their political stance....
Kwa sababu ni mwenye jina na mwenzenu ndio maana mnaongea sana ila sijaona yeyote akitetea watu wasio na sauti huko mtaani.

Kila mtu apambane kivyake Sasa
 
tatzo tuna uhuru wa kwenye makaratasi na sio wa kujitawala maana okoni wa kizungu umetoka saiv tunao wa kwetu binafsi
 
Mods wacheni tutoe tahadhari ili kama wana masiko, basi na wasikie.

Wiki kama mbili zilizopita, yule dada maarufu anaeshi nchini marekani, aliandika katika mtandao wa X makala ndefu ila yenye maneno makali ns matusi mazito juu ya kiongozi fulani kiasi yanayoendelea hapa nchini.

Hata hivyo, kwa haya yanayoendelea, huyu dada sitashangaa akaja na makala nyingine mbaya zaidi na akapata uungwaji mkono mkubwa zaidi.

Anyway, Mungu ana makusudi na kila jambo.
Salary Slip kwani huyu baba waliyemuua alikuwa msemaji sana wa kuipinga serikali?
 
Anaandika Boniyai kutoka Account yake ya X
View attachment 3090046
View attachment 3090047

======


Ali Mohamed Kibao Ameuawa

Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu umekutwa hospitali ya Mkoa wa Kinondoni,Mwananyamala katika chumba cha kuhifadhia maiti mwili wake ukiwa UMEHARIBIWA VIBAYA SANA.

Mwili wa ALI MOHAMED KIBAO ulikutwa umetupwa jana alfajiri maeneo ya UNUNIO (jirani na viwanja vya NSSF) ukiwa na majereha makubwa sehemu za usoni kiasi ndugu zake walipata tabu kuutambua kirahisi.

ALI MOHAMED KIBAO alikamatwa na watu wanao dhaniwa kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi eneo la TEGETA, mbele ya Jengo la KIBO COMPLEX baada ya gari mbili za Jeshi za Polisi za Landcruiser hardtop nyeupe kuzuia (block) basi la TASHIRIF lenye namba T 343 EES alilokuwa amepanda ALI MOHAMED KIBAO kutoka Dar es saalam kuelekea nyumbani kwao Mkoani Tanga.

Kwa bahati nzuri wakati wote wa tukio likitendeka ndani ya gari palikuwa na askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani (Traffic) ambaye alikuwa kiti cha mbele kama abiria na alishuhudia tukio lote, anatambulika kama MACHIWA anayepatikana kwa namba 0652484802.

Namba ya simu aliyokuwa anatumia ALI MOHAMEDKIBAO ni +255 624 724 247 mpaka wakati anatekwa na kwenda kuuwawa,pia ndiyo namba ambayo mara kadhaa waliomteka walikuwa wakimpigia kuhakiki kama ni yeye.

Kwa mujibu wa wenyeji wa UNUNIO ambao ni walima mchicha, wanasema Jana asubuhi walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi baada ya Kuona mwili wa Mtu mzima, mweupe mwenye asili ya Kiarabu ambaye baadae Jana jioni ndugu waliutambua kuwa ni mwili ALI MOHAMED KIBAO ukiwa na majeraha.

Kabla ya umauti wake ALI MOHAMED KIBAO aliwahi kuwa afisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akastaafu na kujiunga na CCM,baadae akachaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Tanga wakati wa Rais Kikwete,na baadae alijiunga CHADEMA.

Baada ya mauaji haya ya Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA na Msaidizi wa Katibu Mkuu kuwawa idadi ya Viongozi wa CHADEMA wakiotekwa inaongezeka
1. Dioniz Kipanya 2. Kombo Bwana Twaha 3. Godwin Mlay 4. Deusdedith Soka 5. Frank Mbise.


Soma Pia:
Boniface Jacob
Ex-Mayor
0712 239 595
Mimi ni mfuasi na mpenzi wa rais SAMIA SULUHU HASSAN.
Napenda nimuombe atoe kauli kuhusu mauaji na utekaji unaoendelea katika taifa letu.
Tukumbuke tu vyama vya siasa vinapita, lakini taifa la Tanzania litaendea kuwepo.
Kulikuwa na vyama vyenye nguvu mfano KANU na ZANU PF.
Leo hii viko wapi?.
 
Mods wacheni tutoe tahadhari ili kama wana masiko, basi na wasikie.

Wiki kama mbili zilizopita, yule dada maarufu anaeshi nchini marekani, aliandika katika mtandao wa X makala ndefu ila yenye maneno makali na matusi mazito juu ya kiongozi fulani kiasi yanayoendelea hapa nchini.

Nilikuwa nasoma na kusisimka, ila kwa tukio hili la leo, siwezi kusisimka tena hata aandike nini.

Nimalizie kwa kusema , kwa haya yanayoendelea, huyu dada sitashangaa akaja na makala nyingine mbaya zaidi na akapata uungwaji mkono mkubwa zaidi.

Anyway, Mungu ana makusudi na kila jambo.
Kiunganisho cha alicho sema
 
Napenda niwe Rais wa Tanzania ili nikomeshe ushenzi huu wa jeshi la polisi.
Nadiriki kuwaita askari polisi,JWTZ au Idara ya usalama wa taifa wanaofanya vitendo hivi wapumbavu.
Siku si nyingi MUNGU atawalipa wao na wanaowatuma.
AMINA.
 
Back
Top Bottom