Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa sababu ni mwenye jina na mwenzenu ndio maana mnaongea sana ila sijaona yeyote akitetea watu wasio na sauti huko mtaani.Hata kama ni CHADEMA, Serikali na Taasisi husika inabidi zichukue hatua na kukomesha huu upuuzi na upumbavu..., mmoja wetu akifa (mwananchi / nguvu kazi) lazima vyombo husika vifuatilie na kuwahoji watuhumiwa no matter their political stance....
Salary Slip kwani huyu baba waliyemuua alikuwa msemaji sana wa kuipinga serikali?Mods wacheni tutoe tahadhari ili kama wana masiko, basi na wasikie.
Wiki kama mbili zilizopita, yule dada maarufu anaeshi nchini marekani, aliandika katika mtandao wa X makala ndefu ila yenye maneno makali ns matusi mazito juu ya kiongozi fulani kiasi yanayoendelea hapa nchini.
Hata hivyo, kwa haya yanayoendelea, huyu dada sitashangaa akaja na makala nyingine mbaya zaidi na akapata uungwaji mkono mkubwa zaidi.
Anyway, Mungu ana makusudi na kila jambo.
Daaaa aliondoka mwehu sasa kaja lucipherKuna tatizo kubwa katika Taifa letu.
Hatuko salama tena.
Mimi ni mfuasi na mpenzi wa rais SAMIA SULUHU HASSAN.Anaandika Boniyai kutoka Account yake ya X
View attachment 3090046
View attachment 3090047
======
Ali Mohamed Kibao Ameuawa
Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu umekutwa hospitali ya Mkoa wa Kinondoni,Mwananyamala katika chumba cha kuhifadhia maiti mwili wake ukiwa UMEHARIBIWA VIBAYA SANA.
Mwili wa ALI MOHAMED KIBAO ulikutwa umetupwa jana alfajiri maeneo ya UNUNIO (jirani na viwanja vya NSSF) ukiwa na majereha makubwa sehemu za usoni kiasi ndugu zake walipata tabu kuutambua kirahisi.
ALI MOHAMED KIBAO alikamatwa na watu wanao dhaniwa kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi eneo la TEGETA, mbele ya Jengo la KIBO COMPLEX baada ya gari mbili za Jeshi za Polisi za Landcruiser hardtop nyeupe kuzuia (block) basi la TASHIRIF lenye namba T 343 EES alilokuwa amepanda ALI MOHAMED KIBAO kutoka Dar es saalam kuelekea nyumbani kwao Mkoani Tanga.
Kwa bahati nzuri wakati wote wa tukio likitendeka ndani ya gari palikuwa na askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani (Traffic) ambaye alikuwa kiti cha mbele kama abiria na alishuhudia tukio lote, anatambulika kama MACHIWA anayepatikana kwa namba 0652484802.
Namba ya simu aliyokuwa anatumia ALI MOHAMEDKIBAO ni +255 624 724 247 mpaka wakati anatekwa na kwenda kuuwawa,pia ndiyo namba ambayo mara kadhaa waliomteka walikuwa wakimpigia kuhakiki kama ni yeye.
Kwa mujibu wa wenyeji wa UNUNIO ambao ni walima mchicha, wanasema Jana asubuhi walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi baada ya Kuona mwili wa Mtu mzima, mweupe mwenye asili ya Kiarabu ambaye baadae Jana jioni ndugu waliutambua kuwa ni mwili ALI MOHAMED KIBAO ukiwa na majeraha.
Kabla ya umauti wake ALI MOHAMED KIBAO aliwahi kuwa afisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akastaafu na kujiunga na CCM,baadae akachaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Tanga wakati wa Rais Kikwete,na baadae alijiunga CHADEMA.
Baada ya mauaji haya ya Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA na Msaidizi wa Katibu Mkuu kuwawa idadi ya Viongozi wa CHADEMA wakiotekwa inaongezeka
1. Dioniz Kipanya 2. Kombo Bwana Twaha 3. Godwin Mlay 4. Deusdedith Soka 5. Frank Mbise.
Soma Pia:
Boniface Jacob
- CHADEMA: Mzee Ally Kibao ametekwa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama akiwa kwenye basi. Usalama wa Taifa waeleze alipo
- Polisi: Tunachunguza kubaini chanzo na watu waliohusika kumchukua Ally Kibao
Ex-Mayor
0712 239 595
Mimi mwenyewe hata sielewi mkuu.Salary Slip kwani huyu baba waliyemuua alikuwa msemaji sana wa kuipinga serikali?
hakuna abiria aliyepiga picha jamani?Kwa bahati nzuri wakati wote wa tukio likitendeka ndani ya gari palikuwa na askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani (Traffic) ambaye alikuwa kiti cha mbele kama abiria na alishuhudia tukio lote, anatambulika kama MACHIWA
MajaribuMimi mwenyewe hata sielewi mkuu.
Inauma mno mkuu, pole kwa wote mlioguswa.Inaumiza sana kumpoteza mtu bila sababu za msingi moyo wangu unavuja damu jamani...uwii
Hakuwa hivyo, basi tu. Mambo kama haya ndio yanazalishaga waasi kwenye nchi.Salary Slip kwani huyu baba waliyemuua alikuwa msemaji sana wa kuipinga serikali?
Hivi mtumishi wa umma hasa askari haruhusiwi kuwa mwanachama wa chama cha upinzani?Hadi kuzuia basi inaonekana kulikuwa na shutuma nzito ikizingatiwa bwana huyu amewahi kuwa mtumishi wa umma(Askari) kule unalishwa viapo vya kutunza Siri.
Pole yake na ndugu zake
Kiunganisho cha alicho semaMods wacheni tutoe tahadhari ili kama wana masiko, basi na wasikie.
Wiki kama mbili zilizopita, yule dada maarufu anaeshi nchini marekani, aliandika katika mtandao wa X makala ndefu ila yenye maneno makali na matusi mazito juu ya kiongozi fulani kiasi yanayoendelea hapa nchini.
Nilikuwa nasoma na kusisimka, ila kwa tukio hili la leo, siwezi kusisimka tena hata aandike nini.
Nimalizie kwa kusema , kwa haya yanayoendelea, huyu dada sitashangaa akaja na makala nyingine mbaya zaidi na akapata uungwaji mkono mkubwa zaidi.
Anyway, Mungu ana makusudi na kila jambo.
Ndio , alikuwa ofisa wa jwtz na ofisa that means alikuwa na cheo cha kuanzia nyota mojaAlikuwa afisa mstaafu wa JWTZ?