TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Mods wacheni tutoe tahadhari ili kama wana masiko, basi na wasikie.

Wiki kama mbili zilizopita, yule dada maarufu anaeshi nchini marekani, aliandika katika mtandao wa X makala ndefu ila yenye maneno makali na matusi mazito juu ya kiongozi fulani kiasi yanayoendelea hapa nchini.

Nilikuwa nasoma na kusisimka, ila kwa tukio hili la leo, siwezi kusisimka tena hata aandike nini.

Nimalizie kwa kusema , kwa haya yanayoendelea, huyu dada sitashangaa akaja na makala nyingine mbaya zaidi na akapata uungwaji mkono mkubwa zaidi.

Anyway, Mungu ana makusudi na kila jambo.
Tujuze Nini ameandika si wotote tuko x
 
Hii nchi bila kuwang'oa hawa mbwa mwitu (ccm ) toka madarakani ,hii nchi tunapoelekea ni kubaya sana , huo nchi inaenda kuwa banana republic kama Burundi na kwingine huko mashenzini ambapo political assassinations ni kugusa tu ,watu wanauawa kama kumbikumbi na kutupwa kama mizoga ya mahayawani ,
Kiufupi maisha ya binadamu hayana thamani tena nchi hii .Hii culture ya impunity iliyotengenezwa ni mbaya mno
 
Anaandika Boniyai kutoka Account yake ya X
View attachment 3090046
View attachment 3090047

======


Ali Mohamed Kibao Ameuawa

Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu umekutwa hospitali ya Mkoa wa Kinondoni,Mwananyamala katika chumba cha kuhifadhia maiti mwili wake ukiwa UMEHARIBIWA VIBAYA SANA.

Mwili wa ALI MOHAMED KIBAO ulikutwa umetupwa jana alfajiri maeneo ya UNUNIO (jirani na viwanja vya NSSF) ukiwa na majereha makubwa sehemu za usoni kiasi ndugu zake walipata tabu kuutambua kirahisi.

ALI MOHAMED KIBAO alikamatwa na watu wanao dhaniwa kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi eneo la TEGETA, mbele ya Jengo la KIBO COMPLEX baada ya gari mbili za Jeshi za Polisi za Landcruiser hardtop nyeupe kuzuia (block) basi la TASHIRIF lenye namba T 343 EES alilokuwa amepanda ALI MOHAMED KIBAO kutoka Dar es saalam kuelekea nyumbani kwao Mkoani Tanga.

Kwa bahati nzuri wakati wote wa tukio likitendeka ndani ya gari palikuwa na askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani (Traffic) ambaye alikuwa kiti cha mbele kama abiria na alishuhudia tukio lote, anatambulika kama MACHIWA anayepatikana kwa namba 0652484802.

Namba ya simu aliyokuwa anatumia ALI MOHAMEDKIBAO ni +255 624 724 247 mpaka wakati anatekwa na kwenda kuuwawa,pia ndiyo namba ambayo mara kadhaa waliomteka walikuwa wakimpigia kuhakiki kama ni yeye.

Kwa mujibu wa wenyeji wa UNUNIO ambao ni walima mchicha, wanasema Jana asubuhi walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi baada ya Kuona mwili wa Mtu mzima, mweupe mwenye asili ya Kiarabu ambaye baadae Jana jioni ndugu waliutambua kuwa ni mwili ALI MOHAMED KIBAO ukiwa na majeraha.

Kabla ya umauti wake ALI MOHAMED KIBAO aliwahi kuwa afisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akastaafu na kujiunga na CCM,baadae akachaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Tanga wakati wa Rais Kikwete,na baadae alijiunga CHADEMA.

Baada ya mauaji haya ya Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA na Msaidizi wa Katibu Mkuu kuwawa idadi ya Viongozi wa CHADEMA wakiotekwa inaongezeka
1. Dioniz Kipanya 2. Kombo Bwana Twaha 3. Godwin Mlay 4. Deusdedith Soka 5. Frank Mbise.


Soma Pia:
Boniface Jacob
Ex-Mayor
0712 239 595
Kila raia ajiinde yeye mwenyewe.
Akija mtu kukuchukua bila utaratibu hakikisha unapambana mpaka mwisho, are yeye au wewe.
 
Mimi nadhani ifike muda hawa viongozi wa chadema waache kupoteza muda kupambania haki za watanzania ambao wengi ni wajinga na machawa.

Waafrika hasa watanzania si watu wa kuwahangaikia na kuwatetea kupigania haki na maslahi yao.

Ni kuwaacha na mashida yao na matatizo yao yawapige kisawasawa mpaka pale akili zao zitakapo funguka.

Hakuna haja ya kupoteza uhai wako kuwatetea wajinga wasiojitambua.
 
Unaonekana unatafuta mtu wa kukuf!ra
IMG_7567.jpeg


Muda sahihi ukifika watakwambia kazaliwa na nyota huyo

Miezi miwili nyuma Othman former DG wa TISS akielekea NY alisimama hapa na kuongea na rafiki zake wanataka nije huko.

Siwezi kukusaidia kwenye umaskini wako ndugu.
 
Kwa sababu ni mwenye jina na mwenzenu ndio maana mnaongea sana ila sijaona yeyote akitetea watu wasio na sauti huko mtaani.

Kila mtu apambane kivyake Sasa
Mwezenu kina nani ? Ofcourse mimi kama mtanzania na binadamu; binadamu mwenzangu akipatwa na majanga ni mwenzangu..., nakushangaa wewe ambaye unaona mtu sio mwenzako sababu ya itikadi; nachelea kusema ndugu yangu unapotoka...

By the way sina chama cha siasa Tanzania kwangu mimi ninayeendeshwa na ideologia practically sioni tofauti ya Vyama vyote Nchini
 
Dkt Samia Suluhu Hassani haya yanayifanyika kwenye nchi hii waona mazuri? Hili halikubaliki siyo kwa mtu mwenye utu uwe CHADEMA, CCM,ACT-WAZALENDO ili jambo ni lakinyama sana.
Kamwe damu ya mtu haiendi bure. Inamlilia muuaji, wauaji, na wale wote wenye mamlaka juu usalama wa watu.

Muda utaongea, na karma lazima itajibu tu. Kiganja cha mkono tayari kimeshaandika ukutani,

MENE, MENE, TEKELI & PERESI
 
IGP na jopo lake wajitafakari naona kazi wameshindwa kabisa. Kila siku vifo, watu kutekwa, kuuawa na kupotea.

Tunaelekea wapi?
Siyo kazi wameshindwa ,hii kazi wanafanya wao wakishirikiana na vikosi vya mauaji vya TISS , kama mlifuatilia ile sheria mpya iliyopitishwa ya kuwalinda watu Wa TISS dhidi ya kushitakiwa mwaka jana ,ile ilikuwa ni maandalizi ya kinachoendelea sasa hivi .
Ccm ni ile ile , bloody murderers and criminals
 
Back
Top Bottom