TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

ALI MOHAMED KIBAO AMEUWAWA..!

Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu umekutwa hospitali ya Mkoa wa Kinondoni,Mwananyamala katika chumba cha kuhifadhia maiti mwili wake ukiwa UMEHARIBIWA VIBAYA SANA.

Mwili wa ALI MOHAMED KIBAO ulikutwa umetupwa jana alfajiri maeneo ya UNUNIO (jirani na viwanja vya NSSF) ukiwa na majereha makubwa sehemu za usoni kiasi ndugu zake walipata tabu kuutambua kirahisi.

ALI MOHAMED KIBAO alikamatwa na watu wanao dhaniwa kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi eneo la TEGETA, mbele ya Jengo la KIBO COMPLEX baada ya gari mbili za Jeshi za Polisi za Landcruiser hardtop nyeupe kuzuia (block) basi la TASHIRIF lenye namba T 343 EES alilokuwa amepanda ALI MOHAMED KIBAO kutoka Dar es saalam kuelekea nyumbani kwao Mkoani Tanga.

Kwa bahati nzuri wakati wote wa tukio likitendeka ndani ya gari palikuwa na askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani (Traffic) ambaye alikuwa kiti cha mbele kama abiria na alishuhudia tukio lote ,anatambulika kama MACHIWA anayepatikana kwa namba 0652484802.

Namba ya simu aliyokuwa anatumia ALI MOHAMEDKIBAO ni +255 624 724 247 mpaka wakati anatekwa na kwenda kuuwawa,pia ndiyo namba ambayo mara kadhaa waliomteka walikuwa wakimpigia kuhakiki kama ni yeye.

Kwa mujibu wa wenyeji wa UNUNIO ambao ni walima mchicha,wanasema Jana asubuhi walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi baada ya Kuona mwili wa Mtu mzima,mweupe mwenye asili ya Kiarabu ambaye baadae Jana jioni ndugu waliutambua kuwa ni mwili ALI MOHAMED KIBAO ukiwa na majeraha.

Kabla ya umauti wake ALI MOHAMED KIBAO aliwahi kuwa afisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akastaafu na kujiunga na CCM,baadae akachaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Tanga wakati wa Rais Kikwete,na baadae alijiunga CHADEMA.

Baada ya mauaji haya ya Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA na Msaidizi wa Katibu Mkuu kuwawa idadi ya Viongozi wa CHADEMA wakiotekwa inaongezeka
1.Dioniz Kipanya 2.Kombo Bwana Twaha 3.Godwin Mlay 4.Deusdedith Soka 5.Frank Mbise.

Boniface Jacob
Ex-Mayor
0712 239 595

Hao ni wapinzani wanataka kumpa shida Rais. Mama anaupiga mwingi sana. Ni wivu tu. Huyo kama angeamua kutulia ccm asingekutwa na hayo mauji. Kihere here chake kwenda upinzani. Na Wanamzingua mama sasa naye akiwazingua hamna kulia lia
 
thecitizen.co.tz
https://www.thecitizen.co.tz › news
Body resembling missing Tanzanian opposition politician found at Dar es ...
1725793878614.png

Archieve Photo : Mzee Ali Kibao

2 hours ago — The opposition Chadema said on Sunday that the family of Ali Kibao's has been informed of a body resembling Kibao's who was abducted by armed gang... he was forcefully taken from his sit on a packed luxurious coach bus while travelling from the ocommercial city Dar es Salaam to Tanga .... in front of dozens of fellow travellers handcuffed bundled into a motorcar... the abductors identified themselves as police officers...
 
Kulaumu basi la Tashriff ni kujaribu kuukimbia mzizi wa fitina tu (trying to project the problem).

Kizimkazi ndiyo shida hapa.
You are very right ndugu Sexless...

Hii ya Kizimkazi as it is now bado ni "circumstantial evidence" ambayo kwa 100% inabeba kweli yote ya mauaji haya, shida ipo huko....

However ili tufike kwenye actual evidence ya kuwa - convict kisiasa na kisheria huyu Kizimkazi, lazima pawepo pa kuanzia....

Tukio hili la kuuwawa Mzee Kibao, liko wazi mno na mazingira yake ingalau ni tofauti kabisa na yale wengine waliochukuliwa na kuuwawa na wengine haijulikani wako wapi, hai ama wafu...

Tashriff bus, dereva, wafanyakazi wa bus hilo na abiria waliokuwa humo watasaidia uchunguzi kuwajua hawa majambazi/magaidi unless polisi wa kweli na halisi wasitake hilo kufanyika...!!
 
ALI MOHAMED KIBAO AMEUWAWA..!

Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu umekutwa hospitali ya Mkoa wa Kinondoni,Mwananyamala katika chumba cha kuhifadhia maiti mwili wake ukiwa UMEHARIBIWA VIBAYA SANA.

Mwili wa ALI MOHAMED KIBAO ulikutwa umetupwa jana alfajiri maeneo ya UNUNIO (jirani na viwanja vya NSSF) ukiwa na majereha makubwa sehemu za usoni kiasi ndugu zake walipata tabu kuutambua kirahisi.

ALI MOHAMED KIBAO alikamatwa na watu wanao dhaniwa kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi eneo la TEGETA, mbele ya Jengo la KIBO COMPLEX baada ya gari mbili za Jeshi za Polisi za Landcruiser hardtop nyeupe kuzuia (block) basi la TASHIRIF lenye namba T 343 EES alilokuwa amepanda ALI MOHAMED KIBAO kutoka Dar es saalam kuelekea nyumbani kwao Mkoani Tanga.

Kwa bahati nzuri wakati wote wa tukio likitendeka ndani ya gari palikuwa na askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani (Traffic) ambaye alikuwa kiti cha mbele kama abiria na alishuhudia tukio lote ,anatambulika kama MACHIWA anayepatikana kwa namba 0652484802.

Namba ya simu aliyokuwa anatumia ALI MOHAMEDKIBAO ni +255 624 724 247 mpaka wakati anatekwa na kwenda kuuwawa,pia ndiyo namba ambayo mara kadhaa waliomteka walikuwa wakimpigia kuhakiki kama ni yeye.

Kwa mujibu wa wenyeji wa UNUNIO ambao ni walima mchicha,wanasema Jana asubuhi walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi baada ya Kuona mwili wa Mtu mzima,mweupe mwenye asili ya Kiarabu ambaye baadae Jana jioni ndugu waliutambua kuwa ni mwili ALI MOHAMED KIBAO ukiwa na majeraha.

Kabla ya umauti wake ALI MOHAMED KIBAO aliwahi kuwa afisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akastaafu na kujiunga na CCM,baadae akachaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Tanga wakati wa Rais Kikwete,na baadae alijiunga CHADEMA.

Baada ya mauaji haya ya Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA na Msaidizi wa Katibu Mkuu kuwawa idadi ya Viongozi wa CHADEMA wakiotekwa inaongezeka
1.Dioniz Kipanya 2.Kombo Bwana Twaha 3.Godwin Mlay 4.Deusdedith Soka 5.Frank Mbise.

Boniface Jacob
Ex-Mayor
0712 239 595
Dah kifo cha huyu mwamba kimeniuma sana.
 
Nimetoka Kanisani baada ya Ibada ya J.pili, nafika nyumbani na kutengewa chakula nikasema nisome tarifa mpya za leo, naingia nimekuta uzi huu wa majonzi na masikitiko, mbona nimeshindwa kula, maana naamini, Mtanzania ni ndugu yangu, thamani yangu ambayo Mungu ameniungamanisha nayo

Kwa sababu hiyo, mmoja wapo anapo uwawa namna hiyo, kama binadamu na Mtanzania, naungamanika na huzuni na majonzi ya kumpoteza mwenzetu

Inauma mno hasa inapokuwa Mtanzania mwenzetu ameuwawa kikatili na hakuna sababu yoyote mbaya ya yeye kuuwawa, na kwamba labda ni mhaini, hapana, ni jambazi, hapana, ni nini basii 😪

Kikombe cha damu katika nchi hii juu ya wao wafanyayo hayo, Mungu wetu, bado hakijajaa na wewe ukashusha ghadhabu yako juu yao?

Inuka Mungu mwenye nguvu, ukomeshaye mateso ya watu wako, Wewe ndio mtoa hukumu ya haki, Tutetee tusio na mtetezi Jehova

Inauma saana
 
Usikute serikali yenye madaraka imekabidhi nchi kwa wahuni au genge fulani?

Pengine tushauzwa au tumepigwa mnada na hatujielewi?

Kwa kinachoendelea huenda nchi ipo kwenye Autopilot mode wakati huo program imekuwa hacked na wahuni.?
 
Hao ni wapinzani wanataka kumpa shida Rais. Mama anaupiga mwingi sana. Ni wivu tu. Huyo kama angeamua kutulia ccm asingekutwa na hayo mauji. Kihere here chake kwenda upinzani. Na Wanamzingua mama sasa naye akiwazingua hamna kulia lia
Umewahi kuona anatoka hadharani kukemea?
 
Tutukanane tupigane lakini kitendo cha kutoa uhai wa mtu ni uhaini wa hali ya juu hakuna mbadala wa uhai. Hakuna atakaye ishi milele na waliofanya tukio hili karma itawafuata tu
 
Rais mbona yupo kimnya au haingii mtandaoni haewezekani matukio yapo tena mengine unaona ni wazi kabisa lakini kiongozi upo kimnya tu, ni nini maana yake?
 
Hii hali imekuwa mbaya sana, nadhani sasa ifike mahala mtu akitekwa hadharani kama mzee huyu, wananchi waingilie kati na ikiwezekana mbwai na iwe mbwai maana hali ni mbaya vinginevyo raia tutaumizwa sana hasa watu wanaotoa mawazo mbadala KWa serikali na kuitwa wakosoaji.
Nawapa pole sana familia,ndugu,jamaa,marafiki na wana chadema KWa kumpoteza mzee wetu na mtanzania mwenzetu,Mungu ampe pumziko la milele.
 
Tungekuwa na Bunge madhubuti huu utekaji na uuaji ungekoma...Tuna ceremonial Parliament
 
Kuwa chadema sasa wanabeba silaha hadharan wanaenda kuteka mabas ili kubeba raia acha ujinga we dogo njaa zisikufanye ivo
Ndio msingi wa hadithi inaanza basi lilisimamishwa na watu waliovaa kiraia.

Ikifika kwa msimuliaji wa kumi waliosimamisha basi walikuwa wamevaa kijeshi, kulikuwa na defender saba, askari wamevaa mitutu and so forth.

Mnyika habari za kutekwa kwa huyo jamaa alizipata wapi kwa haraka sana na ku-post? Kulikuwa na watu wenye number yake ndani ya bus hadi apewe taarifa mara baada ya tukio tu.

Hii senima ni rahisi sana polisi wakianza na kuchunguza mawasiliano wa viongozi wa CDM. Wahusika ni CDM
 
Back
Top Bottom