TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Anaandika Boniyai kutoka Account yake ya X
View attachment 3090046
View attachment 3090047

======


Ali Mohamed Kibao Ameuawa

Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu umekutwa hospitali ya Mkoa wa Kinondoni,Mwananyamala katika chumba cha kuhifadhia maiti mwili wake ukiwa UMEHARIBIWA VIBAYA SANA.

Mwili wa ALI MOHAMED KIBAO ulikutwa umetupwa jana alfajiri maeneo ya UNUNIO (jirani na viwanja vya NSSF) ukiwa na majereha makubwa sehemu za usoni kiasi ndugu zake walipata tabu kuutambua kirahisi.

ALI MOHAMED KIBAO alikamatwa na watu wanao dhaniwa kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi eneo la TEGETA, mbele ya Jengo la KIBO COMPLEX baada ya gari mbili za Jeshi za Polisi za Landcruiser hardtop nyeupe kuzuia (block) basi la TASHIRIF lenye namba T 343 EES alilokuwa amepanda ALI MOHAMED KIBAO kutoka Dar es saalam kuelekea nyumbani kwao Mkoani Tanga.

Kwa bahati nzuri wakati wote wa tukio likitendeka ndani ya gari palikuwa na askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani (Traffic) ambaye alikuwa kiti cha mbele kama abiria na alishuhudia tukio lote, anatambulika kama MACHIWA anayepatikana kwa namba 0652484802.

Namba ya simu aliyokuwa anatumia ALI MOHAMEDKIBAO ni +255 624 724 247 mpaka wakati anatekwa na kwenda kuuwawa,pia ndiyo namba ambayo mara kadhaa waliomteka walikuwa wakimpigia kuhakiki kama ni yeye.

Kwa mujibu wa wenyeji wa UNUNIO ambao ni walima mchicha, wanasema Jana asubuhi walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi baada ya Kuona mwili wa Mtu mzima, mweupe mwenye asili ya Kiarabu ambaye baadae Jana jioni ndugu waliutambua kuwa ni mwili ALI MOHAMED KIBAO ukiwa na majeraha.

Kabla ya umauti wake ALI MOHAMED KIBAO aliwahi kuwa afisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akastaafu na kujiunga na CCM,baadae akachaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Tanga wakati wa Rais Kikwete,na baadae alijiunga CHADEMA.

Baada ya mauaji haya ya Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA na Msaidizi wa Katibu Mkuu kuwawa idadi ya Viongozi wa CHADEMA wakiotekwa inaongezeka
1. Dioniz Kipanya 2. Kombo Bwana Twaha 3. Godwin Mlay 4. Deusdedith Soka 5. Frank Mbise.


Soma Pia:
Boniface Jacob
Ex-Mayor
0712 239 595
Samia, Samia, Samia. Nimekuita màra tatu, mda utaongea zaidi
 
Tatizo sio JPM na wala sio Sa100. Tatizo ni mfumo, haya yote yalitokea na yanaendelea kutokea kwa sababu ya mifumo chini ya serikali ya chama cha kijani na wapo kimya. Inasikitisha sana sijui kama taifa tunaelekea wapi kama serikali inashindwa kuhakikisha raia wake wanakuwa salama.
Hapa naona serikali inapambania usalama wake yenyew na sio usalama wa raia,..
 
Hatuna Rais ndugu yangu, umeshawahi kusikia akitoa kauli yoyote ya KUTOKOMEZA UDHALIMU huo?
Anatakiwa kutoa kauli nakubaliana na wewe kabisa.

Lakini yeye kuhusika nakataa mbinu yake na Abdul ni 👇

IMG_7569.jpeg


Ni carrot on the stick kuhonga watu. Hiyo ni kwa mujibu wa Lissu na hata wanaharakati waliofuatwa.

Utekaji na kuuwa watu sio style yake
 
Kama MTU anatekwa Katikati ya mji, kitovu cha Nchi! Anauwawa na mwili wake unatupwa Jirani tu hapa, je tuko salama kama Nchi?? Who's next? Tunajuaje usalama WA VIONGOZI wetu kama upo? Ununio na magogoni sio mbali, ununio kuna VIONGOZI wakubwa Sana wanaishi huko, je usalama wao ukoje?? Haya wacha tuone who's next....
Inasikitisha sana...
 
Sio watawamaliza wenzetu wewe na Mimi hatuko salama, kwakua hakuna asiye na adui, adui yako atakufanyia unyama kwakua anajua watajua umetekwa na watekaji kama ilivyo anza kuzoeleka
 
J
Tatizo sio JPM na wala sio Sa100. Tatizo ni mfumo, haya yote yalitokea na yanaendelea kutokea kwa sababu ya mifumo chini ya serikali ya chama cha kijani na wapo kimya. Inasikitisha sana sijui kama taifa tunaelekea wapi kama serikali inashindwa kuhakikisha raia wake wanakuwa salama.
jpm ndio alianzisha hivi vitengo vya kuua wapinzani na wakosoaji wake..huyu mama shungi yeye nae kaiga kuua ila policeccm wajue nao ni binadamu yana mwisho na mwisho wake ni mbaya sana
 
Mtakao tekwa hapo baadae. Hakikisheni mnakuwa na kauli nzuri na kuomba msamaha..

Hii kujifanya Chuma na mbobevu wa itikadi wanakuua hawa jamaa.
 
Utekaji wa kipindi cha Jiwe ndio utekaji wa hovyo zaidi kwakua ndio ulikua mwanzo was mfumo huu wa hovyo na ovu wa kupoteza watu wenye mawazo mbadala na Serikali, utekaji huu ni mwendelezo wa utakaji ulio anzishwa na Jiwe, wameanzia walipo ishia wakati ule, watu wanatekwa na kuua wa hakuna anaye Kali, sasa tofauti ya Tanzania na Sudan ni ipi?!?
Yule waziri, wizara imemshinda.
Samia anayafurahia haya mambo.
Naanza kuona bora utekaji wa kipindi cha magufuli. Nilijua mwiulu mchemba ndio wazuri mbovu wa mambo ya mdani kuliko wote waliopita kumbe nilikuwa najidanganya.
 
Magufuli alisha ustikia huu mchezo.

Kuna kijana CDM Mbeya uchaguzi uliopita walimteka hivi hivi na kumpotezea maisha yake.

Ikabidi Magufuli akaombe msamaha kwa ile familia na kuwapa pole (Lakini hela) aifidii maisha ya mtu.

Chadema na genge lenu la wahusika huko serikalini acheni huu ushenzi. Ushindi aupatikani kwa njia hizi za udhalimu.

R.I..P
Umeandika tuhuma nzito sana, je una ushahidi nazo? Au unafanya character assassination?
 
Anatakiwa kutoa kauli nakubaliana na wewe kabisa.

Lakini yeye kuhusika nakataa mbinu yake na Abdul ni 👇

View attachment 3090223

Ni carrot on the stick kuhonga watu. Hiyo ni kwa mujibu wa Lissu na hata wanaharakati waliofuatwa.

Utekaji na kuuwa watu sio style yake
Kama sio style yake huyu mbona hachukuliwi hatua?
Six5b0TZWlBbGx71.jpg
 
Kama mtu amechukuliwa na polisi mbele ya umma bnankuoatikana akiwa amefariki kuna uhalali wa viongozi wa polisi kuendelea kushika madaraka ya uongozi kuanzia waziri na mkuu wa polisi?
Hao wanafanya kwa maelekezo ya mama ndio mana unaskia taarabu zake majukwani kua watu wanajiteka...yeye ndio kila kitu ndio mana kwenye vitabu vya dini hakuna nabii mwanamke
 
Back
Top Bottom