TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Katika hali yoyote ile, Waziri wa mambo ya ndani ya nchi kuendelea kuwa ofisini hadi muda huu ni dharau na kejeli kubwa kwa Watanzania.

Mkuu wa Polisi pia afanye maamuzi magumu japo sioni kama ni magumu, yeye kuendelea kuwa katika nafasi hiyo pia ni aibu kwake na mzigo mzito.

Tunaelekea wapi kaka taifa? Sijui!
taifa lilishapoteza muelekeo linajiendea mfano wa maiti inayoelea baharini
 
👊💪tupo pamoja gentleman,

nakubali kupingwa kwa hoja, but why all this at a time of chadema elections?🐒
Tatizo bado liko kwa vyombo vyetu vya ulinzi wa raia na mali zao...mbona tangu enzi ya JPM watu wanapigwa risasi na wengi kuuawa, hivi vyombo havijawahi kumkamata yeyote kuhusiana na haya matukio!?

Wataendelea kuonekana ni wao mpaka watakapotuletea wahusika.
 
Ushahidi wa mazingira na mahali pa kuanzia pako wazi kabisa, kuwa wanaohusika na kuteka na kuua ni walewale waliosema kuwa mtu unashinda mtandaoni na kikalamu chako ukimtukana rais wetu tukiwapoteza polisi msiwatafute makofi kwa CCM makofi pwaa pwaa,na hutasikia polisi wamewaita na kuwahoji kuhusiana na yanayotokea nchini.
 
Kinachosikitisha zaidi anaepaswa kukemea anasema ni maigizo.
Screenshot_20240908_160716.jpg
 
1. Ma-Bus mengi ya abiria kwa sasa yana Camera, papo pa kuanzia, kama vyombo vya sheria vitaingia kigugumizi kung'amua hili, jamii sasa iwahukumu wadharimu ambao kwa dhahiri nyuso zao zitakuwa zimeonekana kwenye camera za bus au kwa mtu yyt ambaye aliweza kunasa tukio hili.

2. Polisi kujitoa kwenye hili ni dhahiri wanatakiwa kujua chombo kipi kwa mamlaka yapi wanaweza tumia namba zao za magari, after roll Namba ya gari la Polisi itakuwa ilionekana wazi, papo pa kuanzia.

IFIKE MAHALI TUSEME INATOSHA!!
Mkuu, shida sio ushahidi mbona
Shida ni kwamba wanaotakiwa wachukue hatua ndio wahusika
Kama shida ni ushahidi ile kesi ya wale askari watano waliombaka na kumlawiti yule bint ingelikua imekwisha muda
 
Hapo mnaamini kuwa kutakuwa na uchaguzi huru na haki?,Kama watu wanatekwa Kama kuku na kupotezwa.waliisha zoea kula nyama za watu lakini ipo siku watageuka kula nyama za watoto wao wenyewe baada ya kumaliza kula za watu wengine.
Wataanza kulana wao kwa wao nasikiaga tu nyama ya mtu tamu Ina Chumvi nyingi,
 
Raia Samia hajatoa kauli thabiti dhidi ya kundi hili la kigaidi linaloendelea kufanya uhalifu wa kuteka na kuua raia wasio na hatua....

Aidha polisi wameendelea kutoa kauli tata, zilizobeba mizaha, kutojali na zinazoonesha "zero responsibility" kwa Jeshi la Police kinyume kabisa na wajibu wao wa kisheria na kikatiba.......

Kwa niaba ya raia wenzangu, naomba serikali kwa ujumla (Rais Samia Suluhu Hassan) na specific Jeshi la police wajibu maswali haya muhimu ya wananchi:

1. Kazi na jukumu la msingi la Jeshi la Police ni kulinda Usalama wa raia na Mali zao. Kazi yenu polisi pia hutekekezwa kutumia intellejensia ya kunusa uhalifu, kisha kuchunguza, kudhibiti na kukamata wahalifu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Kama hizi ndizo kazi zenu, ni kwanini mauaji haya yanaendelea na ninyi mkiwa mpo kimya tu....?

2. Genge hili la ugaidi linaloendesha shughuli zake mchana kweupe, kila linapomlenga mtu fulani na likimfikia hujitambulisha kuwa ni "police" wakitumia magari ya kifahari sana na wakati mwingine ya Jeshi polisi kwa sura na usajili wa namba zao. Swali muhimu ni hili, kwamba, inakuwaje genge hili la kihalifu linalojitambulisha kama "police" pale linapotenda uhalifu wake mchana kweupe na nyie polisi halisi hamfanyi kuchukua hatua zozote kuwatia mikononi mwenu wauaji hawa...?

3. Serikali (Rais Samia Suluhu Hassan), TANPOL na Waziri wa mapolisi ndugu Masauni, Je mmeshindwa kulinda uhai wa raia? Mnafanya nini kwenye ofisi zetu za umma kama genge hili la ugaidi limewashinda nguvu kiasi cha kujiona lenyewe ndiyo serikali? Kwanini mnadhani mnastahili kuaminika ktk mazingira haya?

##Rais Samia Suluhu Hassan toka mafichoni, acha kuwa chura kiziwi wa Kizimkazi waambie raia kuwa wewe na serikali yako mmeshashindwa kazi, mmeshindwa kutumia vyombo vya ulinzi kutulinda uhai wa watu ili kila mtu achukue hatua binafsi za kujilinda muone kama tutashindwa....!

======================================
UPDATES:


Hatimaye Rais Samia Suluhu Hassan amesikia na kutoka huko alikojificha na kutoa kauli.....

Si kauli thabiti kivile, yenye mamlaka na kumaanisha, lakini ingalau kasikia kilio cha umma na kusema neno japo inaonekana Kuna lijamaa limemwandikia tu hii statement, likaweka picha yake na kuitoa mitandaoni👇

Si kauli ya kumaanisha na kuonesha u - serous wa tatizo lililopo kwa sababu TANPOL a.k.a Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) ndiyo watuhumiwa wa kuhusika na kuendesha genge hili la kigaidi linalo teka na kuua raia bila sababu...

Rais Samia Suluhu Hassan Hassan hayuko serous. Anataka kunufaika kisiasa na damu za watu hawa wanaouwawa....
Screenshot_20240908-205726.png
 
Chukua hatua Rais wangu.

Pengine umesahau , wacha nikukumbushe wewe ndie Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote nchini.

Na pengine umesahau wacha nikukumbushe wewe ndie Mwenyekit wa Baraza la mawazir nchini.

Chukua hatua Rais wangu.

Labda umesahau, wacha nikukumbushe wewe ndie uliyemteua Hamadi Masauni kuwa waziri wa Mambo ya ndani.

Naendelea kukumbumbusha Kwa nia njema Rais wangu, wewe ndie uliyemteua Cammililius Wambura kuwa inspeta jenerali wa polisi nchini.

Na kubwa kuliko yote nakukumbusha kuwa yanayotokea nchini yapo kinyume na sheria za duniani Hadi za dini yako.

Chukua hatua Tafadhar.

Bila kuchukua hatua tutaamin yanayotokea Yana Baraka zako na unafurahia .
 
Hao uliowataja ni political appointees tu..ni wangapi walioteuliwa kwenye hizo teuzi waliukuta utekaji na wameondoka bado utekaji upo?

As i have said for many years, there is no political solution in Tanzania
 
Binadamu anapaswa kuheshimiwa kuliko viumbe wote.
Kumzaa na kumlea binadamu hugharimu zaidi ya miaka 18, inakuwaje kukatisha uhai wake kirahisi namna hiyo?
Tunaenda kuifanya Tanzania kuwa shimo la uhalifu kwa sababu ya ubinafsi wa watu wachache.
 
Usalama haupo, swali ni je kifanyike nini dhidi ya yanayoendelea?
Zipo 'options' tatu:
1. Kusalimu amri, kujisalimisha kwa hao wanaopambania ya kwao ili waendelee bila usumbufu
2. Kupuuza tu na kujifanya hakuna lolote linalo sumbua nchi hii
3. Kukataa na kupinga kwa njia mbali mbali zinazoweza kutumika kwa kila mmoja awezavyo, ili mradi njia hizo zisaidie kuondoa tatizo.
 
Unafikiri hajui watu zaidi ya 100 wametekwa. Unafikiri hajui kinachoendelea? Kuna briefing kila siku kuhusu hali ya usalama wa nchi. Huwa mnamfanya kama mtoto, anajua kila kitu. Anaidhinisha.
 
Back
Top Bottom