Chukua hatua Rais wangu.
Pengine umesahau , wacha nikukumbushe wewe ndie Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote nchini.
Na pengine umesahau wacha nikukumbushe wewe ndie Mwenyekit wa Baraza la mawazir nchini.
Chukua hatua Rais wangu.
Labda umesahau, wacha nikukumbushe wewe ndie uliyemteua Hamadi Masauni kuwa waziri wa Mambo ya ndani.
Naendelea kukumbumbusha Kwa nia njema Rais wangu, wewe ndie uliyemteua Cammililius Wambura kuwa inspeta jenerali wa polisi nchini.
Na kubwa kuliko yote nakukumbusha kuwa yanayotokea nchini yapo kinyume na sheria za duniani Hadi za dini yako.
Chukua hatua Tafadhar.
Bila kuchukua hatua tutaamin yanayotokea Yana Baraka zako na unafurahia .