TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Huu ni muendelezo tu ila yeye ndio muasisi wa huu uhuni...na Wala uwezi kumvua Samia na huu uhuni unyama unaoendelea
Hakuna cha mwasisi acheni unafiki wenu!
Nyinyi CHADEMA na baadhi ya maCCM mlikuwa hammpendi JPM na ndo mlikula bia siku ya kifo chake tulieni sindano iwaingie!
Utekaji upo tokea wakati wa Kikwete kumbuka Dr Ulimboka na ukumbuke Media hazikuwepo nyingi ila matukio yalikuwepo!
 
Kuna msemo: karma is real.

Kwa kuzingatia huo msemo, kesho na keshokutwa, linaweza kutokea jambo kama adhabu kwa haya yanayoendelea na hamtoweza kuamini.

Binafsi sitaki kuingia ndani sana kuhusu hilo, balli naacha Nature/muda ndio utaamua.

Swali: Yakitokea, mtataka tuungane kuomboleza?

Jibu: Msijidanyanye, watu watashangilia kwani avunacho mtu, ndicho apandacho.
 
Tatizo sio JPM na wala sio Samia. Tatizo ni mfumo, haya yote yalitokea na yanaendelea kutokea kwa sababu ya mifumo chini ya serikali ya chama cha kijani na wapo kimya. Inasikitisha sana sijui kama taifa tunaelekea wapi kama serikali inashindwa kuhakikisha raia wake wanakuwa salama.

Kwani kiongozi Mkuu ni nani?
Mwenyezi akiangalia Tanzania kiuongozi na usimamizi wa matendo ya haki au dhuruma na udhalimu anaanza kumuangalia nani ?
Nani anapaswa kuchukua hatua za kusimamia misingi ya haki?
Mifumo msemaji sake wa mwisho ni nani ?
 
Watu wanatekwa wanapotea, hawajulikani walipo na tuna waziri wa mambo ya ndani ya nchi na Jeshi lake ambalo ndio limelalamikiwa muda wote. Yupo tu na hajigusi na mamlaka yake ya uteuzi haimgusi, kwamba anafanya kazi nzuri? Hii ni aibu.

Hivi hawa ndio watu wanaotupigia kelele na ving'ora huko barabarani tuwapishe wakimbie? Huwa wanakimbilia wapi?
Inasikitisha sana
 
Hii ndo shida ya Watanzania!! Prove the existence of karma!!

Tunashindwa kujitetea tunasubiri kutetewa na Karma.
Karma? Ya konyo
 
Siku akiuawa kiongozi wa ccm nchi italipuka kwa shangwe. Kwenye kifo cha jiwe polisi ilitumika kuwakamata watu wasile ndafu na kunywa pmbe zao kushangilia .kifo cha dikteta yule.
 
Ile Sheria mpya ya usalama wa taifa kuwekewa Kinga ya kutoshitakiwa ifutwe haraka kwani wahuni wa ccm wanajificha humo.
TLS hebu tuelimishane juu ya umuhimu wa Sheria hivyo kwa taifa letu Kama Haina manufaa basi serikali ilazimishwe kuifuta Sheria hivyo haraka!
 
Chukua hatua Rais wangu.

Pengine umesahau , wacha nikukumbushe wewe ndie Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote nchini.

Na pengine umesahau wacha nikukumbushe wewe ndie Mwenyekit wa Baraza la mawazir nchini.

Chukua hatua Rais wangu.

Labda umesahau, wacha nikukumbushe wewe ndie uliyemteua Hamadi Masauni kuwa waziri wa Mambo ya ndani.

Naendelea kukumbumbusha Kwa nia njema Rais wangu, wewe ndie uliyemteua Cammililius Wambura kuwa inspeta jenerali wa polisi nchini.

Na kubwa kuliko yote nakukumbusha kuwa yanayotokea nchini yapo kinyume na sheria za duniani Hadi za dini yako.

Chukua hatua Tafadhar.

Bila kuchukua hatua tutaamin yanayotokea Yana Baraka zako na unafurahia .
Hamad Massauni tusimuonee.....pale alipo wenye nchi na chama chao hata leo wanaweza kumwondoa hana effect kwenye mambo haya.

Naye anapima upepo tu.

Juzi mahakama imesemaje kwani?Tulitarajia Mamlaka ya kutoa haki" majaji" wangetoa mwongozo juu ya haya.

But who cares?
 
Back
Top Bottom