TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Uchunguzi tulioufanya kwa macho na Masikio yetu ni kwamba, hata wale Chawa wanaoishi kwa kumsifu tu, tangu mauaji yale ya kishamba, Wameufyata, kule mitandoni wanakokesha kumtukuza hawapo tena! ( Hata nyinyi mnawajua )

Unajua hata ungekuwa na njaa kiasi gani, yako mambo mabaya ambayo mfadhili wako akifanya unajikuta Aibu inakupata tu, kuna ubinadamu ambao hata Chawa wanao, kwahiyo hata wewe kama unawalipa lakini ukiboronga wanarudi nyuma na kuona Aibu.

Ngoja tuone mpaka uchaguzi atabaki na % ngapi.
Sasa maajabu ni hayo; kusikia kwamba bado alikuwa na "umaarufu". Umaarufu wa kitu gani hasa!; kuwa 'Chura Kiziwi', au?

Huyu umaarufu wake, kama aliwahi kuwa nao uliishia pale watu walipo gundua kwamba hamna umakini katika jambo lolote lile. Ni kigeugeu wa kusaka kukubalika bila kuwa na sifa za kukubalika.

Usilaumu. Ngoja nikupe mfano mmoja au miwili halisi ya haraka haraka bila hata ya kuchemsha kichwa kukumbuka.

Mbowe alipokuwa gerezani kwa ughaidi feki, huyu huyu alikuwa akisema "wenzake na Mbowe" tayari walisha hukumiwa jela kwa kosa lile lile. Kelele zilipozidi na kesi ya mchongo ilivyokuwa ikiunguruma na kumtia aibu yeye na wenzake mbele ya wananchi na mataifa ya nje; haraka akageuka na bila aibu kamtoa Mbowe (gaidi) jela; hata bila ya maelezo yoyote
Lakini hapo hapo katoa masharti, Mbowe na wenzake "watumie lugha za staha, na kuanza kumlaghai Mbowe na mazungumzo ya "Maridhiano", huku akijuwa hizo ni njama tu za kumlainisha Mbowe...

Bado unataka mifano zaidi? "4R" maana yake ni kitu gani. Ulisha wahi kusikia akifafanua kwa weledi kwa wananchi nia yake hasa ilikuwa ni kitu gani na hizo "4R"? Pengine hiyo ndiyo iliyo kuzoa hata wewe uanze kusema kuwa alikuwa nao "umaarufu"!
 
Unajua hata ungekuwa na njaa kiasi gani, yako mambo mabaya ambayo mfadhili wako akifanya unajikuta Aibu inakupata tu, kuna ubinadamu ambao hata Chawa wanao, kwahiyo hata wewe kama unawalipa lakini ukiboronga wanarudi nyuma na kuona Aibu.
Kuna kati ya hao "chawa" unao waongelea, ambao ndio watekelezaji wa mauaji; ambao baadhi yao tunao humu, kama 'Tlaatlaah' (sina shaka na nisemayo juu ya huyu); hawa hakuna jambo lolote linalo wastua. Hawana ule ubinaadam wa kawaida tena.
 
Naamini ingekuwa ni Mzee wako ndio kauliwa dakika hii ungekuwa unashtumu mpaka sisimizi. Ila kwa vile hakuhusu basi unapayuka tu kama uharo wa kiporo kilicho chacha.

Hili jambo ni kubwa kuliko siasa, ni swala la uhai wa watu. Japo unajihisi upo salama ila hakuna alie salama.
hakika kaka uhai wa mtu ni muhimu kuliko chochote
 
Uchunguzi tulioufanya kwa macho na Masikio yetu ni kwamba, hata wale Chawa wanaoishi kwa kumsifu tu, tangu mauaji yale ya kishamba, Wameufyata, i kwkule mitandoni wanakokesha kumtukuza hawapo tena! ( Hata nyinyi mnawajua )

Unajua hata ungekuwa na njaa kiasi gani, yako mambo mabaya ambayo mfadhili wako akifanya unajikuta Aibu inakupata tu, kuna ubinadamu ambao hata Chawa wanao, kwahiyo hata wewe kama unawalipa lakini ukiboronga wanarudi nyuma na kuona Aibu.

Ngoja tuone mpaka uchaguzi atabaki na % ngapi.
Ni kweli imani ya wananchi kwa Rais imeshuka sana maana hawaoni kama anakerwa na haya matukio sababu hakuna any official statement aliyotoa kusemea hili zaidi ya kutweet tu kwenye mtandao. Kiukweli imeonyesha kama vile hajali au kama anafahamu ishu nzima from the beginning so anakaushia. As a chief comforter tulitarajia kuona akiwa concerned sababu hii inahusisha maisha ya watu binafsi na wengi waliotekwa ni watu wanaopinga utawala wake au wakosoaji au wapinzani wa kisiasa au wanaharakati so inaleta wasiwasi sana kuhusu uhusika wake.
 
Uporokwe ye kahusika wapi?Hii uhuni mnaweza kuwa mmefanya wenyewe kwenye hiyo saccos yenu.
Na km ni kwa chama twawala itajulikana ni muda tu
Tulia wewe na sambusa zako na burger za mlenda.

Unatupigaga fiksi humu ndani eti unashindiaga burgers.
 
Kuna kati ya hao "chawa" unao waongelea, ambao ndio watekelezaji wa mauaji; ambao baadhi yao tunao humu, kama 'Tlaatlaah' (sina shaka na nisemayo juu ya huyu); hawa hakuna jambo lolote linalo wastua. Hawana ule ubinaadam wa kawaida tena.
Bali walichosahau ni kwamba Shetani hana rafiki, zamu yao haiko mbali
 
Natamani kuona akiangukia pua mchana kweupe,how come unaua wapiga kura ilihali unataka throne? Bangladesh!
Uchunguzi tulioufanya kwa macho na Masikio yetu ni kwamba, hata wale Chawa wanaoishi kwa kumsifu tu, tangu mauaji yale ya kishamba, Wameufyata, kule mitandoni wanakokesha kumtukuza hawapo tena! ( Hata nyinyi mnawajua )

Unajua hata ungekuwa na njaa kiasi gani, yako mambo mabaya ambayo mfadhili wako akifanya unajikuta Aibu inakupata tu, kuna ubinadamu ambao hata Chawa wanao, kwahiyo hata wewe kama unawalipa lakini ukiboronga wanarudi nyuma na kuona Aibu.

Ngoja tuone mpaka uchaguzi atabaki na % ngapi.
 
Kuna chawa mmoja humu ukimpiga spana huwa anatishia kwamba ni Afisa wa Serikali toka jumapili sijamuona akianzisha uzi zaidi ya kuona reaction yake kwa Kijana wa kububujikwa machozi. We are all humans na tuna mioyo wakati mwingine hata kama ni Chawa au Kunguni nafsi itakusuta tu.
Yule ni fala tu kama mafala wengine, ashawahi kujifanya ananitishia nikamcheki, anasema eti kesho nitakuona nikasema huyu bwege hajui kama atakufa bila kuniona
 
Katika miaka ya karibuni Tanzania kumekuwa na mauwaji mengi ya kutisha.Lakini yote karibu yamefanyika kwa kificho na wahanga kukutwa wakiwa kwenye viroba.
Wauwaji inaonekana walikusudia kutoa ujumbe fulani kwa watu fulani.Kwa bahati mbaya kila walivyofanya kama kwamba ujumbe haukufika na wakajiona bado hawajaeleweka.
Kuona hivyo wakaamua ngoja sasa tufanye zaidi ili ujumbe ufike na ulete athari tuliyotaka.Vile vile inawezekana ni kundi jipya la wauwaji ambao wameona watumie fursa za malalamiko ya mauwaji yaliyotangulia ili na wao wafanye ya kwao kwa malengo yale yale maovu kwa maslahi yao.
Tukumbuke siku za karibuni kumekuwa na mipasho mingi kutoka kwa wanasiasa na hata makundi ya kidini.Ilipokuja suala la bandari na DP World tukasikia mengi na kwa bahati waliotoa mipasho sana hatimae wakapigwa chenga kwa maslahi ya taifa.
Huyu aliyechaguliwa kuuliwa kwa mara ya mwisho japo ni kutoka chama cha upinzani lakini alikuwa na sifa ambazo wauawaji walitaraji atapeleka ujumbe mzito huko walikopenda ujumbe ufike.
Kwa mtazamo huo haitoshangaza kuwa iwapo uchunguzi utafanyika kwa kina na kwa utaalamu basi wauwaji wakipatikana watawashangaza sana watanzania.Wanaweza kuwa ni wafuasi wa viongozi wa dini,wakereketwa wa vyama vya siasa hata kutoka ndani ya chama tawala chenyewe au kutoka chama kikuu cha upinzani nchini.
Hakukuwa na sababu ya kumuua na kumtupa karibu na mashamba ya wakulima ili aonekane haraka.
 
Mambo yatakuwa yaleyale tu..

Usishangae kesi wakapewa viongozi wakubwa wa upinzani ili kuzima fukuto lao kuelekea uchaguzi mwakani.
 
Kwa mtazamo huo haitoshangaza kuwa iwapo uchunguzi utafanyika kwa kina na kwa utaalamu basi wauwaji wakipatikana watawashangaza sana watanzania. Wanaweza kuwa ni wafuasi wa viongozi wa dini,wakereketwa wa vyama vya siasa hata kutoka ndani ya chama tawala chenyewe au kutoka chama kikuu cha upinzani nchini.
Hakukuwa na sababu ya kumuua na kumtupa karibu na mashamba ya wakulima ili aonekane haraka.
Umeharibu uzuri wa uzi mwanzo ulianza vizuri
 
Umeharibu uzuri wa uzi mwanzo ulianza vizuri
Uko vile vile.
Muhimu ni kuwa hilo kundi ni la waovu waliojificha ndani ya makundi hayo niliyoyataja au tuseme waliofichwa humo.
 
Kwa watu wenye upeo mpana, kuna mengi ya kujiuliza kuhusu kifo cha Ally Kibao:

1) Ally Kibao, alichukuliwa ndani ya basi la abiria, mbele ya abiria wote. Na waliomchukua wala hawakujificha nyuso zao, na waliingia ndani ya basi, kama watu wenye mamlaka. Jambo la kujiuliza, hivi mnadhani kama hawa watekaji dhamira yao ilikuwa ni kumpoteza tu Ally? Kama lengo lilikuwa tu kumwua, mnadhani walishindwa nini kumteka akiwa kwenye eneo ambalo hakuna watu wengi, na hivyo wasiwepo mashuhuda wa tukio?

2) Ally Kibao alichukuliwa akiwa kwenye basi muda wa jioni, basi ambalo lingefika Tanga usiku. Mnadhani kama walitaka tu kumpoteza, kwa nini wasingemvizia hata huko Tanga ambako angefika usiku, na angeshuka kutoka kwenye basi, na kutekwa kwake kungetengeneza maswali mengi, juu ya nani kamteka?

3) Kwa kuzingatia majibu ya swali la 1 na la 2, ni dhahiri, watu waliomteka walidhamiria tendo lile lifanyike mbele ya watu wengi, ili hao watu walioshuhudia walisimlie tukio lile kwa watu wengi, na habari ziwafikie watu wengi. Je, nia hii ya kutaka taarifa ile iwafikie watu wengi ililenga nini?

4) Baada ya kumwua, maiti yake ilienda kutupwa Ununio, eneo la walima mbogamboga. Hivi mnadhani kuwa wauaji walishindwa kuutupa mwili wa Ally kwenye eneo ambalo usingeonekana kiurahisi? Ni dhahiri, waliutupa eneo hilo ili mwili ule uonekane.

Ni dhahiri watekaji wa Ally waliamua kumteka mbele ya watu wengi ili watu wajue kuwa wao wana uwezo wa kumchukua mtu yeyote wakati wowote akiwa kwenye eneo lolote, na hakuna anayeweza kulizuia hilo, wakiamua. Pili baada ya kumwua, waliurejesha mwili wake kwenye eneo la watu ili watu wajue kuwa wao wana uwezo wa kukuchukua muda wowote, wanaweza kukua hata mbele ya watu, na watu wakajua kuwa umeuawa, lakini hakuna anayeweza kuzuia au kufanya kitu kingine chochote.

DHAMIRA YA TUKIO:
Marehemu Ally Kibao, anatajwa kuwa alikuwa mkufunzi wa CHADEMA, hasa vijana, katika mbinu za kufanya siasa zinazolenga ushindi wakati wa uchaguzi, na namna ya kupambana na mbinu zote chafu za CCM. Vijana walimtegemea sana kwa kuzingatia kuwa aliwahi kuwa senior officer wa jeshi, na aliwahi kuwa katibu mwenezi wa CCM mkoa. Vijana walimwona Ally ni mlinzi na mwalimu wao. Kuuelewa ukweli huu, kunatupatia mwanga wa kwa nini watekaji waliamua kumteka mbele ya watu wengi, kisha kumwua na kuirejesha maiti yake. Walitaka wale vijana waliokuwa wakimtegemea wajue kuwa wanayemtegemea si chochote na si lolote mbele yao watekaji, wao wakiamua wanaweza kumfanya chochote, mtu yeyote, wakati wowote, na katika mazingira yoyote, hata uwe katikati ya kundi la watu. Baada ya kumwua walitaka hawa vijana wajue kuwa mkufunzi na mtu wao waliyemtegemea, wao wamemwua, hayupo tena, halafu hawa vijana wajiulize, kama mkufunzi wetu, na mtu tuliyemtegemea anaweza kufanyiwa hivi, je, sisi???

MAUAJI YA ALLY KIBAO NI TERRORISM, iliyolenga kuwatisha wote waliomwona Ally kuwa ni kiongozi na kinga yao.
 
Wasiojulikana Si lolote mbele ya nguvu ya umma.

Tukio la Mwanza la wananchi kugomea askari wasio na sare kumkamata mtu ni tone tu la yajayo.

Wananchi tumeipa mamlaka Serikali itulinde,

Hii haimaanishi kuwa sisi hatuwezi kujilinda la hasha,

Tumewaajiri Serikali, Bunge, mahakama,polisi watulinde, tunawalipa mshahara Ili tufanye shughuli zingine Ili kupata Kodi ya kuendesha Nchi.

Wananchi tuna HAKI ya kuishi, na hayupo wa kututisha, hayupo.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Amin
 
Lengo lao ilikuwa ni kuwatisha watu. Na tukitishika wataona wamefanikiwa. Lazima wananchi sasa kuja juu zaidi, ili wajue kuwa mipango yao ya kishetani imeshindwa.
 
Back
Top Bottom