TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Ujumbe wa Mdude kwa marafiki, ndugu na watanzania
1726739962554.jpg

Screenshot 2024-09-19 144521.png
 
Chizi huyo....

Hana adabu huyo.....

Hawa Makhuluku tabu sijui wanajionaje ?!! 😲😲

Wanajionaje hawa ?!!
 
Anaandika Boniyai kutoka Account yake ya X


======


Ali Mohamed Kibao Ameuawa

Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu umekutwa hospitali ya Mkoa wa Kinondoni,Mwananyamala katika chumba cha kuhifadhia maiti mwili wake ukiwa UMEHARIBIWA VIBAYA SANA.

Mwili wa ALI MOHAMED KIBAO ulikutwa umetupwa jana alfajiri maeneo ya UNUNIO (jirani na viwanja vya NSSF) ukiwa na majereha makubwa sehemu za usoni kiasi ndugu zake walipata tabu kuutambua kirahisi.

ALI MOHAMED KIBAO alikamatwa na watu wanao dhaniwa kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi eneo la TEGETA, mbele ya Jengo la KIBO COMPLEX baada ya gari mbili za Jeshi za Polisi za Landcruiser hardtop nyeupe kuzuia (block) basi la TASHIRIF lenye namba T 343 EES alilokuwa amepanda ALI MOHAMED KIBAO kutoka Dar es saalam kuelekea nyumbani kwao Mkoani Tanga.

Kwa bahati nzuri wakati wote wa tukio likitendeka ndani ya gari palikuwa na askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani (Traffic) ambaye alikuwa kiti cha mbele kama abiria na alishuhudia tukio lote, anatambulika kama MACHIWA anayepatikana kwa namba 0652484802.

Namba ya simu aliyokuwa anatumia ALI MOHAMEDKIBAO ni +255 624 724 247 mpaka wakati anatekwa na kwenda kuuwawa,pia ndiyo namba ambayo mara kadhaa waliomteka walikuwa wakimpigia kuhakiki kama ni yeye.

Kwa mujibu wa wenyeji wa UNUNIO ambao ni walima mchicha, wanasema Jana asubuhi walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi baada ya Kuona mwili wa Mtu mzima, mweupe mwenye asili ya Kiarabu ambaye baadae Jana jioni ndugu waliutambua kuwa ni mwili ALI MOHAMED KIBAO ukiwa na majeraha.

Kabla ya umauti wake ALI MOHAMED KIBAO aliwahi kuwa afisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akastaafu na kujiunga na CCM,baadae akachaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Tanga wakati wa Rais Kikwete,na baadae alijiunga CHADEMA.

Baada ya mauaji haya ya Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA na Msaidizi wa Katibu Mkuu kuwawa idadi ya Viongozi wa CHADEMA wakiotekwa inaongezeka
1. Dioniz Kipanya 2. Kombo Bwana Twaha 3. Godwin Mlay 4. Deusdedith Soka 5. Frank Mbise.
Boniface Jacob
Ex-Mayor
0712 239 595


Soma Pia:
Ni kweli
P
 
Kila kona iwe Makazini, vijiwe vya kahawa hata kwenye Magari ya abiria kila Mtanganyika analaani kuuwawa kwa huyu Mzee.

Ndio Maana watu wameungana iwe viongozi wa dini zote, wapagani na hata wahuni mitaani. Wanalaani huyu mzee kuuwawa

Hawana furaha na wanaona nchi yao ya Tanganyika imekuwa kama Mexico ambapo mtu kuuwawa kama nzi ni kawaida.

Je, ni nani anawanyima raha Watanganyika hawa? Waliozoea kuishi kwa amani na upendo hata Kama wanatofauti za kisias?
Walaaniwe na walaanike hadi kizazi cha nne wale wote walioshiriki,walioagiza,waliotekeleza mpango huo haramu.
 
Imagine umeshatekwa na wale watu na upo kwenye 18 zao kwenye nyumba moja iliyozungushiwa ukuta mkubwa na uko huko ndani wewe na wao bila mtetezi.
Mzee ali mohamed kibao navaa viatu vyake yani kama namuona najaribu kuwaza alivyokuwa ametiwa pingu huyoooo ndani ya gari mpaka kwenye nyuma ya siri.
Huko anaketishwa na watesi wake labda chini ya sakafu mikono ikiwa imetiwa pingu hawezi kujitetea mara interogation inaanza na maswali ya vitisho huku akijisemea moyoni wataniuwa au wataniacha. Mara anashangaa kwa macho ya kikatili anatobolewa jicho la kwanza kisha la pili nuru inatoweka haoni tena chochote duniani anaanza kulia kwa uchungu jaribu kuwaza sauti ya mzee kama yule akilia kama mtoto mdogo. Mara anashtukia katikati ya mmaumivu hayo anakula nondo ya kichwa na kupoteza fahamu mileleee........
 
Halafu hawa mbwa ndio wanataka eti tuwaheshimu. MUNGU atupe Tu uvumilivu, halafu kuna MTU anasema kila MTU atakufa Tu......Tumuogope Mungu
 
UNAFUKUA KABURI

Mama hapendi hiyo tabia
Hisia na dhahania hazipigwi rungu hawawezi kuzuia watu kukumbuka mateso ya mwisho ya wapendwa wao!
Unadhani watoto wake au mnyika ambae alikuwa kwenye ofisi yake hawana trauma?
 
Mods msifute huu uzi maana tunajaribu kuvaa viatu vya marehemu mzee wetu sio kosa.
 
Halafu hawa mbwa ndio wanataka eti tuwaheshimu. MUNGU atupe Tu uvumilivu, halafu kuna MTU anasema kila MTU atakufa Tu......Tumuogope Mungu
Utawafanya nini? Maana kama ungekuwa na uwezo wa kuwafanya chochote ungeliishawafanya. Zaidi unatamba tu nyuma ya keyboard! Ahahahahaha!!!
 
Back
Top Bottom