MSAGA SUMU
JF-Expert Member
- May 25, 2015
- 6,661
- 21,656
Ujumbe wa Mdude kwa marafiki, ndugu na watanzania
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni kweliAnaandika Boniyai kutoka Account yake ya X
======
Ali Mohamed Kibao Ameuawa
Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu umekutwa hospitali ya Mkoa wa Kinondoni,Mwananyamala katika chumba cha kuhifadhia maiti mwili wake ukiwa UMEHARIBIWA VIBAYA SANA.
Mwili wa ALI MOHAMED KIBAO ulikutwa umetupwa jana alfajiri maeneo ya UNUNIO (jirani na viwanja vya NSSF) ukiwa na majereha makubwa sehemu za usoni kiasi ndugu zake walipata tabu kuutambua kirahisi.
ALI MOHAMED KIBAO alikamatwa na watu wanao dhaniwa kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi eneo la TEGETA, mbele ya Jengo la KIBO COMPLEX baada ya gari mbili za Jeshi za Polisi za Landcruiser hardtop nyeupe kuzuia (block) basi la TASHIRIF lenye namba T 343 EES alilokuwa amepanda ALI MOHAMED KIBAO kutoka Dar es saalam kuelekea nyumbani kwao Mkoani Tanga.
Kwa bahati nzuri wakati wote wa tukio likitendeka ndani ya gari palikuwa na askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani (Traffic) ambaye alikuwa kiti cha mbele kama abiria na alishuhudia tukio lote, anatambulika kama MACHIWA anayepatikana kwa namba 0652484802.
Namba ya simu aliyokuwa anatumia ALI MOHAMEDKIBAO ni +255 624 724 247 mpaka wakati anatekwa na kwenda kuuwawa,pia ndiyo namba ambayo mara kadhaa waliomteka walikuwa wakimpigia kuhakiki kama ni yeye.
Kwa mujibu wa wenyeji wa UNUNIO ambao ni walima mchicha, wanasema Jana asubuhi walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi baada ya Kuona mwili wa Mtu mzima, mweupe mwenye asili ya Kiarabu ambaye baadae Jana jioni ndugu waliutambua kuwa ni mwili ALI MOHAMED KIBAO ukiwa na majeraha.
Kabla ya umauti wake ALI MOHAMED KIBAO aliwahi kuwa afisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akastaafu na kujiunga na CCM,baadae akachaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Tanga wakati wa Rais Kikwete,na baadae alijiunga CHADEMA.
Baada ya mauaji haya ya Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA na Msaidizi wa Katibu Mkuu kuwawa idadi ya Viongozi wa CHADEMA wakiotekwa inaongezeka
1. Dioniz Kipanya 2. Kombo Bwana Twaha 3. Godwin Mlay 4. Deusdedith Soka 5. Frank Mbise.
Boniface Jacob
Ex-Mayor
0712 239 595
Soma Pia:
- CHADEMA: Mzee Ally Kibao ametekwa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama akiwa kwenye basi. Usalama wa Taifa waeleze alipo
- Polisi: Tunachunguza kubaini chanzo na watu waliohusika kumchukua Ally Kibao
- LIVE - Tanga: Yanayojiri Kwenye mazishi ya Ali Kibao Kiongozi wa Chadema
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
Walaaniwe na walaanike hadi kizazi cha nne wale wote walioshiriki,walioagiza,waliotekeleza mpango huo haramu.Kila kona iwe Makazini, vijiwe vya kahawa hata kwenye Magari ya abiria kila Mtanganyika analaani kuuwawa kwa huyu Mzee.
Ndio Maana watu wameungana iwe viongozi wa dini zote, wapagani na hata wahuni mitaani. Wanalaani huyu mzee kuuwawa
Hawana furaha na wanaona nchi yao ya Tanganyika imekuwa kama Mexico ambapo mtu kuuwawa kama nzi ni kawaida.
Je, ni nani anawanyima raha Watanganyika hawa? Waliozoea kuishi kwa amani na upendo hata Kama wanatofauti za kisias?
Hisia na dhahania hazipigwi rungu hawawezi kuzuia watu kukumbuka mateso ya mwisho ya wapendwa wao!UNAFUKUA KABURI
Mama hapendi hiyo tabia
Mjue sana Mungu ili uwe na amani na hapo ndipo mema yatakapokujilia.Halafu hawa mbwa ndio wanataka eti tuwaheshimu. MUNGU atupe Tu uvumilivu, halafu kuna MTU anasema kila MTU atakufa Tu......Tumuogope Mungu
Utawafanya nini? Maana kama ungekuwa na uwezo wa kuwafanya chochote ungeliishawafanya. Zaidi unatamba tu nyuma ya keyboard! Ahahahahaha!!!Halafu hawa mbwa ndio wanataka eti tuwaheshimu. MUNGU atupe Tu uvumilivu, halafu kuna MTU anasema kila MTU atakufa Tu......Tumuogope Mungu