Inaelezwa kuwa majira ya saa 10:00 (usiku) marehemu akiwa maeneo ya bar ya kitambaa cheupe alivamiwa na mtu/watu wasiojulikana ambao walimchoma na silaha yenye ncha kali kati ya shingo na bega la kushoto na kupelekea kifo chake. Kiini cha tukio kinachunguzwa.
Pia soma: Zanzibar: Askari wa JKU auawa, mkuu wa kituo cha polisi ashambuliwa
Mbinu ni kumvizia marehemu akiwa uchochoroni na kumchoma na silaha yenye ncha kali. Marehemu amekutwa na mali zake zote na ana jeraha moja lililotokana na silaha yenye ncha kali lililopo kati ya shingo na bega la kushoto.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya kilwa road kwa uchunguzi zaidi. Wafanyakazi wa bar watano wamekamatwa kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.
Source: Fortunatus Buyobe Twitter account
NB: Kifo ni kifo tu ndugu zangu Wana JF, isije hiki ndio kiwe maarufu, pia tuwapongeze polisi wanafanya kazi nzuri sana, uharifu umepungua.
Matukio mengine yanayohusu watu wasiyojulikana soma: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana