Dar: Askari polisi auawa baa ya Kitambaa Cheupe, njia panda ya Nzasa, usiku wa kuamkia 6.10.2024

Hapo Kitambaa bei ni elekezi au wanatupiga kama Wavuvi?
Katika nchi maskin kama tanzania mtu yupo tayari akanywe safari lager moja kwa elfu 10 badala ya bei halisi ya 1,800 ili tu nae aonekane tajiri na apige picha na madem
 
Wasomi kulinda bank mlangoni na kufungua milango ya mabosi.
We na usomi wako unafanya nini ndugu.?? Acha kebehi zisizo na msingi.. kumfungulia boss mlango ni shida... au usomi kwako ni uboss.. ndiyo ninyi mnaofanya vijana washindwe kujiajiri au kuchagua kaz kisa amesoma..
 
Si umesoma hapo, wamekamatwa watu watano kwa uchunguzi zaidi,

Kule kwa Mzee Kibao kimya Hadi sasa, ngoja tuendelee kusubiri pengine waliomuuwa watapatikana Inshallah,
Kwa kibao ilikuwa barabarani ulishauri wawakamate nani pale?

😀
 
Tarehe 06.10.2024 saa 10:00 (usiku) maeneo ya bar inayojulikana Kitambaa Cheupe, njia panda Nzasa, askari namba J.3297 PC. Barnaba Andrea Mhonya (30 yrs) mkazi wa Chamazi na askari wa Jeshi la Polisi Tanzania aliuwawa na mtu/watu wasiojulikana kwa kumjeruhi na silaha yenye ncha kali kati ya shingo na bega la kushoto.

Inaelezwa kuwa majira ya saa 10:00 (usiku) marehemu akiwa maeneo ya bar ya kitambaa cheupe alivamiwa na mtu/watu wasiojulikana ambao walimchoma na silaha yenye ncha kali kati ya shingo na bega la kushoto na kupelekea kifo chake. Kiini cha tukio kinachunguzwa.

Pia soma: Zanzibar: Askari wa JKU auawa, mkuu wa kituo cha polisi ashambuliwa

Mbinu ni kumvizia marehemu akiwa uchochoroni na kumchoma na silaha yenye ncha kali. Marehemu amekutwa na mali zake zote na ana jeraha moja lililotokana na silaha yenye ncha kali lililopo kati ya shingo na bega la kushoto.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya kilwa road kwa uchunguzi zaidi. Wafanyakazi wa bar watano wamekamatwa kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.

Source: Fortunatus Buyobe Twitter account

NB: Kifo ni kifo tu ndugu zangu Wana JF, isije hiki ndio kiwe maarufu, pia tuwapongeze polisi wanafanya kazi nzuri sana, uharifu umepungua.

Matukio mengine yanayohusu watu wasiyojulikana soma: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
Mmmhh!

What are the motives behind?
 
Habari hii inaacha mashaka makubwa sana. It looks like a special mission.
 
Back
Top Bottom