Dar: Askari polisi auawa baa ya Kitambaa Cheupe, njia panda ya Nzasa, usiku wa kuamkia 6.10.2024

Dar: Askari polisi auawa baa ya Kitambaa Cheupe, njia panda ya Nzasa, usiku wa kuamkia 6.10.2024

Huyu ndiye Askari J.3297 PC.BARNABA ANDREA MHONYA View attachment 3117301mkazi wa Chamazi aliyeuwawa kwa shabulio la kisu maeneo ya bar ya Kitaa Cheupe Mbagala.

Advance kasoma Umbwe boys na alifaulu kwa Div 1,

Chuo Kikuu kasoma Ardhi University Bachelor of Science in Accounting and Finance hadi mauti yanamkuta, alikua anasoma Masters.

Mwaka 2022 akajiunga na jeshi la Polisi na baada ya mafunzo alikuwa akihidumu kama mhasibu wa polisi kanda maalumu ya kipolisi Temeke.

Marehemu hakuwa ameoa wala kupata mtoto enzi za uhai wake.

Kwa kuwa washambuliaji/mshambuliaji hakuchukua chochote kutoka kwake, inaleta hisia kuwa tukio hili lilikuwa ni la kulipiza kisasi.

Natuma salamu za pole kwa uongozi wa jeshi la polisi kwa kumpoteza askari msomi.
Credit: Fortunatus Buyobe
Bwana mdogo sana aise watafutwe waliyomfanyia unyama huo
Ila kwa harakaharaka inaweza kuwa kisasi

Ova
 
Tarehe 06.10.2024 saa 10:00 (usiku) maeneo ya bar inayojulikana Kitambaa Cheupe, njia panda Nzasa, askari namba J.3297 PC. Barnaba Andrea Mhonya (30 yrs) mkazi wa Chamazi na askari wa Jeshi la Polisi Tanzania aliuwawa na mtu/watu wasiojulikana kwa kumjeruhi na silaha yenye ncha kali kati ya shingo na bega la kushoto.

Inaelezwa kuwa majira ya saa 10:00 (usiku) marehemu akiwa maeneo ya bar ya kitambaa cheupe alivamiwa na mtu/watu wasiojulikana ambao walimchoma na silaha yenye ncha kali kati ya shingo na bega la kushoto na kupelekea kifo chake. Kiini cha tukio kinachunguzwa.

Pia soma: Zanzibar: Askari wa JKU auawa, mkuu wa kituo cha polisi ashambuliwa

Mbinu ni kumvizia marehemu akiwa uchochoroni na kumchoma na silaha yenye ncha kali. Marehemu amekutwa na mali zake zote na ana jeraha moja lililotokana na silaha yenye ncha kali lililopo kati ya shingo na bega la kushoto.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya kilwa road kwa uchunguzi zaidi. Wafanyakazi wa bar watano wamekamatwa kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.

Source: Fortunatus Buyobe Twitter account

NB: Kifo ni kifo tu ndugu zangu Wana JF, isije hiki ndio kiwe maarufu, pia tuwapongeze polisi wanafanya kazi nzuri sana, uharifu umepungua.

Matukio mengine yanayohusu watu wasiyojulikana soma: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
huyu polisi handsome boy,,,inaelekea ni mambo ya mapenzi!!
 
sasa muhasibu akawe na sifuri kaka?
Mbona unaukosa ule uhalisia wa JF IS THE HOME OF GREAT THINKERS?

Kwani mhasibu ni nani ndugu?

Si tulisha kubaliana kuwa kama ilivyo katika viungo vya mwili, hata kwenye hizi taaluma hakuna iliyo na umuhimu zaidi mno katika jamii kuliko nyingine?

Au wewe ndiyo wale wahasibu wenye kujimwambafai na indispensability?

Angalizo:

Graves are full of indispensable people.
 
Ulikomferm kuwa chanzo ni Malaya?
Bar/club sehemu za starehe zozote unazozijua na ugomvi wa Malaya ni chai na maandazi chai na chapati yaan vinaenda hapa na hapa kwa hio kwa kadrio la chini kabisa naweza niseme ndio inaweza kua ni sababu ya yote, pole kwa marehemu mwendo ameumaliza
 
Tarehe 06.10.2024 saa 10:00 (usiku) maeneo ya bar inayojulikana Kitambaa Cheupe, njia panda Nzasa, askari namba J.3297 PC. Barnaba Andrea Mhonya (30 yrs) mkazi wa Chamazi na askari wa Jeshi la Polisi Tanzania aliuwawa na mtu/watu wasiojulikana kwa kumjeruhi na silaha yenye ncha kali kati ya shingo na bega la kushoto.

Inaelezwa kuwa majira ya saa 10:00 (usiku) marehemu akiwa maeneo ya bar ya kitambaa cheupe alivamiwa na mtu/watu wasiojulikana ambao walimchoma na silaha yenye ncha kali kati ya shingo na bega la kushoto na kupelekea kifo chake. Kiini cha tukio kinachunguzwa.

Pia soma: Zanzibar: Askari wa JKU auawa, mkuu wa kituo cha polisi ashambuliwa

Mbinu ni kumvizia marehemu akiwa uchochoroni na kumchoma na silaha yenye ncha kali. Marehemu amekutwa na mali zake zote na ana jeraha moja lililotokana na silaha yenye ncha kali lililopo kati ya shingo na bega la kushoto.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya kilwa road kwa uchunguzi zaidi. Wafanyakazi wa bar watano wamekamatwa kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.

Source: Fortunatus Buyobe Twitter account

NB: Kifo ni kifo tu ndugu zangu Wana JF, isije hiki ndio kiwe maarufu, pia tuwapongeze polisi wanafanya kazi nzuri sana, uharifu umepungua.

Matukio mengine yanayohusu watu wasiyojulikana soma: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
Itakuwa wanajiua kama Mkuu wa mkoa alivyosema kuwa wananchi wanajiteka
 
Jinga sana wewe
Teheeee nn kidoti , wazee walikuwa wanatoa sana simulizi za ubaya wa kutotembea usiku uku tukiwa tunachoma mahindi kwenye nyumba za msonge mwisho wanamaliza na huo msemo . Hivyo uwa tunautafakali sana tunawahi kuludi home mapema
 
Back
Top Bottom