Mkuu engine za kwenye bus nyingi yazo ni 90 series, mpaka sasa wanatoa hizi 95 mpya kama ambazo wamezitangaza kwenye huu uzi, kinachofanyika ni kile kile ingawa wengine wanasemaga mambo ya kubana pump ila kuchanganya haraka ni kwamba ile engine inaweza kubeba tani 15 mpaka 20 hivi, ila likipakia abiria na mizigo yao inakua na kama tani 8 au pungufu, so gari inakua nyepesi sana hata gear hazichukui muda kuchanganya!
Halafu kwenye roli mara nyingi tunafunga fuse ya speed, angalau kwenye 90kph, ikifika hapo inakata, ila kwenye bus wanaitoa hii so dereva anaendesha mpaka anagotesha mshale mwisho.
Halafu bus nyingi zinakua na gear 8au 10 wakati roli nyingi kubwa ukitoa hizo 90 series zinakua na gear 10,12, au 16 kabisa kwahiyo gari yenye gear nyingi hivyo mpaka ichanganye ni tofauti na huyu wa gear chache, hata ukianza kuzivua hizo gear kwenye mlima ni tofauti na dereva wa bus.
Kingine ni udereva tu Mkuu ndo unaleta huo udambwidambwi, mimi nina madereva ambao wanatoka kwenye maroli na kwenda kwenye mabus na wengine wanafanya viceversa, mfano nina madereva nilikua nao kwenye maroli ila saivi wapo Newforce, Hood, Imo na NBS,.. So hapo ni udereva tu.
Dereva wa roli hawezi kuendesha kama bus maana litamuua, kusimama na roli lilikua 100kph na mzigo wa tani 30 mgongoni ni ngumu ukilinganisha na bus la Abiria 55..