Dar: Dunstan Daudi Mutajura adaiwa kutekwa eneo la Buza

Ma don wa kihaya sasa ni wakati wenu wa kupaza sauti huu utekaji uishe mkijikusanya akina Mzee Mkwama. Bwesha, Mukandara, Ishengoma, Rwabizi, Rugarabamu, Kato, Dr Rwejuna. OMUTWALE WOTE pigeni hodi kwa mkuu wa drama mumueleze mambo ya kutekana ni ya kishamba.
 
Jiji la das-es laam ni la ajabu sana.. Mtu anatekwa mchana kweupe wanamuangalia tu., 🤒🤒🤒
Suala la Kudhibiti utekaji na Watekaji siyo kazi rahisi hata kidogo kama unavyofikiri, Kumbuka, hao Watekaji ni Watu Wabobevu na Wataalamu wakubwa kwenye kazi hizo za Kuteka Watu, wamesomea darasani na kupata Mafunzo ya Umahiri kuhusiana na shughuli hizo za Utekaji ( Professional Abductors/Kidnappers). Zinahitajika nguvu kubwa sana na za ziada pamoja na Wananchi kuwa tayari kujitolea muhanga ili kupambana na hao Watekaji sambamba na kuvikomesha kabisa vitendo hivyo vya utekaji na Watekaji wenyewe.
Narudia tena kusema, kudhibiti Watekaji siyo kazi rahisi hata kidogo.
 
Jiji la das-es laam ni la ajabu sana.. Mtu anatekwa mchana kweupe wanamuangalia tu., 🤒🤒🤒
Wewe utafanya nini? Kwanza kitendo cha haraka, mnakuwa na mshtuko mnajiuliza hawa vipi? Mara kashaingizwa kwenye gari. Halafu wanakuwa na silaha utawafanya nini? Utapigwa risasi kwa kuingilia visivyokuhusu.
 
Kutekana kwa ransom au sababu zingine zozote ni aina ya ujambazi unaosambaa kwenye miji mikubwa.Kwa Dar es salaam bado linaonekana jambo geni.
Nairobi imekuwa jambo linalosumbua vyombo vya usalama na mpaka mwishoni wa mwaka 2024 watu 85 wametekwa na baadhi yao kuuwawa.Imekuwa jambo la kawaida wafanyabiashara na watu watu mashuhuri kuwa na, walinzi binafsi.
Johanessburg utekaji na car jacking ni maisha ya kila siku kwa wakazi wa Jiji hilo.
Polisi lazima waanze kufanya kazi ya kuzuia hii hali isiendelee kabla ya kuzoeleka na kuwa sehemu ya maisha.
 
Kafanya nini?

Mbona siyo maarufu?
 
Kabisa hili jambo lisipozuiwa litaonekana jambo la kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…