Naona Makalla anawaruhusu polisi kuendelea kuwapiga watuhumiwa wakiwa mikononi mwao, tujiandae kupokea taarifa zaidi za mahabusu kufia vituo vya polisi.
Hata hiyo sababu aliyoitoa Makalla, kwamba baadhi ya hao panyarodi walishafungwa miezi sita hadi mwaka mmoja, haina maana wazazi wao ndio wakawatafute vijana wao mahospitalini, hii ni kauli ya mihemko.
Kawaida, kule mahakamani, baada ya mtuhumiwa kukutwa na hatia, hakimu/jaji hutoa nafasi kwa mawakili wa pande zote mbili, waseme kwanini mtuhumiwa afungwe miaka mingi, au miaka michache.
Sasa hiyo ni nafasi nzuri kwa mawakili wa serikali kuiambia mahakama, mtuhumiwa anastahili adhabu kubwa zaidi kwasababu amerudia kosa, kwani adhabu aliyopewa mwanzo haikutosha kumbadili tabia.
Inashangaza, hawa polisi wetu waliozoea kubambikia kesi watuhumiwa, kuwaruhusu wapige watuhumiwa wakiwa mikononi mwao ni kosa kubwa sana, litakuja kuwaumiza panya rodi na wale wasio panya rodi.
Jamaa wanatatua tatizo moja kwa kutengeneza tatizo lingine, huu ni mfano halisi wa mamlaka iliyochoka akili inayostahili kupumzika kuwaongoza watanzania.