Umeongea kitu sahihi kabisa.
Kutatua hili tatizo ni lazima kuliangalia kuanzia kwenye mzizi wake(Malezi ya watoto). Jamii tumejisahau sana katika hili.
Natoa mfano: Nili kaa mwanza mjini (Ilemela) kwa muda wa wiki 2 hivi hapo mwezi wa tatu mwaka huu, nilishangaa kukuta idadi kubwa ya watoto umri kati ya miaka 10 - 15 wakizagaa zagaa mitaani kutafta msaada wa chakula, hii ikimanisha hakuna mtu wa kuwasiamia au hawataki kusimamiwa na wametoroka nyumbani. Na mara nyingi watu wamekua wakiwafukuza wasionekane kwenye maeneo yao.
Ukiwatazama zaidi ubagundua wengi wao wameacha shule mapema kabisa au hawajawai kwenda shule kabisa.Kuna watu wanaleta siasa kua hao vijana wamekosa ajira binafsi sikubaliani nao na hata ksma wapo walio soma wakosa ajira ndo waamue kujiunga huko basi hao wamekosa sifa kabisa kuajiriwa popote. Issue ni kwamba vijana hawa washakata tamaa hakuna future wanayoiona mbele kwao kuishi na kufa yote sawa tu ndo mana wako hivo.
Sasa jiulize mtoto kama hyu akikua kufikia miaka 18 akakutana na ushawishi wa genge lolote la kiuhalifu, sidhani kama atakua na chembe ya huruma kwa jamii ambayo haikuonyesha kumjali kipindi chote alipo kua anakua.
Na kiukweli hao panya road wakipata support ya kisiasa let's say Alshababu au Jirani yetu EA asiependa amani kwa majirani zake, akawaongezea nguvu(Silaha + Mafunzo kdg) kwa kweli miji mingi itakua haikaliki.
Nguzo ya malezi izingatiwe kwenye jamii zetu. Iwe ni kosa kabisa kukuta mtoto chini ya miaka 15 anazagaa mtaani, halmashauri zitenge fungu kabisa la kuchukua hawa vijana na kuwawekea mazingira rafiki kwao. Nje ya hayo yajayo yanafurahisha.
Sent from my CPH1819 using
JamiiForums mobile app