Dar es Salaam: Askari 300 waongezwa kudhibiti panya road

Anyway, Mungu na Akubariki.
Naona unakimbia sababu umeshindwa kujibu hoja iliyotokana na swali lako mwenyewe.

Nimekuuliza mwanzo:
Wewe mpaka sasa hivi kwanini umeshindwa kwenda kuwashitaki viongozi husika juu ya huyo binti aliyeuliwa na panyaroad. Sababu ni ushahidi tosha juu ya kushindwa kutimiza wajibu wao wa kulinda raia na mali zao?
Au huyo binti sio mtanzania?

Jibu hilo swali.
 
Hakika umenena ukweli. Wa kuanza nao ni hawa wezi wanaojiita viongozi, wanaotoza toza hovyo fedha ili wastarehe.
 
Endelea kujidanganya Tu hawa panya road ni shaba
Sijidanyanyi ila wewe ndiyo unajidanganya. Wakisema wauawe, nina uhakika asilimia kubwa ya watakaouawa siyo panya road. Unajifanya hujui polisi wetu? Ni yale yale ya kujidanganya kuwa ili tumalize ufisadi basi inabidi tupishe hukumu ya kifo wa mafisadi bila kujiuliza hata sasa hivi jela kuna mafisadi wangapi.
 
Panya road wengi wao ni WATOTO WA MAPOLISI, wanaishi nao huko huko kwenye makambi yao. Serikali hii ya CCM ni ya ajabu sana.
 
Eeee Mungu tusaidie kwa kweli .Watoto tunaowazaa ni majanga duu mpaka binadamu anaitwa Panya Road na kuweza kuwauwa wengine.Huyu binti kimeniuma sana kwa kweli .
 
Kuna ustawi wa Jamii hawa vijana wapewe maarifa ya kujiajiri kama uashi mdogomdogo plumbing carwashing sio kuwalaumu tu.
 
Nasikitika sana jeshi la polisi linavyo wapa umaarufu hawa.Et askari mia3 wameongezwa,je ingekuwa alqaed ?
 
Operation kula panya. Chimumunye chichiteme. Kamanda Nakapanya

 
Wakulaumiwa ni Samia na wasaidizi wake wanaokula mshahara wetu bure, tatizo la panya lodi lilikuwa limeisha kipindi cha Magufuli, Maana Magufuli aliliruhusu kila mmoja hafanye Kazi ilimradi afuate Sheria, vijana wengi wakadunduliza mitaji wakafungua vibanda na kufanya shughuri zao bila bughuza wakawa wanajingizia kipato, baada ya Magufuli kufa Samia kafanikiwa kushika madaraka kawafukuza wote,na kuwaharibia mitaji yao,hivi mnafikili vijana wote waliokuwa barabarani wameenda wapi?hata wamwage asikari kiasi gani tatizo la panya lord haliwezi isha, vijana wananjaa, Serikali hiwape vijana ajira la sivyo hali itakuwa mbaya zaidi.
 
Kwann wameshindwa kuendelea na shule secondary au kuingia veta nk.

Lipo jambo JAMII na Serikali Kwa ujumla tunajitoa uhusika.
Wengi wao,hawajapata malezi bora
Unakuta baba mama hawana habari nao
Watoto kutwa wako kwenye masingeli,kamari tu
Watoto kama hao hata uniform za shule hawazijui

Ova
 
Armed robbery + Haki za binadamu !! Kazi Kweli Kweli !!
 
Duh !!
 
Ngoja siku wakutaitishe wakule kiboga tuone Kama utakuja hapa na hii ngonjera there is no excuse ya uhalifu,,,
 
Ngoja siku wakutaitishe wakule kiboga tuone Kama utakuja hapa na hii ngonjera there is no excuse ya uhalifu,,,
Mawazo ya kiuwaji hayo, unawapa RUHUSA askari waue raia bila uchunguzi Wala kufikishwa mahakamani.

POLISI wanatakiwa waongeze DORIA na kuwajibika ikiwa kundi lolote litadhuru RAIA.

Ninyi ndo huwa mnachoma binadamu wenzenu moto hadharani.
 
Wewe unataka wapewe mikate na siagi kwa vitendo wanavyofanya? Hao wauwawe tu. Hata wewe pia ukijifanya kimbelembele unakula chuma vilevile. Watu kama nyie mnakera sana
 
Nilishasema humu,ilala kuna kundi
Walikuwa wanajiita chaukucha
Walikuwa wanasumbua ilala hadi buguruni mpk mto kigogo huko
Iliundwa task force maalum,baraka
Zote zlitoka juu tena
Mbona waliwafyeka ilikuwacni kuua tu

Ova
Mzee wa Kino nawakumbuka Chaukucha... ilikuwa balaa. Hadi leo kuna timu ya mpira huko Msimbazi Bondeni inaitwa Chaukucha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…