Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Nimetafuta sukari maduka mengi ya nyumbani Tandika Mwembeyanga na Temeke mwisho sikufanikiwa kuipata, baadaye akaja kijana mmoja ninayefahamiana naye akaninong'oneza kwamba siwezi kupata sukari wiki hii, labda nisubiri upepo upite.
Baada ya uchunguzi wangu wa wazi nimebaini kwamba maduka karibu yote ya rejareja hayauzi tena sukari jijini Dar kutokana na mgogoro wa bei, taarifa zinaonyesha kwamba maduka ya jumla likiwemo la mfadhili wa CCM aitwaye Zakaria kilo moja ya sukari inauzwa kwa Tsh 2800 /= tena kwa masharti kwamba ni lazima ununue na vitu vingine, huku Muuzaji wa reja reja akitakiwa kuiuza kilo hiyo hiyo kwa Tsh 2600 /= kutokana na bei elekezi ya Serikali .
Wauzaji wa rejareja wameona isiwe tabu wameamua kuiachia serikali iuze yenyewe sukari kama inavyouza dawa kwenye maduka ya MSD