Dar es Salaam hakuna sukari madukani

Dar es Salaam hakuna sukari madukani

Nimetafuta sukari maduka mengi ya nyumbani Tandika Mwembeyanga na Temeke mwisho sikufanikiwa kuipata, baadaye akaja kijana mmoja ninayefahamiana naye akaninong'oneza kwamba siwezi kupata sukari wiki hii, labda nisubiri upepo upite.

Baada ya uchunguzi wangu wa wazi nimebaini kwamba maduka karibu yote ya rejareja hayauzi tena sukari jijini Dar kutokana na mgogoro wa bei, taarifa zinaonyesha kwamba maduka ya jumla likiwemo la mfadhili wa CCM aitwaye Zakaria kilo moja ya sukari inauzwa kwa Tsh 2800 /= tena kwa masharti kwamba ni lazima ununue na vitu vingine, huku Muuzaji wa reja reja akitakiwa kuiuza kilo hiyo hiyo kwa Tsh 2600 /= kutokana na bei elekezi ya Serikali .

Wauzaji wa rejareja wameona isiwe tabu wameamua kuiachia serikali iuze yenyewe sukari kama inavyouza dawa kwenye maduka ya MSD
Hata Arusha hakuna, hii ni hatua nzuri maana sukari inaleta vitambi
 
Nenda Tegeta kwa ndevu sukari iko bei sh 2600
Mwongo! Tegeta kwa ndevu jakuna sukari hata duka moja! Nimepita maduka yote hadi ya uchochoroni kuisaka na sijaipata! Nimekwenda hadi maduka ya namanga, kibo na nyuki na kunduchi kwa wapemba nimeambulia patupu! Nimerudi na ndizi mbivu tu angalau. Sukari kuadimika ndiko kupendwa kwa ccm kunazidi!
 
Suala lipo wazi huwezi kuwabana wa chini ilhali tatizo lipo juu,hakuna mfanya biashara mdogo au wa kati atakaye kubali kuuza au kununua sukari kwa bei ya hasara.

Na matokeo yake ndio haya.
 
Ngoja kwanza kuna wanafunzi walitoroka chuo kikuu chaDodoma,
 
Serikali itambue kwamba mwananchi wa kawaida anachotaka ni mkate wake wa kila siku, maji safi, amani na utulivu, malazi na elimu.
Ninyi ibeni, fanyeni ufisadi, jengeni ma hekalu, oeni wake hata kumi, somesheni watoto wenu ulaya, katibiweni India, nunueni ma V8 Sisi hatujali ila tunataka sukari hasa kipindi hiki cha mfungo.
Jamani we are not asking for too much. Sukari tu mahindi yetu tunayo
 
Poleni sana. Nilinunua ya kunitosha mpaka 7 mwishoni.
Wapumbavu bado ni wengi Tanzania Hongera mpumbavu Ila ujue sio wote wanaweza kufanya hivyo. Mfikirie na mama ntilie nae. Hana uwezo wa kununua hata kilo 2.
 
Back
Top Bottom