Dar es Salaam: House girl amshtaki bosi wake kwa kutomlipa mshahara kwa miaka Mitano

Watu wa kigoma anaweza fanya kazi kwako hata miaka 10 anasema boss nitunzue mshahara wangu asee siku akikwambia nipe mushahara wangu niende mkuu mpe tuu amasivyo yatakayokukuta ni zaidi ya huo mshahara. Naandika hivi nikiwa nimeshuhudia visa vingi kwa macho yangu sio kuambiwa
Yani kuna dada angu wa kazi ameniambiaa hivyooo aiseeee huu mtego...alafu 70k aiseee mbona balaaa
 
Duuuh kumbe wafanyakazi wa 35k wapo?? Naombeni connection
Me napata wa 70 kwenda juu
Hamna huyo ni vile tu amempata kitambo ila kwa huku mijini hamna anakuja kufanya kazi kwa 35,000 siku hizi.

Uuwiii! Mbona tunakoma siku hizi tena ukiwa na watoto wadogo ndio mtihani yaani kumpata wa kumlipa 70 tu ni kipengele.
 
Maisha si mchezo kuna wakati mambo yanakuwa magumu sana

Ova
 
Yani kuna dada angu wa kazi ameniambiaa hivyooo aiseeee huu mtego...alafu 70k aiseee mbona balaaa
Usiingie huu mtego, mpe pesa yake mkuu, mwambie akafungue hata account. Siku akibadilika hamna rangi utaacha ona!
 
Zuhura Ramadhani ambaye ni dada wa kazi za ndani amemshitaki mwajiri wake Khadija Katusi Muoza katika Serikali za Mtaa wa Mpiji Magoe Jijini Dar es Salaam akidai kutolipwa mshahara wake kwa muda wa miaka mitano.

Akisimulia kilichotokea Zuhura ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 30 anasema amefanya kazi kwa mwajiri wake huyo kwa zaidi ya miaka 14, lakini ndani ya miaka mitano iliyopita hakulipwa mshahara hali ambayo imesababisha amshitaki.

Akisimulia Zuhura anasema “Kipindi cha nyuma alikuwa akinilipa, mshahara wangu ulikuwa ni Tsh. 35,000 kwa mwezi, alisema kuwa mambo yake sio mazuri na ananihifadhia mshahara wangu kisha atanilipa.

“Nilipoona miaka inazidi kwenda bila kulipwa mshahara wangu ikabidi nianze kumsisitiza anipatie kwa kuwa nami pia nilikuwa nina mahitaji yangu, lakini akawa ananizungusha.

“Hapo kati mama yangu akanza kupata changamoto za kiafya akiwa Singida, ikatakiwa nianze kumuhudumia kwa kutuma fedha lakini sikuwa nayo, nilipomwambia mwajiri wangu (Khadija) akasema hana hela ya kunipa.

“Dada yangu wa Arusha akaenda kumchukua mama na kwenda ndaye Arusha kumuuguza, gharama za matibabu zilipotoka tukatakiwa kulipa Tsh. 360,000, mpaka sasa mama yangu bado anaumwa na yupo hospitali gharama zinazidi kuongezeka.

“Nilipoona tumeanza kutofautiana ikabidi niondoke hapo kwa bosi wangu lakini bado kesi yangu ikaendelea Serikali za Mtaa, (Khadija) alipoitwa akaahidi kwa maandishi kuwa atanilipa Tsh. 2,860,000 ikiwa ni kaisi ambacho ninamdai kwa kuwa kuna wakati nilikuwa natoa hela zangu mwenyewe na kununua vitu vingine ndani kwa ahadi kuwa atanirudishia.

"Hapo kati kuna siku alinitumia Tsh. 10,000 na kudai kuwa anapunguza deni, nikamrudishia kwa kuwa niliona anachofanya ni dharau.

“Alipoona hivyo Mei 22 (2023) akaniita Serikali za Mtaa na kutoa Sh 200,000, nilitaka niikatae lakini kwa kuwa mama anaumwa nikakubali na kuituma kwa mama Arusha. Baada ya hapo akaahidi kuwa atanilipa hela yote iliyosalia Mei 25 lakini haijawa hivyo, amekuwa kimya mpaka sasa.

“Kinachoniuma nimewalea Watoto wake vizuri, sijawahi kuwa na tatizo hata kidogo, mfano mtoto wake wa kwanza nilimkuta akiwa na umri wa miaka mitano na leo hii yupo form 6, pia nimewalea wengine wawili kwa upendo kwa muda wote.”

SERIKALI ZA MTAA YAFUNGUKA
Mwenyekiti wa Mpiji Magoge, Saidi Diuchile anasema “Kweli huyo binti anamdai aliyekuwa mwajiri wake, wameshaandikishiana hapahapa Serikali za Mtaa, deni jumla ni zaidi ya Sh 2,860,000, na amemlipa laki mbili.

“Uwezekano wa kumlipa kiasi chote sidhani kama hilo linawezekana kwa kuw ahata hiki kiwango alicholipwa Zuhuru ni baada ya kusumbuana na kumpresha mdaiwa.

“Nimeshauri kama akiendelea kusumbua Zuhura aende Mahakamani kwa kuwa nyaraka za maandishi zipo na mdaiwa amekiri kudaiwa.”

MDAIWA - KHADIJA KATUSI MUOZA
Anasema “Kweli mimi nadaiwa na hilo wala siwezi kulipinga, nimeishi naye vizuri tu, kilichotokea ni maisha kubadilika na mambo kuwa magumu, nia ya kumlipa ipo ila sina hela. Nikipata nitamlipa, ndio maana nimemshamlipa laki mbili.”

Alipoulizwa sababu za kutokumlipa dada wake wa kazi kwa muda wote huo wa miaka mitano, amesema “Maisha tu ndugu yangu, ningekuwa na hela ningemlipa ila sina.”

Kuhusu kama kweli Zuhura alikuwa akitmia fedha zake kuhudumia kwa ahadi kuwa atarejeshewa, anasema "Ni kweli alikuwa anatoa fedha zake nilizokuwa namlipa nyuma akahifadhi kwa ajili ya kunisaidia."
Wanyaturu wanyiramba warangi wadigo wabondei kwa kazi za uyaya nawapongeza sana mko vizuli sana tatizo waajiri ndio vimeo kama vipi tinga mahakamani bade lake kupigwa mnada
 
Hapa kwangu kuna bint yupo ila mambo yalipokuwa magumu nikawaeleza wazazi wake na yeye kuwa nimeshindwa kumlipa naomba arudi kwao lakini wote bint na wazazi walikataa na na kuniomba nikae nae kama mtoto wangu,hivyo yupo hapa home mwaka wa 3 sasa.
 
Miaka mitano bila mshahara na bado hajashtuka, alipaswa ashtuke kuanzia mwaka mmoja au miwili, na huyu binti atakuwa kaishi miaka mingapi hapo kwa huyo mwajiri wake? Manake kama alianza kazi mtoto mkubwa akiwa na miaka mitano na ameondoka mtoto akiwa form 6 basi aliishi miaka mingi sana hapo kwa huyo dada,.more than 10yrs
Mwaka mzima hulipwi?!

Alitakiwa ashtuke kuanzia miezi 3 kwa mbinde 6.
 
Zuhura Ramadhani ambaye ni dada wa kazi za ndani amemshitaki mwajiri wake Khadija Katusi Muoza katika Serikali za Mtaa wa Mpiji Magoe Jijini Dar es Salaam akidai kutolipwa mshahara wake kwa muda wa miaka mitano.

Akisimulia kilichotokea Zuhura ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 30 anasema amefanya kazi kwa mwajiri wake huyo kwa zaidi ya miaka 14, lakini ndani ya miaka mitano iliyopita hakulipwa mshahara hali ambayo imesababisha amshitaki.

Akisimulia Zuhura anasema “Kipindi cha nyuma alikuwa akinilipa, mshahara wangu ulikuwa ni Tsh. 35,000 kwa mwezi, alisema kuwa mambo yake sio mazuri na ananihifadhia mshahara wangu kisha atanilipa.

“Nilipoona miaka inazidi kwenda bila kulipwa mshahara wangu ikabidi nianze kumsisitiza anipatie kwa kuwa nami pia nilikuwa nina mahitaji yangu, lakini akawa ananizungusha.

“Hapo kati mama yangu akanza kupata changamoto za kiafya akiwa Singida, ikatakiwa nianze kumuhudumia kwa kutuma fedha lakini sikuwa nayo, nilipomwambia mwajiri wangu (Khadija) akasema hana hela ya kunipa.

“Dada yangu wa Arusha akaenda kumchukua mama na kwenda ndaye Arusha kumuuguza, gharama za matibabu zilipotoka tukatakiwa kulipa Tsh. 360,000, mpaka sasa mama yangu bado anaumwa na yupo hospitali gharama zinazidi kuongezeka.

“Nilipoona tumeanza kutofautiana ikabidi niondoke hapo kwa bosi wangu lakini bado kesi yangu ikaendelea Serikali za Mtaa, (Khadija) alipoitwa akaahidi kwa maandishi kuwa atanilipa Tsh. 2,860,000 ikiwa ni kaisi ambacho ninamdai kwa kuwa kuna wakati nilikuwa natoa hela zangu mwenyewe na kununua vitu vingine ndani kwa ahadi kuwa atanirudishia.

"Hapo kati kuna siku alinitumia Tsh. 10,000 na kudai kuwa anapunguza deni, nikamrudishia kwa kuwa niliona anachofanya ni dharau.

“Alipoona hivyo Mei 22 (2023) akaniita Serikali za Mtaa na kutoa Sh 200,000, nilitaka niikatae lakini kwa kuwa mama anaumwa nikakubali na kuituma kwa mama Arusha. Baada ya hapo akaahidi kuwa atanilipa hela yote iliyosalia Mei 25 lakini haijawa hivyo, amekuwa kimya mpaka sasa.

“Kinachoniuma nimewalea Watoto wake vizuri, sijawahi kuwa na tatizo hata kidogo, mfano mtoto wake wa kwanza nilimkuta akiwa na umri wa miaka mitano na leo hii yupo form 6, pia nimewalea wengine wawili kwa upendo kwa muda wote.”

SERIKALI ZA MTAA YAFUNGUKA
Mwenyekiti wa Mpiji Magoge, Saidi Diuchile anasema “Kweli huyo binti anamdai aliyekuwa mwajiri wake, wameshaandikishiana hapahapa Serikali za Mtaa, deni jumla ni zaidi ya Sh 2,860,000, na amemlipa laki mbili.

“Uwezekano wa kumlipa kiasi chote sidhani kama hilo linawezekana kwa kuw ahata hiki kiwango alicholipwa Zuhuru ni baada ya kusumbuana na kumpresha mdaiwa.

“Nimeshauri kama akiendelea kusumbua Zuhura aende Mahakamani kwa kuwa nyaraka za maandishi zipo na mdaiwa amekiri kudaiwa.”

MDAIWA - KHADIJA KATUSI MUOZA
Anasema “Kweli mimi nadaiwa na hilo wala siwezi kulipinga, nimeishi naye vizuri tu, kilichotokea ni maisha kubadilika na mambo kuwa magumu, nia ya kumlipa ipo ila sina hela. Nikipata nitamlipa, ndio maana nimemshamlipa laki mbili.”

Alipoulizwa sababu za kutokumlipa dada wake wa kazi kwa muda wote huo wa miaka mitano, amesema “Maisha tu ndugu yangu, ningekuwa na hela ningemlipa ila sina.”

Kuhusu kama kweli Zuhura alikuwa akitmia fedha zake kuhudumia kwa ahadi kuwa atarejeshewa, anasema "Ni kweli alikuwa anatoa fedha zake nilizokuwa namlipa nyuma akahifadhi kwa ajili ya kunisaidia."
Miaka yote kavumilia kufanya kazi bila malipo?!

Alitakiwa avumilie miezi 3 hadi 6 tu, then asanuke.
 
Yaani mie Wasambaa Wanyaturu sina hamu [emoji119]nilimtoa mdada Singida hafanyi kazi mie ndo nafanya kazi na mimba yangu ya kuzaa nikaona hapana nikaongea nae ajirekebishe akasema yeye aliambiwa kuna kazi dar ya Bar nauli hana aliposikia nataka mdada kwa shoga yake akaona aje apate kufika dar ila kazi za ndani haitaji basi nikamruhusu nikampa mshahara wa wiki 2 alizokaa tukaagana kiroho safi mpaka leo anakuja kwangu kusalimia akikaa anakuja Dada nimekuja kukuona kapendeza na kaweupe ka kinyaturu na shape MashaAllah mji umemkubali.
Naomba namba yake
 
Nmependa majibu ya mdaiwa-Bi hadija

HAKIKA NI MUUNGWANA SANA,

Nia ya kulipa anayo,Sema Mambo yamebana[emoji106]

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kwa maelezo inaonyesha mwajiri sio mkorofi bali maisha yamebadilika
Mwajiri bomba kabisa,
Ndo maana wameweza kuishi miaka yote bila kulipwa Hadi anamkopa housegal wake

Inaonekana walishajenga undugu kabisa

Sema hili suala mpk wamefikishana uko huenda Kuna Watu nje wanapush mwajiri akomolewe[emoji26]

Back
Top Bottom