Kwa nini mnakuwa na mahousegelo nyie wanawake?Duuh mi sipendi kabisa kupitisha maana ukilimbikiza miezi 2 tuu laki na 20 ndo miaka 5 si nitafungwa..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa nini mnakuwa na mahousegelo nyie wanawake?Duuh mi sipendi kabisa kupitisha maana ukilimbikiza miezi 2 tuu laki na 20 ndo miaka 5 si nitafungwa..
Hapana lazima uwe na utu mbona watoto wake mda wana upata wa kusoma mtu mwenye roho mbaya lazima atafute visababu vya kusaidia.Sure.....ila tatizo unakuta yy ndo kila kitu nyumba watoto n.k huo muda wa kusoma saa ngapi
Mambo mengi mkuu...siku hizi si mnataka tusaidiane kuleta msosi? Sasa tukikaa nyumbani tunatoa wapi.?Kwa nini mnakuwa na mahousegelo nyie wanawake?
Yah..unakuta mtu ana mtoto mmoja yuko home tuu sidhani kama kuna ulazima w mdada..sema jamii yetu ndo imeshakua hivyoWengine hulazimisha kua na wasichana wakazi wakati huwezo hawana, kweli wewe mko watatu nyumbani na mama hafanyi kazi msichana wakazi ni nini ndo madeni tunao accumulate tuache kuiga majirani.
Mhm msosi gani mnaletaga nyie bwana 90%ya billz ndani ya nyumba vidume tunawajibika.Mambo mengi mkuu...siku hizi si mnataka tusaidiane kuleta msosi? Sasa tukikaa nyumbani tunatoa wapi.?
Ukiona binti wa kazi anafanya ukatiri kwa watoto wa boss wake, basi jua chanzo ni boss mwenyeweZuhura Ramadhani ambaye ni dada wa kazi za ndani amemshitaki mwajiri wake Khadija Katusi Muoza katika Serikali za Mtaa wa Mpiji Magoe Jijini Dar es Salaam akidai kutolipwa mshahara wake kwa muda wa miaka mitano.
Akisimulia kilichotokea Zuhura ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 30 anasema amefanya kazi kwa mwajiri wake huyo kwa zaidi ya miaka 14, lakini ndani ya miaka mitano iliyopita hakulipwa mshahara hali ambayo imesababisha amshitaki.
Akisimulia Zuhura anasema “Kipindi cha nyuma alikuwa akinilipa, mshahara wangu ulikuwa ni Tsh. 35,000 kwa mwezi, alisema kuwa mambo yake sio mazuri na ananihifadhia mshahara wangu kisha atanilipa.
“Nilipoona miaka inazidi kwenda bila kulipwa mshahara wangu ikabidi nianze kumsisitiza anipatie kwa kuwa nami pia nilikuwa nina mahitaji yangu, lakini akawa ananizungusha.
“Hapo kati mama yangu akanza kupata changamoto za kiafya akiwa Singida, ikatakiwa nianze kumuhudumia kwa kutuma fedha lakini sikuwa nayo, nilipomwambia mwajiri wangu (Khadija) akasema hana hela ya kunipa.
“Dada yangu wa Arusha akaenda kumchukua mama na kwenda ndaye Arusha kumuuguza, gharama za matibabu zilipotoka tukatakiwa kulipa Tsh. 360,000, mpaka sasa mama yangu bado anaumwa na yupo hospitali gharama zinazidi kuongezeka.
“Nilipoona tumeanza kutofautiana ikabidi niondoke hapo kwa bosi wangu lakini bado kesi yangu ikaendelea Serikali za Mtaa, (Khadija) alipoitwa akaahidi kwa maandishi kuwa atanilipa Tsh. 2,860,000 ikiwa ni kaisi ambacho ninamdai kwa kuwa kuna wakati nilikuwa natoa hela zangu mwenyewe na kununua vitu vingine ndani kwa ahadi kuwa atanirudishia.
"Hapo kati kuna siku alinitumia Tsh. 10,000 na kudai kuwa anapunguza deni, nikamrudishia kwa kuwa niliona anachofanya ni dharau.
“Alipoona hivyo Mei 22 (2023) akaniita Serikali za Mtaa na kutoa Sh 200,000, nilitaka niikatae lakini kwa kuwa mama anaumwa nikakubali na kuituma kwa mama Arusha. Baada ya hapo akaahidi kuwa atanilipa hela yote iliyosalia Mei 25 lakini haijawa hivyo, amekuwa kimya mpaka sasa.
“Kinachoniuma nimewalea Watoto wake vizuri, sijawahi kuwa na tatizo hata kidogo, mfano mtoto wake wa kwanza nilimkuta akiwa na umri wa miaka mitano na leo hii yupo form 6, pia nimewalea wengine wawili kwa upendo kwa muda wote.”
SERIKALI ZA MTAA YAFUNGUKA
Mwenyekiti wa Mpiji Magoge, Saidi Diuchile anasema “Kweli huyo binti anamdai aliyekuwa mwajiri wake, wameshaandikishiana hapahapa Serikali za Mtaa, deni jumla ni zaidi ya Sh 2,860,000, na amemlipa laki mbili.
“Uwezekano wa kumlipa kiasi chote sidhani kama hilo linawezekana kwa kuw ahata hiki kiwango alicholipwa Zuhuru ni baada ya kusumbuana na kumpresha mdaiwa.
“Nimeshauri kama akiendelea kusumbua Zuhura aende Mahakamani kwa kuwa nyaraka za maandishi zipo na mdaiwa amekiri kudaiwa.”
MDAIWA - KHADIJA KATUSI MUOZA
Anasema “Kweli mimi nadaiwa na hilo wala siwezi kulipinga, nimeishi naye vizuri tu, kilichotokea ni maisha kubadilika na mambo kuwa magumu, nia ya kumlipa ipo ila sina hela. Nikipata nitamlipa, ndio maana nimemshamlipa laki mbili.”
Alipoulizwa sababu za kutokumlipa dada wake wa kazi kwa muda wote huo wa miaka mitano, amesema “Maisha tu ndugu yangu, ningekuwa na hela ningemlipa ila sina.”
Kuhusu kama kweli Zuhura alikuwa akitmia fedha zake kuhudumia kwa ahadi kuwa atarejeshewa, anasema "Ni kweli alikuwa anatoa fedha zake nilizokuwa namlipa nyuma akahifadhi kwa ajili ya kunisaidia."
Kweli aisee...Mhm msosi gani mnaletaga nyie bwana 90%ya billz ndani ya nyumba vidume tunawajibika.
Nyie ata luku ikiisha utasikia baba mwenye nyumba yupo safarini bado mnashindwa nunua. Kaeni tuu nyumbani hamna faida yoyote kwenye maofisi...kwanza kutega mabosi tuu na mitako yenu🤣🤣🤣🤣
Yaani humu malaika bwana..Huyo anaongea pumba, anasahau kuwa binti kafanya kwa miaka 14.
Hawa sio tu kazi waligeuka kuwa familia.
Na mwajiri mambo yameharibika miaka 5 iliyopita, so hiyo 35k kwa miaka ya nyuma hienda ulikuwa mshahara mkubwa
Yes, mawasiliano yanapatikana.Mawasiliano yake yanapatikana mkuu?
Hapana muvumilia ni mwendo wakuwainamisha kwa desk tuuKweli aisee...
Ila mtuvumilie tuu na mitako yetu
Ohhhhh kumbe, pole sana.huyu ni mzee mama[emoji1787]
Inategemea ntu na ntu...mi hata kunikaribia tuu unajiuliza mara mbili...ndo uniinamishe kabisa? 😆 😆 😆 😀 😆Hapana muvumilia ni mwendo wakuwainamisha kwa desk tuu
Huyu ungemkata hela ya nauli tuYaani mie Wasambaa Wanyaturu sina hamu 🙌nilimtoa mdada Singida hafanyi kazi mie ndo nafanya kazi na mimba yangu ya kuzaa nikaona hapana nikaongea nae ajirekebishe akasema yeye aliambiwa kuna kazi dar ya Bar nauli hana aliposikia nataka mdada kwa shoga yake akaona aje apate kufika dar ila kazi za ndani haitaji basi nikamruhusu nikampa mshahara wa wiki 2 alizokaa tukaagana kiroho safi mpaka leo anakuja kwangu kusalimia akikaa anakuja Dada nimekuja kukuona kapendeza na kaweupe ka kinyaturu na shape MashaAllah mji umemkubali.
Mhm atakubali bwana wewe hapa jf.Inategemea ntu na ntu...mi hata kunikaribia tuu unajiuliza mara mbili...ndo uniinamishe kabisa? 😆 😆 😆 😀 😆
Ebu piga pass ya upendo basi jamani kumbe unajua kabisa totoz la ukweli basi nipatie contact zake mie nimuoe kabisaYaani mie Wasambaa Wanyaturu sina hamu 🙌nilimtoa mdada Singida hafanyi kazi mie ndo nafanya kazi na mimba yangu ya kuzaa nikaona hapana nikaongea nae ajirekebishe akasema yeye aliambiwa kuna kazi dar ya Bar nauli hana aliposikia nataka mdada kwa shoga yake akaona aje apate kufika dar ila kazi za ndani haitaji basi nikamruhusu nikampa mshahara wa wiki 2 alizokaa tukaagana kiroho safi mpaka leo anakuja kwangu kusalimia akikaa anakuja Dada nimekuja kukuona kapendeza na kaweupe ka kinyaturu na shape MashaAllah mji umemkubali.