Kula karanga, korosho, pweza, sambusa, mishikaki, maziwa, mayai, matunda kwa muda tofauti katika siku sio kula hovyo hovyo, hivi ni aina ya vyakula vyenye virutubisho vingi muhimu lakini pia visivyo na side effects nyingi vikizidi. Kula hovyo ni ulaji wa vyakula vya sukari, junk foods na kushindilia tumbo mikate, chapati, ugali au wali katika mlo mmoja.
Kwa nini hivyo vitu usinunue ukahifadhi Hom, Uwe unaandaliwa, kumbuka hivi vya kununua vikiwa tayari vimeandaliwa(mfano kula kwa mama ntilie sio salama)
Vuta picha mama ntilie anaweka panadol/magadi kwenye maharage ili yaive haraka
Unawekewa Bia kwenye nyama ili iive haraka
Hao wauza supu ya Pweza wanachanganya na Viagra ili watumiaji tuamini supu ya pweza inaongeza nguvu za kiume
Mpaka wauza karanga eti wanatumia kemikali kwa ajili ya kukaanga karanga
Hapo hatujahusisha uchafu tunaolishwa kutokana na imani za kishirikina (kutumia maji yaliooshewa maiti)
Unanunua vitumbua mpishi kachambia sehemu za siri tukiachana na hizi chapati ambazo tunashuhudia wanatumia vipande vya godoro
Wale wa juisi ya miwa hatujui yale maji wanayogandishia barafu usalama wake upoje hii ni moja ya sababu inayonifanya niwaambie wanikamulie yamoto na huwa nakuwa makini haswa
Binafsi nimemuelewa sana mke wangu kuniletea rafiki yake awe ananipikia, na anajua kupika haswa kama yeye mwenyewe
Kazi yangu ni kununua mahitaji ya kuwekwa kwenye friji yatawekwa muhimu nile kilicho salama tu
Hata juisi hataki ninunue ananiambia tu lete matunda nitakutengemezea juisi unayohitaji
Tukirudi huko mahotelini, hatujui mazingira ya jikoni yapoje
Binafsi nimekula kwa mama ntilie miaka si chini ya 20
Ila naamini chakula salama ni kile unachokiandaa au kinachoandaliwa na mtu anayekujali, sio hivi vya biashara
Note: KUNA MAZINGIRA YANATULAZIMU KULA HIVYO VYAKULA VILIVYOANDALIWA TAYARI HATA KAMA SI SALAMA KWA 100% ILA NDO HIVYO HATUNA JINSI TUNAAMUA TU LIWALO NA LIWE