Dar es Salaam kuna vumbi sana kipindi hiki ila ukivaa Barakoa na kunawa mikono unaonekana mshamba!

Dar es Salaam kuna vumbi sana kipindi hiki ila ukivaa Barakoa na kunawa mikono unaonekana mshamba!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kiukweli Dar es Salaam kipindi hiki kuna joto na vumbi kali linalopulizwa na upepo wa hapa na pale.

Kwa kawaida vumbi hubeba vijidudu vya kila aina hasa ukizingatia wakazi wa Dar wana tabia ya kutema mate na kupenga kamasi hovyo hovyo tu.

Japokuwa ukivaa barakoa unaonekana " wakuja" lakini kwa vumbi hili heri lawama kuliko fedheha, barakoa na kunawanawa ni muhimu ili utembee salama barabara za vumbi.

Nawatakia Dominica yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hilo vumbi itakuwa ndio limeanza mwaka huu, miaka iliyopita hapakuwahi kuwa na vumbi dsm au labda barakoa zilikuwa bado hazijatengenezwa?!

Semeni ukweli uwaweke huru, Tanzania ni sehemu ya ulimwengu sisi sio kisiwa kilichopo sayari nyingine.
 
Huyu mtoto wa Lumumba ni kichaa, anadhani wote ni MATAGA ambao akili zao zinashikiliwa na mtu mmoja aliyeko Karagwe
 
Tutatengeneza mabarabara ya kiwango cha Rami mpaka vichocboroni vumbi liishe
Tanzania ni nchi tajiri sana tutashirikiana na Matajiri wenzetu waChina

Nasema uongo ndugu zangu?
Kweeeeriiiiiiiiiiii

Mitano teeenaaaaaaa

Tumeipenda wenyeweeeeeww

Wacha ituuuuuweeeeeeee
 
Acha zako, talalilla, sema kuna corona, kuwa muwazi, sema we need to observe measure against corona as stipulated by WHO. Stop Magufulis' indoctrination about corona!
Tulisha piga maombi na Mungu akatujibu kwa kuisambaratisha Corona
 
Jamaa kafikisha ujumbe wenye akili wataelewa. Vaa barakoa kuzuia vumbi maana barakoa zipo kabla ya Corona na zina matumizi tofauti. Wewe vaa mwisho wa siku kila mtu atabeba msalaba wake, wakati mwingine ushamba unasaidia kuliko kujuwa kila kitu. Ukiwa mjinga utapata msaada ila wewe unajuwa kila kitu wanakuacha. Tuvae barakoa vumbi lipo tunawe mikono kabla ya kula ndio ustaarabu.
 
Acha zako, talalilla, sema kuna corona, kuwa muwazi, sema we need to observe measure against corona as stipulated by WHO. Stop Magufulis' indoctrination about corona!
Una ushahidi au unabwabwaja tu bwashee?!!
 
Hilo vumbi itakuwa ndio limeanza mwaka huu, miaka iliyopita hapakuwahi kuwa na vumbi dsm au labda barakoa zilikuwa bado hazijatengenezwa?!

Semeni ukweli uwaweke huru, Tanzania ni sehemu ya ulimwengu sisi sio kisiwa kilichopo sayari nyingine.
Mabadiliko ya tabia nchi!
 
Back
Top Bottom