Dar es Salaam kuna vumbi sana kipindi hiki ila ukivaa Barakoa na kunawa mikono unaonekana mshamba!

Aina hili la vumbi limekuwa maarufu sana kuliko mavumbi ya aina nyengine yote japokuwa wenye kupata mafua kutokana na vumbi hili wengi hupona ila bado watu huliogopa na kuliongelea hili vumbi kuliko mavumbi mengine,pamoja na uchache wa vifo vya mafua yenye kusababishwa na hili vumbi ila vifo hivyo hutisha sana watu kuliko wingi wa vifo vya mafua yenye kusababishwa na mavumbi ya aina nyengine.
 
Hilo vumbi itakuwa ndio limeanza mwaka huu, miaka iliyopita hapakuwahi kuwa na vumbi dsm au labda barakoa zilikuwa bado hazijatengenezwa?!

Semeni ukweli uwaweke huru, Tanzania ni sehemu ya ulimwengu sisi sio kisiwa kilichopo sayari nyingine.
Kabisa yaaani
 
Pole pole amekuruhusu kuandika uzi wa kuikwepa corona au umejilipua tu
 
Na jioni watu wanywe maji moto Maana kuna kabaridi sana ni muhimu watu wakaachana na vinywaji vya baridi
 
Na wewe unaogopa kusema corona ipo hadi usingizie vumbi? Vumbi la Dar umeliona mwaka huu pekee? Lakini afadhali umeona na kubaini uongo wa viongozi wako wa CCM kuhusu corona, chukua hatua hata CCM wakikuona mshamba ilimradi hakuna sheria ya kukuzuia kuvaa barakoa.
 
Joni siutuambie kuna neunonia tuu inayoenea kama kale kaugonjwa kama fua.
 
Jiandae kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa kutangaza ugonjwa huu wakati huna mamlaka hayo. Tumefikia mahali hakuna ruhusa ya kuusema ukweli kwa ajili ya kulinda sifa za kisiasa.
Wametoka mpaka number za simu eti ukiona mtu anaongelea huu ugonjwa kwenye magroup screenshot alafu utume kwa nambers zao🥶🤐
Nchi za wenzetu mtu wa/familia ya taifa lao akitishiwa maisha au akitekwa tu vyombo vinavyohisika vinahangaika kuokoa maisha ya huyo mtu au familia yake no matter what it's gonna take lakini bongo serikali halilitambui hilo jukumu lake.
 
Tuna pelekwa kama kondoo na mtu mmoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…