Dar es salaam limegeuka jiji la makelele, Serikali imelala?

Mkuu,

Wewe ni mkongwe, kwanini usiwasilishe lalamiko lako na sheria ichukue mkondo wake?

SHERIA NA KANUNII.
"..Sheria ya Mazingira, 2004 Kifungu 106(5) (5) Si ruhusa kwa mtu yeyote kupiga kelele aukusababisha kelele kuzidi kiwangokilichoainishwa au kitakachobainishwakuhusiana na upigaji kelele. (6) Litakuwa ni kosa kwa mtu yeyote kumwagauchafu au kupiga kelele bila kuzingatia njiailiyobainishwa kuwa ni bora katika Kanunizinazoweza kutungwa na Waziri.II. Kanuni za Usimamizi wa Mazingira zaViwango vya Udhibiti wa Kelele na Mitetemoza mwaka 2015Katika kudhibiti kelele na mitetemo, Waziri mwenyedhamana ya mazingira kupitia Kifungu cha230(2)(s) cha Sheria ya Usimamizi wa MazingiraSura 191, mwaka 2015 alitunga Kanuni zaUsimamizi wa Mazingira za Viwango vya Udhibitiwa Kelele na Mitetemo za mwaka 2015 (Tangazo laSerikali Na. 32 la mwaka 2015).."
 

Attachments

Ivi mashirika ya kutetea haki za binadamu watusaidie watembea miguu bodaboda wametawala Hadi mwendokasi,dar imekuwa sio salama Tena kwa mtembea kwa miguu( watu kipato Cha chini).Serilali,Vyama Sasa, Police haoni hawa bodaboda wanatugonga wanakimbia .
 
Tatizo ni mipango mji.
Maeneo mapya yapimwe na kuzingatia upana wa barabara za mtaa na huduma kwa jamii,
Zoezi liwe endelevu la upimaji wa mji.
 
Yote haya sababu kubwa ni;
1. CCM, hawa jamaa wameshindwa kabisa kupitiq serikali zake kuhamasisha mipango miji, wapi makanisa yakae, wapi masoko yakae, wapibiashara ndogondogo zikae, wapi viwanja viwekwe, nyumba zijengwe kwa mipango sio kiholela. CCM imefeli sana kwenye swala la mipango miji, tuna jiji la hovyo, chafu lenye kelele kila kona.
2. Umasikini wa fikra na vipato, yaani kila kona ni biashara, rasmi na zisizo. Matangazo ya viwanja kupitia spika za kichina ni kila mahali.

Kuna haja ya kuangalia namna nyingine ya kuishi, huko Moro, Tanga nk huenda mtu ukawekeza na kuishi kwa amani.
 

Mama yuko bize kununua magoli ya Simba na Yanga, vitu muhimu kama hivi tunavyojadiili humu hana time navyo.
 
Sheria zipo sana tu lakini wa kuzisimamia kisawasawa ndio tatizo !
Maana akizisimamia sawasawa watu wengine watakuja kuingiza siasa zao humo ghafla mambo yanarudi tena kulekule tulikotoka !
 
Dalafala za Temeke Buza zina spika kwa nje.
 
Kinondoni inaongoza kwa kelele kwa sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…