Dar es Salaam ni mkoa uliojaa masikini wengi wanaojificha kwenye kivuli cha miundombinu tu

Wanajua dar ndiyo sehemu yenye unyama mwingi tz na kila maendeleo zaidi yapo dar hapa tz
 
Pls,tunazungumzia mafukara wewe sio fukara
 
Watu wa mikoani mnateseka sana na Dar, hamna sehemu yakuishi na kutoboa kirahis kama Dar.
 
Jamani msitujazie wingi Daslam. Maana mtafanya rural to Daslam migration iongezeke.

Kila mtu ashinde mechi zake.


By the way kuhusu ukwasi wa fursa za Daslam watakupa ndugu zako waliozamia kama wewe uliyeifata AFRICA SUPER LEAGUE, Daslam.
 
Kitu ulichoacha kukitafiti ni "population density".

Population ya watu ni uchumi kama ulikuwa huelewi sasa.

Ndiyo maana hata biashara kichaa Dar zinalipa vizuri tu.

Sehemu zingine ukipeleka biashara ya kipumbaf pumbaf unakufa njaa ama kufirisika.

Mfano biashara ya utumbo na makanyagio ya kuku waweza ifanya mikoani ukatoboa,
?
Lakini Dar je?
 
Kijana usifananishe bei za ardhi Dar na Mikoani, naona umekomalia ujenzi tu huku ukisahau thamani ya makazi siyo nyumba tu bali, na eneo iliyopo hiyo nyumba

Tukijumlisha hivyo vyote, tutakuta wanaojenga Dar wanatumia gharama nyingi kuliko wanaojenga Mikoani au nje ya miji, ndio maana nyumba za kupanga Dar ni ghali kuliko Mikoani mkuu

Nyumba yenye kodi ya 500K Mikoani ni kubwa na nzuri kuliko yenye kodi hiyo hiyo Dar, sasa ingekuwa Mikoani ujenzi ni gharama kuliko Dar, basi nyumba za kupanga zisingeshikika kwenye kodi
 
Hata mkoani kuna maeneo kodi ni mlima. Swala la kodi inategemea na potentiality ya eneo kibiashara na fursa zingine au idadi ya watu kwenye eneo husika. Mfano kodi ya eneo kama chanika kwa nyumba za kawaida itakua chini ukilinganisha na maeneo ya mkoani yaliuopo senta za kibiashara nk. Tuitumie hiyo hiyo chanika mpaka mvuti kule ingia ndani kodi ni ndogo ukilinganisha hata na arusha mjini pale, moshi tena hata moshi pembeni km kcmc nk kodi kule ni kumbwa kulinganisha na eneo kama chanika hata mbagala au gongo la mboto
Coz kcmc uhitaji wa wanafunz nk ni mwingi saana vyumba bei juu kulingakisha na mifano hiyo niliyokupa
 
Sasa mkuu kwanini Dar umetolea mifano maeneo ya nje ya mji kama Chanika na Mvuti, ila Mikoani umetoa mifano maeneo ya mijini, kwanini hiyo hiyo Dar usitolee mifano kama Mikocheni au Sinza nk

Au kwanini huko Mikoani usitolee mifano ya maeneo yaliyo nje ja miji, Dar yote maeneo ni Potential, labda yale maeneo ambayo yako mwishoni kabisa mwa mji kama unaenda Pwani ndio angalau kidogo

Tena napo inategemea maana kuna maeneo kama Ununio na Mbweni, yako nje ya mji ila bei zake hazishikiki, ila huko Mikoani kuna maeneo kibao katikati ya miji yana bei rafiki kabisa achilia mbali vijijini
 
nimenunua ardhi Dsm, nimenunua ardhi mikoa kama mitatu pia. usijifariji. popote ulipo inategemeana na ardhi unanunua wapi, ila kwenye ordinary people hapo dsm ardhi ni bei ndogo kuliko mikoa kama mwanza, arusha, mbeya, dodoma na kwengine.
 
Sijasema hakuna life nimesema kwa Tanzania, Dar ndio sehemu mtu anaweza kuanzia zero tu hero kuliko sehemu yeyote Tanzania, tukiongelea Dar usiiweke Mwanza mkuu, na wala sijabeza mkuu ila nakwambia Dar imeshindikana kuliko kwote ulipotaja, unadhani sijapita huko mkuu ? Nimepita ila tuwe wakweli Dar ni mwisho wa matatizo, mkuu we dar unajua wapi na wapi labda ? Dar hata wingi wa watu unachangia kwanini hamkubali kwamba hakuna mkoa hata unaofikia nusu ya Dar mzee kwani Tatizo nini ? โ€ฆUnadhani kwanini Rostam, Bakhresa, na Mo wote wapo dar es salaam na Masaki ? Kwanini unadhan top 5 ya wealthy people in Tanzania wote wapo Dar ? Maisha ni popote ila Dar kwa wapiga kazi ina fursa kuliko mkoa wowote ule Tanzania, dar maandaz unauza, maji unauza , yan vitu ambavyo mkoani unapata bureโ€ฆ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ