Dar es Salaam: Nyumba yapigwa mnada kwa kushindwa kulipa milioni 7

Dar es Salaam: Nyumba yapigwa mnada kwa kushindwa kulipa milioni 7

kama huna uwezo wa kukopa acheni,tunalaumu wakopeshaji ilihali ni matatizo yetu yanatupeleka kukopa na hatulazimishwi.
 
Ingepaswa iwe Riba kiasi gani Kwa miaka miwili kulingana na uzoefu wako au jinsi unavyoelewa?



Kwa mujibu wa BOT kwa watoa mikopo midogo midogo riba ni 3.5% reducing P.M

Sasa lets say huyu akatumia straight line ili ampopoe mwenye nyumba.
3.5% × 12 × 3 = 1.26.


7,000,000 + (7,000,000 × 1.26) = 15, 820,000/=
Ukijumlisha na gharama za kukusanya madeni inakuwa

15, 820, 000 + 1,500,000= 17,320,000. Hapa ni Riba Jumlisha Principle.

Ukitumia reducing kama inavyopaswa kuwa ingecheza kwenye 15m ambapo kama imeuzwa kwa 23, mwenye nyumba angepewa kwenye 7m kwa hayo mauzo.

Kama sijakosea yeye anasema riba tu imeongezeka ikawa 17m. Sasa imepatikanaje?
 
Afisa mikopo nae katoaje pesa wakati mtu hana biashara


Kuna kipindi hapo nyuma michezo ya mijini ilichezwa hivi:

Wanakuja wadada wazuriii unashawishiwa ukope bila hata vigezo, wanakupamba na kukuaminisha una uwezo na ukipata mtaji utafika mbali, ila kumbe kuna wahuni wameshaweka target mwakani wananunua nyumba yako bei chee.

Kama nyumba yako ina thamani ya M150, unakopeshwa M20 hadi M30. Halafu kinachofanyika mnunuzi wa nyumba yako anaandaa M50. Hapo M20/30 ni ya kuinunua nyumba yako na inayobaki ya kukutuliza wewe na ukigoma itatumika kuweka mazingira sawa mahakamani kwenye kesi.

Ukikopa tu ukafeli kurejesha hizo notice ni chap chap hujakaa sawa ushaletewa wakusanya madeni, hujakaa sawa mnunuzi kaja kukupa dili uchukue M20 yeye alipe deni umekataa hujakaa sawa mnada.

Ukibahatika mahakamani ukawa na mwanasheria mzuri ndo mambo kama hayo yanatazamwa. Mkopaji ana sifa za kukopeshwa?
 
Nishawishiwe mkopo kisa wadada wazuri 😆😂🤣 aisee tutaishia kulana kimasihara tu hakuna kingine
Sasa si hizo akili unazo wewe. Unadhani mmasai kaingia mjini, kauza uza mifugo kajenga eneo mafuta akikutana na wadada na komwe zao na uniform wakamjaza sifa atafanyaje?
 
Niliona picha ya hiyo nyumba sehemu wahuni wamezurumu nyumba sio ya 7m ile hata familia wangeamua kuuza wenyewe huko kimara kwanza pana kiwanja kikubwa vile cha 7m daslm watu wezi sana....pana vitu tutavijua zaidi huko mbele...
Hiyo ndio kazi ya makanisa
 
Back
Top Bottom