Nimeshuhudia mwaka huu mwanzoni ndugu yangu naye ilibakia ponya ponya nyumba yake iuzwe tukaingilia kati,ila hii ilikuwa ni taasisi ya kiserikali.Kifupi ni kuwa sidhani kama nyumba itarudishwa,kama kulikuwa na makubaliano waliingia na aliyakubali,tena kwa maandishi,sijui kama hiyo haki ataipata.Mikopo imewafanya watu wajiue,mikopo imesababisha baadhi ya watu kupata mapresha na na kisukari,mikopo imesababisha familia zikasambaratika na hata ndoa kuvunjika,inahitajika elimu kwanza kabla kuchukua na sio kukurupuka...