Dar es Salaam: Nyumba yapigwa mnada kwa kushindwa kulipa milioni 7

Huyu mwenzenu anataka kuuza kituo cha watoto yatima.
Waumini wa Msikiti wa Ijumaa Mwanza wamvaa Bim na nduguye Sheraly kuhusu shule ya Thaqafa na Msikiti wa Ijumaa

Na hawa Saudi Arabia waliogoma kuipa mkopo Pakistan ndugu zao katika imani nao vipi, tena wakawaelekeza IMF ambao wanatoza riba au hilo Saudi hawajui. Hapo Pakistan wametoka kukumbwa na mafuriko yaliyopata 40% ya nchi nzima. Saudi refuses to give Pakistan interest-free loan

Saudi Arabia inatoza riba vizuri tu kwa kuiita "commission", alafu nenda Amana bank uone kama unapewa hela bure.
World Bank to Get $750‐Million Loan From Saudi Arabia (Published 1974)

Hiyo sheria haitekelezeki kirahisi hivyo, na kukopa mtu halazimishwi wala kuweka rehani vitu hapangiwi. Ukikosa kujiongoza mwenyewe ukasubiri huruma utaumia. Tumia akili
Ttzo upo mbali na Uislamu sahihi

Mnashadidia sana Uislamu wa mitandao ambao sio sahihi
 
Dar es Salaam. Familia ya Festo Aaron, inayoishi Kimara Bonyokwa iko njia panda baada ya kukosa makazi kutokana na nyumba yao kupigwa mnada na taasisi ya Uwezo Financial Service kwa kushindwa kurejesha deni la Sh7 milioni.

Mwaka 2020 familia hiyo yenye watoto watano ilikopa Sh6 milioni katika taasisi ya Uwezo inayodaiwa kuwa na uhusiano na waumini wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) kwa makubaliano ya kurejesha Sh7 milioni ndani ya mwaka mmoja.

Taasisi hiyo imekuwa ikikopesha fedha hizo kwa kuzingatia sifa mbili, ambazo ni mkopaji awe muumini wa dhehebu hilo awe mwaminifu katika kutoa fungu la kumi kila mwaka.

Akizungumza na Mwananchi, Festo alisema mwaka 2020, mke wake Happy Josia alikopa kwenye taasisi hiyo Sh6 milioni lengo wakipata fedha hizo wapate mtaji wa kuanzisha biashara.

“Makubaliano yalikuwa kurejesha riba ya Sh1 milioni kwa kiasi tulichokopa, tulitakiwa kurejesha Sh7 milioni ndani ya mwaka mmoja,” alisema Festo.

Amesema fedha hizo walizielekeza kwenye biashara ya nguo na viatu katika duka waliloanzisha maeneo ya Kimara lakini hata hivyo janga la Uviko-19 lilotokea kwa mwaka huo lilisababisha biashara yao kwenda mrama.

“Tulipambana na kufanikiwa kufanya rejesho moja Sh500,000 lakini hata hivyo mambo yalizidi kwenda ovyo ndipo tulipoenda kufanya mazungumzo na taasisi kuwaeleza hali halisi na wakatuongezea muda,” amesema.

Festo amesema miezi michache baadae walipotaka kwenda kulipa deni hilo waliambiwa riba imeongezeka hadi kufikia Sh10 milioni kutoka Sh7 milioni jambo lilowashangaza na kwenda kwa wachungaji wa Kanisa hilo lakini hata hivyo hawakupata msaada.

“Hadi mwanzoni mwa mwaka huu tuliambiwa deni riba yake imefikia Sh17 milioni hivyo tulishangaa na kuwauliza imefikaje? Wakawa hawataki mazungumzo tena ndipo wakaanza kutangaza mnada nyumba yetu na wakauza kwa Sh 23milioni,” amesema.

Happy ambaye ndiye aliyekopa amesema anashangazwa na uharaka wa kuiuza nyumba hiyo.

“Tunaziomba mamlaka kuongea na taasisi hii ikubali kutuachia nyumba yetu na iridhie kurejesha deni la msingi la Sh7 milioni tulilokopa ili tuendelee na maisha,”amesema.

Mwananchi, lilizungumza na Mchungaji wa kiongozi wa Kanisa la TAG Kimara, Ruth Temu amesema taarifa za familia hiyo kukutana na kadhia hiyo alishazipata na ana mpango wa kwenda kuzungumza nao.

“Siwezi kusaidia chochote kuhusu hili sakata japo taasisi iliyokopesha naijua lakini masharti waliyokubaliana siyajui kwa hiyo siwezi kuwasaidia chochote,” amesema Temu.

Alipotafutwa ofisa mikopo wa taasisi ya Uwezo, Patro Mwashambwa alikiri kuidai familia hiyo huku akieleza suala la nyumba ya familia hiyo kupigwa mnada haihusiki kwani iliyofanya hivyo ni kampuni za ufilisi iliyopewa jukumu hilo na Mahakama.

“Siwezi kueleza sana, tunawadai na nyumba yao kupigwa mnada imefanywa na taasisi ya ufisili waliopewa jukumu hilo na Mahakama kupata fedha za kulipa deni hili,” amesema.

Naye Ofisa kutoka taasisi ya Ngomeni iliyopewa jukumu la kupiga mnada nyumba hiyo, Kristian Samweli amesema walitekeleza amri ya mahakama baada ya mdaiwa kushindwa kulipa deni analodaiwa.

“Sisi tumeuza na tulifuata taaratibu zote zinazotakiwa ikiwepo kumpatia notisi ya kumtaka alipe lakini alishindwa, pia tuliwafahamisha viongozi wa Serikali za mitaa, juu ya kusudio la kuuza nyumba hiyo, kimsingi tuliiuza kwa Sh23 milioni baada ya kufuata utaratibu” amesema
Weka picha mkuu...muhimu sanaa 😀😄
 
Yeye alipewa Mkopo akaenda kutolea Fungu la Kumi
 
Riba ni 1 million Kwa mwaka ndani ya miaka mitatu deni limefika 17 million how?
Hilo kwakweli sio halisi lakini hatujui mkataba unasemaje.

Pengine ni milioni Moja kwa mwaka wa kwanza ambao unatakiwa urejeshe pesa yoote.Ikizihapo % inaongezeka kila mwezi.

Hawa wahuni wanaokopesha mikopo wanakuja na Maneno matamu lakini wanaficha vitu ndani ya mkataba ambavyo utakuja kushtuka pale unapodhani umemaliza deni harafu wanakwambia bado hichi na hichi.
 
Tukiwaambia Riba haifai mnatuona ss washamba hlf ni kanisa na waumini wake yni ndo uone sasa jinsi wagalatia walivokua hawana huruma na waumini wao

Laiti hii ingetokea kwa Waislamu comments zingekua zishafika 1000 uko ila kwasababu nyani haoni ............ basi wacha wamalizane wenyewe
Kwa nilivyosoma naona km kanisa halihusiki Moja Kwa moja!
Lkn pia kanisa halikumtuma akakope
 
Nina miaka 15 sijaingia kanisani. Huyu ni muumini, mtoa fungu la kumi kwa uhakika. Lakini leo ataishi kama mtumwa kwa kukosa makazi, kisa mkopo wa kutoka kanisani.
Sijaona km kanisa linahusika Moja Kwa moja
Ila ninachoona hapa ni dhuluma tu
 
Ttzo upo mbali na Uislamu sahihi

Mnashadidia sana Uislamu wa mitandao ambao sio sahihi
Kama wewe ambavyo unashadadia u-kristo usio sahihi!
U-kristo sahihi watu hawafanyi hivi!
Ss umeelewa, sio Kila anaejiita mchungaji, mkristo ana kanisa ni sahihi wengine wenzio tu km unavyoona huko kwenu!
Kwahiyo usijumuishe
 
Afisa mikopo nae katoaje pesa wakati mtu hana biashara
Lakini masharti yakikazwa pia wabongo utawasikia "mikopo hatupewi, masharti magumu"

Yakilegezwa ndio hivyo sasa. Namaanisha itabidi kila mmoja abebe jukumu lake. Responsibility. Ni wajibu wao kujua watalipaje na riba zina mahesabu gani. Ujinga kutojua ndio kosa lao hapa, na tokeo lake mateso yamejidhihiri.

Tukirudi kwenye wakopeshaji ukavaa viatu vyao. Ivi unajua kati ya 6M za mwanzo walilamba rejesho la laki tano tu😳. Na miaka inasonga tu. Huwaonei huruma biashara yao itaendaje?
 
Back
Top Bottom