Dar es Salaam: Nyumba yapigwa mnada kwa kushindwa kulipa milioni 7

Dar es Salaam: Nyumba yapigwa mnada kwa kushindwa kulipa milioni 7

Tukiwaambia Riba haifai mnatuona ss washamba hlf ni kanisa na waumini wake yni ndo uone sasa jinsi wagalatia walivokua hawana huruma na waumini wao

Laiti hii ingetokea kwa Waislamu comments zingekua zishafika 1000 uko ila kwasababu nyani haoni ............ basi wacha wamalizane wenyewe
Wagalatia ni watu gani mkuu.


YESU NI KRISTO
 
Hawa wajinga sijui tuwaeleze nn muelewe..
MKOPO SIO WA KUANZISHIA BIASHARA, MKOPO NI KWA AJILI YA KUENDELEZA BIASHARA..!!!asa endeleeni kujitoa fahamu mje kulia mbele..eti tunaomba mamlaka zitusaidie!!! idiot kabisa..hakuna atakusaidia hapo Kwa ujinga wako mchukua mkopo na mume wako..na ww mume inaonekana uyo mke ndio anakuongoza..
uko sahihi kabisa maana millioni 6 miaka mi3 dah !
 
shida sio COVID..shida ilianza pale alipochukua mkopo Kuanzia biashara yaan starting capital..mkopo sharti uwe wa KUENDELEZA biashara ambayo Tayar ipo unajua mzunguko wake ,unajua ups down zake...


Kuchukua mkopo na Kuanzishia biashara ni risk sana kama kuvamia kambi ya jeshi!!!!!?
hapo hapo walitoa kidogo wakaila nyingine wakalipia ada watoto[emoji1787][emoji1787][emoji1787]hiyohiyo pesa ya mkopo
 
Niseme mara ngapi?nitakaa nanyi mpaka lini enyi wenye imani haba?? Kuwa usikope kuanzisha biashara. Hasa hasa kwa kutegemea biashara hiyo ndo irejeshe mkopo. Kopa kuendeleza biashara.
Tatizo la Wabongo wanapenda sana biashara za kuigana,wengi hawana ubunifu wao kama wao!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Wabongo wengi kwenye masuala ya mikopo si waaminifu,wanasingizia korona kwani nchi yetu ilikuwa locked kama Kenya?
 
Niliona picha ya hiyo nyumba sehemu wahuni wamezurumu nyumba sio ya 7m ile hata familia wangeamua kuuza wenyewe huko kimara kwanza pana kiwanja kikubwa vile cha 7m daslm watu wezi sana....pana vitu tutavijua zaidi huko mbele...
hakuna kitu hapo kifupi wajipange upya tu ,hii ishu kwa nilivyosoma maelezo nimeelewa ishu hii imepita mahakamani na mahama lazima iliita pande zote mbili wakazisikiliza na mahakama wakatoa muda wahusika walipe na wahusika hawakufanya hivyo pili ilikaziwa hikumu hapo ndipo mahakama ikajirizisha kwa kutoa Amri ya kuuza dhamana zilizowekwa kufidia deni na gharama zote za ufunguaji wa kesi na kesi yenyewe vinalipwa na mkopaji .hivyo usitegemee jipya ilibidi mkopaji afungue kesi kabla nyumba haijauzwa labda kidogo pangekua na uchelewaji wa amri ya mahakama .kifupi dawa ya deni ni kulipa hakuna ujanja mwingine na kabla ya kukopa soma vizuri mkataba
 
Wabongo wengi kwenye masuala ya mikopo si waaminifu,wanasingizia korona kwani nchi yetu ilikuwa locked kama Kenya?
Mbona hata Serekali yetu nayo pia inasingizia Corona na Vita vya Ukraine imesababisha vitu kupanda bei!? Yaani uzuri wa Mtanzania huwa hakosi sababu ya kusingizia!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
watu wengi wanaochangia hawaionei huruma hiyo kampuni iliyotoa pesa wao wanoionea huruma familia iliyouziwa nyumba tu !hivi millioni 6 kwa miaka mitatu wamepeleka rejesho moja tu?hivi watu walitakeje hapo kampuni ifanyeje ?
Hao wamiliki wa nyumba ni matapeli kama matapeli wengine kwa kitendo tu mke kwenda kukopa badala mme au wote kwa pamoja mme akiongoza utaiona janja yao
 
Dar es Salaam. Familia ya Festo Aaron, inayoishi Kimara Bonyokwa iko njia panda baada ya kukosa makazi kutokana na nyumba yao kupigwa mnada na taasisi ya Uwezo Financial Service kwa kushindwa kurejesha deni la Sh7 milioni.

Mwaka 2020 familia hiyo yenye watoto watano ilikopa Sh6 milioni katika taasisi ya Uwezo inayodaiwa kuwa na uhusiano na waumini wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) kwa makubaliano ya kurejesha Sh7 milioni ndani ya mwaka mmoja.

Taasisi hiyo imekuwa ikikopesha fedha hizo kwa kuzingatia sifa mbili, ambazo ni mkopaji awe muumini wa dhehebu hilo awe mwaminifu katika kutoa fungu la kumi kila mwaka.

Akizungumza na Mwananchi, Festo alisema mwaka 2020, mke wake Happy Josia alikopa kwenye taasisi hiyo Sh6 milioni lengo wakipata fedha hizo wapate mtaji wa kuanzisha biashara.

“Makubaliano yalikuwa kurejesha riba ya Sh1 milioni kwa kiasi tulichokopa, tulitakiwa kurejesha Sh7 milioni ndani ya mwaka mmoja,” alisema Festo.

Amesema fedha hizo walizielekeza kwenye biashara ya nguo na viatu katika duka waliloanzisha maeneo ya Kimara lakini hata hivyo janga la Uviko-19 lilotokea kwa mwaka huo lilisababisha biashara yao kwenda mrama.

“Tulipambana na kufanikiwa kufanya rejesho moja Sh500,000 lakini hata hivyo mambo yalizidi kwenda ovyo ndipo tulipoenda kufanya mazungumzo na taasisi kuwaeleza hali halisi na wakatuongezea muda,” amesema.

Festo amesema miezi michache baadae walipotaka kwenda kulipa deni hilo waliambiwa riba imeongezeka hadi kufikia Sh10 milioni kutoka Sh7 milioni jambo lilowashangaza na kwenda kwa wachungaji wa Kanisa hilo lakini hata hivyo hawakupata msaada.

“Hadi mwanzoni mwa mwaka huu tuliambiwa deni riba yake imefikia Sh17 milioni hivyo tulishangaa na kuwauliza imefikaje? Wakawa hawataki mazungumzo tena ndipo wakaanza kutangaza mnada nyumba yetu na wakauza kwa Sh 23milioni,” amesema.

Happy ambaye ndiye aliyekopa amesema anashangazwa na uharaka wa kuiuza nyumba hiyo.

“Tunaziomba mamlaka kuongea na taasisi hii ikubali kutuachia nyumba yetu na iridhie kurejesha deni la msingi la Sh7 milioni tulilokopa ili tuendelee na maisha,”amesema.

Mwananchi, lilizungumza na Mchungaji wa kiongozi wa Kanisa la TAG Kimara, Ruth Temu amesema taarifa za familia hiyo kukutana na kadhia hiyo alishazipata na ana mpango wa kwenda kuzungumza nao.

“Siwezi kusaidia chochote kuhusu hili sakata japo taasisi iliyokopesha naijua lakini masharti waliyokubaliana siyajui kwa hiyo siwezi kuwasaidia chochote,” amesema Temu.

Alipotafutwa ofisa mikopo wa taasisi ya Uwezo, Patro Mwashambwa alikiri kuidai familia hiyo huku akieleza suala la nyumba ya familia hiyo kupigwa mnada haihusiki kwani iliyofanya hivyo ni kampuni za ufilisi iliyopewa jukumu hilo na Mahakama.

“Siwezi kueleza sana, tunawadai na nyumba yao kupigwa mnada imefanywa na taasisi ya ufisili waliopewa jukumu hilo na Mahakama kupata fedha za kulipa deni hili,” amesema.

Naye Ofisa kutoka taasisi ya Ngomeni iliyopewa jukumu la kupiga mnada nyumba hiyo, Kristian Samweli amesema walitekeleza amri ya mahakama baada ya mdaiwa kushindwa kulipa deni analodaiwa.

“Sisi tumeuza na tulifuata taaratibu zote zinazotakiwa ikiwepo kumpatia notisi ya kumtaka alipe lakini alishindwa, pia tuliwafahamisha viongozi wa Serikali za mitaa, juu ya kusudio la kuuza nyumba hiyo, kimsingi tuliiuza kwa Sh23 milioni baada ya kufuata utaratibu” amesema
Kama wanawatoto hakuna mtoto hapo atayekuwa anaenda kanisani tena na utopolo wa dini ndio umeishia hapo.
 
Back
Top Bottom